Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?

  • Total voters
    244
Gaddafi alijitahidi sana kusaidia Africa, sema ndio hivyo baadae wakubwa waliona ni kikwazo kwa maslai yao! Mandela alipata zaidi umaarufu hasa kwa msamaha wake kwa makaburu licha ya kuwekwa jela kwa miaka kibao! Kwangu mimi Gaddafi ni zaidi ya Mandela
Na ule msamaha si baada ya kusukwa huko gerezani..!!!! Toka lini mzungu akampenda mwafrika kama hana maslahi?
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Mkuu,
Kuna baadhi ya watu huwa wanatao majawabu au maoni yao kwa jicho la dini,hili naliongea baada ya kuwa na mjadala kuhusu hili na vijana wenzangu Miaka ya nyuma.

Vijana wengi historia ya vita ya kagera hatuijui sana.
 
1) gaddafi ni shujaa anaejielewa na alikuwa na msimamo mmoja juu ya wanyonyaji wake,anaongea anachohisi na ukweli mtupu.
2) mandela alikuja kufanywa mwanasiasa akawa anaongea kisanii na kisiasa kamaq anavyotarajiwa kuongea ili apendeze kwa wanyonyaji wake,kama kawaida yetu waafrica, ndio mana afirica ni shamba la bibi, wamiliki wake hawapo africa
Mzungu toka lini akampenda mwafrika kama hana maslahi naye? Gadaffi na Mandela aliyetoka jera ni vitu viwili tofauti.
 
Kati ya hao uliowataja nitamchagua Gaddafi. Ikiwa utataka nimtaje aliye na mchango mkubwa kwa Africa wote ntamtaja namba moja Nyerere na namba mbili Lumumba.

Mandera hana la maana kwa Africa zaidi ya kukaa jela.
Atakayekupinga ana MAPEPO makali sana, na ni mtu ambae ni MZITO SANA KICHWANI. Ukitaja Mchango wa Afrika utamtaja Hayat Nyerere, ubaya ni kwamba hakuna kumbukumbu zake muhimu.

Madiba ni nothing kwa Afrika ila kwa wazungu ni shujaa, jamaa aliamua kuikabidhi SA kwa wazungu baada ya kutoka jela.
 
Swali la mleta hoja ni nani ni mwamba wa Africa?? Sasa hapo Amani ,busara na hekima zimesaidia vipi Africa kama utamfananisha na Gaddafi aliyekuwa aaisaidia AU na nchi za kiafrica kiuchumi ???
Msamehe bure, hawa ndio wanaoiwekaga ccm madarakani tanzania. Eti Gadaffi anafananishwa na Mandela!!!
 
Swali la mleta hoja ni nani ni mwamba wa Africa?? Sasa hapo Amani ,busara na hekima zimesaidia vipi Africa kama utamfananisha na Gaddafi aliyekuwa aaisaidia AU na nchi za kiafrica kiuchumi ???
Akili yako ni ya Kibashite, Mandela kaongoza miaka 5 tu tena ambapo nchi ndiyo imepata uhuru pekee, Gadaffi miaka 42, S.A na Libya wapi penye maendeleo? Note mchango wa amani, busara, hekima na maarifa ni mkubwa kuliko mchango wa fedha.
 
Atakayekupinga ana MAPEPO makali sana, na ni mtu ambae ni MZITO SANA KICHWANI. Ukitaja Mchango wa Afrika utamtaja Hayat Nyerere, ubaya ni kwamba hakuna kumbukumbu zake muhimu.

Madiba ni nothing kwa Afrika ila kwa wazungu ni shujaa, jamaa aliamua kuikabidhi SA kwa wazungu baada ya kutoka jela.
Umenena vyema. Madiba ndio maana anapewa sifa sana na wazungu kwa kuwa hakugusa maslahi yao ya kiuchumi na kijamii huko SA. Wazungu waliendelea kuwa wamiliki wa uchumi na pia 1st class citizens.

Lakini kwa upande wa Africa hakuna hata nchi moja aliyowahi kuisaidia.sasa inakuwaje leo tumtaje kama HERO wa Africa!!!!
 
Back
Top Bottom