Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
Ghadafi alikuwa anti imperialist na marafiki zake wakubwa walikuwa Fidel Castro, Chavez,morales na ndio maana Omar all bashir anamchukia sana gadaffi hata kifo cha Gadafi ,Al bashir alifurahi sababu gadaffi alikuwa ana destabilize Sudan kwa kuwafadhili akina Garang akidai Bashir ni imperialist japo alikuwa na motive zingine kuona Sudan ingekuwa super power.Mpaka s.Sudan inapata Uhuru ni kwasababu ya kazi kubwa ya Gadaffi

Ishu ya Uganda Gaddafi aliona Tanzania ni imperialist ina occupy sehemu isiyo yake japo alikengueka na kuomba msamaha baadae

Ila ukizungumzia liberation Gaddafi katoa pesa nyingi kumsaidia Mandela na marafiki zake wa karibu mno walikuwa Chavez, Castro anti imperialist wenzake wenye muono sawa na pindi Mkutano was UN ukifanyika Gaddafi alikuwa anaenda pamoja na Chavez NY .na Chavez kwenye moja ya hutuba zake alikuwa ana mchambua Gaddafi na liberation na mipango yao ya kuunganisha afrika kama ilivyo s.America

Wote ni mashujaa wa Africa ,
Gaddafi kapigania South ,kapigania Uhuru wa s.Sudan nk .

Mandela kakaa sana jela japo ni inspirational ila gadaffi ,samora ,nyerere walipigania ya wa Africa wote





3ef6133357177cedae31aedb8aec4b66.jpg
Mkuu nimependa uchambuzi wako
 
Mandela hakuisaidia Afrika bali alisaidiwa na Afrika. Walioisaidia Afrika wapo akina Nyerere kwa hamasa (solidarity) na Ghadafi kifedha.

Mandela ana umaarufu uliokuzwa na wazungu kwa uamuzi wake wa kuwaachia wazungu ardhi waliyokuwa wameipora na kuwaacha waafrika wenzake wakiteseka.

Lakini kwa kuwa bado tunaishi katika hangover ya anti-apartheid iliyoyokea huko SA, tunamwabudu Mandela zaidi ya waliopambana kwa fedha na damu kumkomboa Mandela.

Kwa hiyo Ghadafi na Mandela hawapaswi kulinganishwa kwani hawatalingana kamwe. Mmoja alitafuniwa na waliokuwa wapambanaji huko nje, mwingine alipindua nchi akiwa na miaka 30 akaijenga ikafikia viwango vya ulaya kimiundombinu. Ghadafi alibugi kipengele kimoja tu cha haki za binadamu.
 
Nyerere alifanya makubwa sana kuliko hao wawili sema tu hakupewa promo.najua mtabisha sana ila someni tena historia mtajua kwanini tulikuwa masikini sana.mtagundua ni misaaada tuliyowapa wenzetu na juhudi za kuunga jangea la sahara kuwa nchi moja ndio limechangia
 
Mtasema huyu Bora yule sio bora kipimo hicho kinapimwa ndani ya nchi zao nini wamefanya na uhusiano wa kimataifa.. Afrika kusini ishajitia dosari kwa kubagua waafrika wenzao Tena kufikia hatua ya kuwauwa!! Nawachukia wao na hata mashujaa wao!
 
Kukaa jela ndo awe mwamba!? Acha kumlinganisha Gadaffi na vitu vya ajabu
 
Shujaa wa Africa ni Tata Nyarusare! Wa Kamunyonge Bi-afra.jirani na Green Bar.
 
Na kuvaa jezi ya Bafana Bafana ktk African Cup of Nations 1996
Kati ya hao uliowataja nitamchagua Gaddafi. Ikiwa utataka nimtaje aliye na mchango mkubwa kwa Africa wote ntamtaja namba moja Nyerere na namba mbili Lumumba.

Mandera hana la maana kwa Africa zaidi ya kukaa jela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mandela nasikia wazungu walimnyongonyesha kwa kumuonesha gerezani kila aliyekuwa nae bega kwa bega kuwa amewafuata wazungu walimfanyia hivyo mpaka anatoka alikuwa anaona hakuna mtu wa kuitetea afrika ,
alipopata madaraka akaamua kuwashirikisha hao hao wazungu bila kinyongo.
gadafi alitumia sehemu ya utajiru wake kuikomboa afrika(alijaribu lkn hakuweza)
Kuikomboa Afrika ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa alikuwa ni mbaguzi wa kidini wa kiwango cha juu, na alikuwa anatumia mali zake kushawishi na kuwahonga baadhi ya viongozi ili kuibadilisha Afrika kuwa ya dini moja. Huo umoja wa Afrika aliokuwa anazungumzia ni Tofauti na ile ya NKURUMAH na NYERERE yeye alikuwa kwenye mrengo wa kidini , ndio sababu kuu ya kumpa sapoti NDULI wakati wa vita ya kagera akiamini kuwa bongo ndio ilikuwa kikwazo kwa baadhi ya sera zake mbovu
Tupe ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom