Hivi ninyi mnaojifanya kuja na majina ya kichaga na kuingiza masuala ya ukristo katika propaganda zenu mnadhani wote humu ni wajinga.
Ni wazi nia yenu ni kuwadanganya watu kuwa ninyi ni CHADEMA ama wafuasi wa Dr Slaa wakati sio hivyo. Ni wachochezi wakubwa.....Nia yenu ni kuendeleza hizi siasa za udini kwa faida yenu na sio CHADEMA wala Dr Slaa.
Hi inafanana na baadhi ya sms na email messages zilizozagaa ambazo naamini kuwa nazo ama baadhi yake zina malengo kama haya.....
Moderator, nashauri mfunge mlango wa uanachama humu hadi baada ya uchaguzi.....Hiyo itasaidia kuwadhibiti wale walioshajiunga endapo watathubutu kuendeleza huu upupu lakini pia kuwazuia hawa wanaoingia kwa ajili ya kuendelea kuwafitinisha na kuwagombanisha watanzania...
Angalia huyu amejiunga leo tayari anamwaga upupu akijifanya kumunga mkono luteni.....