Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
Gadafi ni zaidi coz harakati zake zililenga kukomboa walibya na Africa kwa ujumla wakati Nelson yeye aliegemea kwa wasauzi zaidi
 
Sisi ni wepesi sana wa kusahau. Kweli Gaddafi kwetu ni shujaa au msaliti. Mwaka 1978 majeshi yake na rafiki ya Idd Amini Dada yaliua ndugu zetu wasio na hatia mkoani Kagera, bado ni shujaa kwenu. Kwangu Gaddaf alipata haki yake.
 
Mkuu naumia sana mnapolinganisha MANDELA na mwanasiasa yeyote duniani. Mtu kafungwa 27, lakini kasamehe waliomfunga! Kakaa madarakani muhula 1tu!! MANDELA hana mpinzani duniani.
Chunguza kidogo kitu inaitwa Mandela Effect (Ni ya kutisha kidogo, far fetched.. Ila nzuri kuijua)
 
Mimi namuona shujaa Mandela kwa kusamehe

Ni jambo ambalo binaadamu wachache sana wanaliweza
Unless you were not the one jailed!
Yaani at the weakest point in life.. Mandela anatoka jela.. Amenyong'onyezwa kisha anapewa Taifa?!

Halafu mtu mwenye ideal tofauti kabisa na serikali iliyopo anatumika only one term anaachia.. Preaching umoja na sio usawa.. Wakati lengo lao mwanzo lilikuwa ni kurejesha usawa kwanza...

Mandela is a big mystery.
 
Mkuu naumia sana mnapolinganisha MANDELA na mwanasiasa yeyote duniani. Mtu kafungwa 27, lakini kasamehe waliomfunga! Kakaa madarakani muhula 1tu!! MANDELA hana mpinzani duniani.
mandela ni diplomasia mzuri lkn hakua Wanaharakat ni hawa kina nyerere,,gadafi wameshirikiana sana na cheguavara kukomboa africa
 
Sisi ni wepesi sana wa kusahau. Kweli Gaddafi kwetu ni shujaa au msaliti. Mwaka 1978 majeshi yake na rafiki ya Idd Amini Dada yaliua ndugu zetu wasio na hatia mkoani Kagera, bado ni shujaa kwenu. Kwangu Gaddaf alipata haki yake.
Hapa wanamsifia ni ndugu zake wa dini fulani ila ata mm nilifurahi sana huyu shetani alivyoondolewa duniani kwa aibu
db577f452746486ebb8b47d264509235.jpg
huyu alifazili kutunguliwa ndege ya french ikauwa watu wasiyo na hatia alimpa iddi amini dada wanajeshi na vifaa auwe ndugu zetu hapa tanzania alafu kuna watu wanamuita shujaa wa kutete waafrika huyu ni shetani tu labda akumbukwe kwa kusambaza dini yake afrika
 
..waTz hatupaswi kumsifia mtu aliyetoa roho za askari wetu ktk vita vya Uganda.

..Ndiyo maana vijana wa kiTz mnadharaulika kwasababu mnakurupuka kujadili mambo mazito lakini hamsomi.
Zungumza ukweli kama uonekavyo in its purest form na uwe SPECIFIC ktk subject husika.,Hii issue ya ghadaffi kuua askari wa Tz tambua ilikua ni vita,kwani nyerere hajazisaidia nchi za kusini mwa africa kujikomboa na kupata uhuru kutoka kwa wakoloni tena KIJESHI??.,So stick to the Question yupi bora na sio kumkosoa mtu kwakua kuna suala la kitaifa
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.


vijana wa sikuhizi huenda hawakumruka kumsoma Hendry kisinja kwenye kuisoma vita ya uganda na tanzania kama wewe, unaezeeka kwa kuruka ruka ndo maana unataka kufinda watu ujinga wako.....
 
mandela media tu za wazungu ndio zinambeba hana alichofanya africa izo ni propaganda za makaburu tu baada ya kuachiwa uchumi
 
Bado kidogo tu watu wataleta mada ya nani shupavu kati ya Mungu na Shetani. Alieleta uzi huu naona alivuta bange kwanza ndo akaleta hii maada. Moja ya madikteta waliotisha duniani ni pamoja na Gaddafi, kawateketeza wapinzani kwa mitutu ya bunduki na wengine walizikwa mwenye makaburi ya halaiki na kufukiwa na makatapila wakiwa hai.Vita ya Kagera alimletea Iddi Amin silaha kali za maangamizi ili kuja kuwateketeza Watanzania.Alikuwa kiongozi pekee duniani aliekuwa anasafiri na chakula chake kwenye ziara za kiserkali akiamini kuwa vyakula vya ugenini vina najisi !!!.Alibeba pia mahema yake ya kulalia akiamini ikulu za wenzake anakoenda si salama au kuna najisi !!!. Misaada ya kimaendeleo aliyokuwa anatoa Gaddafi kwa wanainchi wake hazikuwa pesa zake mfukoni bali ni utajiri wa mali ya asili ya Libya hasa wingi wa mafuta.Gaddafi alichukiwa na duniani nzima ndio maana baada ya kuuawa Walibya wote walishangilia kwa nguvu.Maraisi wote duniani hakuna hata mmoja alienda kwenye msiba wake, alizikwa na watu wasiozidi kumi ambao ni wa familia yake tena sehemu isiojulikana.Watu wanafananisha kifo cha Gaddafi na mbwa alietupwa.Wanaomwona Gaddafi shujaa hadi afananishwe na Mandela wanapaswa kupimwa akili zao.Gaddafi alitesa watu na kuona vitu vya wenzake ni najisi, malipo ya Mungu yapo hapa hapa duniani kwani nae alikufa kifo cha aibu kuliko raisi yeyote duniani, aliifuata najisi ya maji machafu kwenye bomba alimokimbilia kujificha, hakuona sehemu yeyote salama zaidi ya bomba la maji machafu !!!.Alieleta uzi huu aufute mara moja maana ni aibu kubwa kumwita huyu shetani shujaa.
 
Back
Top Bottom