Bado kidogo tu watu wataleta mada ya nani shupavu kati ya Mungu na Shetani. Alieleta uzi huu naona alivuta bange kwanza ndo akaleta hii maada. Moja ya madikteta waliotisha duniani ni pamoja na Gaddafi, kawateketeza wapinzani kwa mitutu ya bunduki na wengine walizikwa mwenye makaburi ya halaiki na kufukiwa na makatapila wakiwa hai.Vita ya Kagera alimletea Iddi Amin silaha kali za maangamizi ili kuja kuwateketeza Watanzania.Alikuwa kiongozi pekee duniani aliekuwa anasafiri na chakula chake kwenye ziara za kiserkali akiamini kuwa vyakula vya ugenini vina najisi !!!.Alibeba pia mahema yake ya kulalia akiamini ikulu za wenzake anakoenda si salama au kuna najisi !!!. Misaada ya kimaendeleo aliyokuwa anatoa Gaddafi kwa wanainchi wake hazikuwa pesa zake mfukoni bali ni utajiri wa mali ya asili ya Libya hasa wingi wa mafuta.Gaddafi alichukiwa na duniani nzima ndio maana baada ya kuuawa Walibya wote walishangilia kwa nguvu.Maraisi wote duniani hakuna hata mmoja alienda kwenye msiba wake, alizikwa na watu wasiozidi kumi ambao ni wa familia yake tena sehemu isiojulikana.Watu wanafananisha kifo cha Gaddafi na mbwa alietupwa.Wanaomwona Gaddafi shujaa hadi afananishwe na Mandela wanapaswa kupimwa akili zao.Gaddafi alitesa watu na kuona vitu vya wenzake ni najisi, malipo ya Mungu yapo hapa hapa duniani kwani nae alikufa kifo cha aibu kuliko raisi yeyote duniani, aliifuata najisi ya maji machafu kwenye bomba alimokimbilia kujificha, hakuona sehemu yeyote salama zaidi ya bomba la maji machafu !!!.Alieleta uzi huu aufute mara moja maana ni aibu kubwa kumwita huyu shetani shujaa.