Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
..nawahurumia.

..hawajui kazi aliyofanya Brigadier.Muhidin Kimario kuamrisha mapambano dhidi ya askari wa Gaddafi.

..na Walibya walishaanza kutuelemea na ilikuwa almanusra tushindwe vita ile.
hiyo vita si mlikuwa mnatumika tu na mabeberu...idd amin alikuwa mzalendo!!
 
hiyo vita si mlikuwa mnatumika tu na mabeberu...idd amin alikuwa mzalendo!!

..hapana.

..hata silaha mabeberu wa Uingereza walikataa kutuuzia.

..msaada wa nje tulioupata ulitoka Algeria, walituletea meli ya silaha.

..na Msumbiji walituma kikosi cha askari kuja kutusaidia.

..kuna taarifa Zambia walitusaidia lakini sina uthibitisho wa hilo.

..Mabeberu walitamani tushindwe ili tusiweze kusaidia ktk vita vya ukombozi kusini mwa Afrika.
 
Not true mkuu, kafungue upya makabrasha...nyerere alitumika tu!!..propaganda za miaka ya sabini hazifanyi tena kazi sasa, watu wamezinduka!
 
Not true mkuu, kafungue upya makabrasha...nyerere alitumika tu!!..propaganda za miaka ya sabini hazifanyi tena kazi sasa, watu wamezinduka!

..ukweli ndio huo niliokwambia.

..Mabeberu walitamani tushindwe vita ile.

..walitishika na ushindi wa Frelimo dhidi ya mabeberu na wakoloni wa Kireno.

..na Frelimo walipigana wakitokea ktk makambi yao yaliyokuwa Tanzania.

NB:

..kwani Iddi Amin alifanya jambo gani kwa Waafrika mpaka umuone wa maana?
 
Kwa uonavyo wewe kati ya colonel Muammar Gaddafi au Nelson Mandela (Tata Madiba) nani shujaa/mwamba wa Afrika?

View attachment 534066

Ninaomba tusimuongelee mwalimu Nyerere kwa maana yeye nafasi yake kwa Afrika haina mpinzani.
Gaddafi gani? Yule aliyesaidia Nduli Idi Amin Dada kuvamia nchi yetu Tanzania mnamo 1978/1979?
Gaddafi gani? Yule aliye mastermind mauaji na kuteketeza roho za abiria 270 wasiokuwa na hatia waliokuwa ktk ndege ya PAN AM 103 mnamo mwaka 1988 kunako Lockerbie?
Sema, Gaddafi gani?
 
Copy & Paste!
Bora hata ungetumia muda wako kufanya tafsiri kwa Kiswahili, angalau ungeonekana wa maana.
 
Tetesi za Zambia kutusaidia zipo , kumbuka sisi pia tuliwasaidia sana Zambia mwaka 1967 wakati wamewekewa vikwazo vya kununua mafuta na kusafirisha copper, (south Rhodesia), Zambia walikuwa wanasafirisha copper kwenye Ndege kuleta Dar , na wakawa wanarudi na mapipa ya mafuta kutoka hapa infact Zambia ndio walisaidia ujenzi wa Airport ya Mtwara maana walitaka watumie bandari ya Mtwara kusafirisha copper yao, vikwazo vilipoondolewa ndo na mradi ukafia hapo
 
Mkuu, hii inaitwa tit-for-tat. Umemuuliza swali zuri sana bro.
Lazima aje atuambie sio kutoa maneno ya kijiweni tu kama tunashangilia mechi ya lipuli na pamba.

Kwa Afrika na ukubwa wake ..kuna mafanikio ya wazi unaweza kuyaona au kuyasikia yanayohusiana na Ghadaffi ... Kuanzia west Afrika mpaka East.. Birth to south.

Ukiachilia diplomasia ya ukipigwa shavu la kushoto geuza la kulia ..Mzee Madiba alifanya nn!? Xenophobia na Ubaguzi wa wao kwa wao unaoendelea leo ni zao la incompetent leadership..

Wazungu walitaka kugeuza focus ya waafrika kucelebrate our true successful leaders(heros) kwa kumfanya Mandela kuwa Hero.. mzungumzaji na si Mtendaji... Asijetaka confrontation ..Nani atakupa heshima!? Heshima toka kwa aliyekudharau akakutukana, akadhulumu akakuibia hauiombi ..Unaichukua..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uonavyo wewe kati ya colonel Muammar Gaddafi au Nelson Mandela (Tata Madiba) nani shujaa/mwamba wa Afrika?

View attachment 534066

Ninaomba tusimuongelee mwalimu Nyerere kwa maana yeye nafasi yake kwa Afrika haina mpinzani.
Gaddafi is best in africa huwezi kumfananisha na mandela hata kidogo.

mandela kawahakikishia wazungu kuwa maslahi yao yataendelea kuwa salama( kawauza watu wake) huku yeye na familia yake wakihakikishiwa neema.mandela hata nyerere hamfikii.

Gaddafi ni mpambaji wa kweli aliyesimamia maslahi ya watu wake na waafrika wengine kadri awezavyo na alikua na mapenzi ya kweli na africa na waafrica, na alionesha wazi kukerwa na unyonyaji wa westerners kwa bara la africa. Ukiona westerners wana mpamba sana muafrika hujue huyo kuna mahali wana msalahi nae. R.i.p son of africa.
 
Gadafi next level.
Umaarufu wa Mandela umetokana na kupigiwa debe na wazungu baada ya kuwakumbatia.





MAGUFULI4LIFE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…