Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya waumini wa wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory Of Christ Tanzania Church).
Waumini hao walikuwa wanaandamana kwenye njia ya Morogoro Road wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali.
Baadhi ya mabango ambayo yameoneka yakiwa yameshikiriwa na waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima) lililopo eneo la Ubungo leo Juni 15, 2025 yakiwa na jumbe mbalimbali.
Ikumbukwe Waumini hao wamekusanyika eneo la umbali wa takribani mita 300 tokea lilipo Kanisa hilo ambalo limezungukwa na askari, ambapo wamefanya maombi na kuimba nyimbo kabla ya kuanza kuelekea eneo la Kanisa ambapo wametawanywa kwa milio ya risasi ambazo zilifyatuliwa juu na askari Polisi.
Awali kabla ya waumini kuanza maandamano, Jeshi la Polisi liliwataka watawanyike eneo hilo, lakini waamini wanasisitiza kuwa wamekuja kusali.