Polisi yawakamata watu 632 kwa kuvunja sheria ndani ya wiki tatu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam:

Kufuatia kikao cha ujirani mwema cha tarehe 18 Machi 2022 ndani ya Kanda No. 2 inayohusisha mikoa ya Kipolisi Ilala, Temeke, Kinondoni, Pwani na Rufuji, pamoja na mambo mengine Makamanda wa Mikoa hiyo walikubaliana kufanya Operesheni ndani ya Kanda hiyo. Amri ya Utendaji Namba 6 ya mwaka 2022 iliandaliwa tarehe 21 Machi hadi 08 April 2022 kwa lengo la kuzuia na kupambana na uhalifu wa makosa makubwa kama ifuatavyo;
  • Makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha
  • Makosa ya wizi wa Magari, pikipiki na bajaji.
  • Makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu
  • Makosa ya madawa ya kulevya ( ya viwandani na ya shambani)
  • Makosa ya uvunjaji na kuiba.
  • Wizi wa Mifugo.
Katika kipindi cha operesheni hii kumekuwa na mafanikio makubwa ambapo jumla watuhumiwa 632 walikamatwa, silaha/bunduki za moto 5, Pistol bandia 1 na risasi 53, Magari 9 Pikipiki 65 za wizi, mitambo ya kutengezeza gongo 15, pipa 70 zenye kimea cha kutengenezea gongo na lita 773 za Gongo, madawa ya kulevya ya viwandani (Heroini kete 88 na Gramu 250) na Bhangi; Gunia 31, Puli 520, Kete 5695 Misokoto 1726, Hekari 6 za shamba la Bhangi, kilo 46 za mbegu za Bhangi na Mirungi Kg 4.5, jino la Tembo, vyombo mbalimbali na vifaa vya kielektoniki vilivyotokana na matukio ya uvunjani nyumba pia vilipatikana.

Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
 
Hii taarifa inafikirisha sana kati ya hao lazima wapo na waliobambikiziwa kesi wasizozijua mwanzo wake Wala mwisho wake na kuteswa sana ili wakiri makosa wasiyoyatenda
 
Ndio ulivyo kariri.
 
Back
Top Bottom