Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
Mimi namuona shujaa Mandela kwa kusamehe

Ni jambo ambalo binaadamu wachache sana wanaliweza
 
Kila mmoja ni shujaa wa wakati wake, lakini niko na ghadafi mwanafunzi mtiifu sana wa gamaliel nasser mkombozi wa waarabu na baba wa suez canal
 
Gadaffi alitoa msaada mkubwa kwa Tata Madiba enzi hizo, ila Mandela alimtupa Gadaffi at the time of need
 
Ghadafi alikuwa anti imperialist na marafiki zake wakubwa walikuwa Fidel Castro, Chavez,morales na ndio maana Omar all bashir anamchukia sana gadaffi hata kifo cha Gadafi ,Al bashir alifurahi sababu gadaffi alikuwa ana destabilize Sudan kwa kuwafadhili akina Garang akidai Bashir ni imperialist japo alikuwa na motive zingine kuona Sudan ingekuwa super power.Mpaka s.Sudan inapata Uhuru ni kwasababu ya kazi kubwa ya Gadaffi

Ishu ya Uganda Gaddafi aliona Tanzania ni imperialist ina occupy sehemu isiyo yake japo alikengueka na kuomba msamaha baadae

Ila ukizungumzia liberation Gaddafi katoa pesa nyingi kumsaidia Mandela na marafiki zake wa karibu mno walikuwa Chavez, Castro anti imperialist wenzake wenye muono sawa na pindi Mkutano was UN ukifanyika Gaddafi alikuwa anaenda pamoja na Chavez NY .na Chavez kwenye moja ya hutuba zake alikuwa ana mchambua Gaddafi na liberation na mipango yao ya kuunganisha afrika kama ilivyo s.America

Wote ni mashujaa wa Africa ,
Gaddafi kapigania South ,kapigania Uhuru wa s.Sudan nk .

Mandela kakaa sana jela japo ni inspirational ila gadaffi ,samora ,nyerere walipigania ya wa Africa wote





3ef6133357177cedae31aedb8aec4b66.jpg
Said like a professional
 
Kwanza mtoa mada naona kama kafananisha Daud na Goliath Mandela hajaifanyia chochote Africa no kosa kubwa kumfananisha na hili jabali la Africa gaddaf hakupigania nchi yake tu Bali na Africa kwa ujumla kwa Mali na fikra na ushaur alitaka kuunganisha nchi za kiarabu lakin akaona waarabu ni wanafiki wakubwa akaona Africa ndio asili yangu akaachana nao Mimi naweza kufananisha Gaddafi vs nyerere japo Tanzania hatukua na fedha ila tungekua na fedha nyerere angeitumia kuikomboa africa
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Nadhani wengi hawamjui vizuri huyu Ghadaffi mkuu. Si mtu mzuri kama wamfikiriavyo.
 
Gaddafi shujaa kwa wananchi wa Libya japokuwa na Mandela kwa Afrika Kusini pia. Kila mmoja alipigania maslahi ya taifa lake. Ushujaa wao unatafsiri tafauti kulingana na mtazamo wa mtu.
Ni vyombo vya habari hasa za magharibi vilivyompatia umaarufu mkubwa Mandela baada ya kuona aibu na kujua hawana cha kupoteza wakimuachia huru. Gaddafi anachukiwa na nchi za magharibi.Zaidi ya hapo ni ushabiki tu.
 
Gaddafi huyo Mandela ni kibaraka wa mabepari tu
 
Vijana wa kikosi kazi cha zamani, Gaddafi ana nafasi kubwa katika Bara la Africa pamoja na viongozi wakuu wengine kama vile, nyerere. Inkrumah, abde nasser, kaunda, haile Selassie, kamuzu banda, huyo Mandela anakwezwa na mabeberu kwa kuwa aliwahurumia makaburi ambao ni wazungu, kama kuumia Tanzania imeumia Sana kukomboa nchi za kusini ya Bara la Africa wakati huo Mandela yupo jela, Mandela aliulizwa na waandishi wa Habari 1994 dsm, je Nani kama nyerere alijibu huyu kanjfunza ujasiri na kwa Africa huyu ni baba wa Africa huru,
 
Bila fidel castrol nyerere kadaffi and many mores freedom fighter's mpaka hii leo wengekuwa wanapigwa bakora hao south Africas
 
Mkuu naumia sana mnapolinganisha MANDELA na mwanasiasa yeyote duniani. Mtu kafungwa 27, lakini kasamehe waliomfunga! Kakaa madarakani muhula 1tu!! MANDELA hana mpinzani duniani.
 
Jibu ni rahisi tu
Anayechukiwa na wazungu ndo shujaa wa Africa
Anachukiwa na wazungu sababu ya udikteta, mauaji ya watu wasio na hatia na kukosa diplomasia. Marekani na Ulaya hawapendi hayo mambo kabisa.
Alafu unajua wazungu walimfunga Mandela miaka mingapi?
 
Ebu muacheni jaman colonel kadaffi eboo..kukaa jera ndoo sifa... Kaddafi ni mmoja ya watu waliokuwa mstari wa mbele kwa Mandela kuwa free
 
Mkuu naumia sana mnapolinganisha MANDELA na mwanasiasa yeyote duniani. Mtu kafungwa 27, lakini kasamehe waliomfunga! Kakaa madarakani muhula 1tu!! MANDELA hana mpinzani duniani.
Huo u shujaa ni wa nchi yake tunazungumzia mwamba wa africa ni nani hivi ww mandela unaweza hata kumfananisha na nyerere
 
Back
Top Bottom