John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Jeshi la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam limewakamata matapeli sugu wa viwanja kwa tuhuma za kujipatia Tsh. milioni 100 kwa njia ya udanganyifu, wakijifanya wanamiliki na kuuza viwanja vya makazi ambavyo siyo vyao.
Matukio waliyoyafanya yametokea kati ya mwezi Januari na Februari 2022.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salam, Muliro Jumanne amesema watuhumiwa hao 11 akiwemo mwanamke wamekamatwa maeneo ya Goba Kinondoni baada ya kuwatapeli Masista wa Kanisa Katoliki Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Maria Kipalapala, Tabora.
Watuhumiwa hawa watafikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi. “Jeshi la Polisi linawaomba Wananchi waendelee kutoa taarifa mbalimbali ili zifanyiwe kazi na vitendo vya kihalifu viweze kupungua,” amesema Muliro.