POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

Hapo kwenye"labda"
 
Uliyoyasema yote ni kweli shukuru Mungu umesanuka mapema. Me ndomana sikuizi najinywea zangu ndani na wife. Nina li stock langu la Konyagi nimenunua duka la jumla wife nimemchukulia flying fish tukimaliza tujapiga game ya kibabe tunalala. Me nliacha pombe baada ya kukubuu kwenye umalaya nikaona nitakufa mapema na Ukimwi niache watoto wanateseka.
 
Mimi namshukuru tu Mungu kuniepusha na hiki kikombe,siijui ladha ya bia zaidi ya pombe ya kienyeji ya asili ambayo nayo nimeicha since 1997 bado nikiwa mdogo.

Hongera mkuu umepiga hatua moja muhimu sana tunza dhamiri yako usirudi nyuma.
 
Pombe ni ndugu wa madeni
 
Baba angu alikufa maskini sabab ya kampany za pombe yey ,kazi zake niza kijungu jiko ila bar anakaa na maboss wa bandar na ubalozini

Alikuwa anapendeza mbaya but home watoto hali mbaya

Pombe sio chain na mm najiona naelekea kule kule tu japo SHH ananingalia kila mwezi bado nanga inapaaa
 
Mi mwenyewe mzee wangu alikuwa cha pombe sana nami nikaingia huko nimeshtuka sasa na sitarudi tena. Jitahidi sana utoke huko fikiria tu unatarajaia nini baadae? Unataka kujenga familia ipi?
 
Mi mwenyewe mzee wangu alikuwa cha pombe sana nami nikaingia huko nimeshtuka sasa na sitarudi tena. Jitahidi sana utoke huko fikiria tu unatarajaia nini baadae? Unataka kujenga familia ipi?
Ushauri bomba
 
POMBE IS NOT FOR EVERYONE

BIA TAMU
 
Nenda na budget yako halaf acha mbwembwe na misifa....
Elfu kumi ni budget kubwa sana.....

Tatizo lenu pombe zinawatawala hamjui kuzitawala.......

Siku zote POMBE sio mbaya Tatizo ni watu wenyewe...

Overdrinking na ujinga ujinga mwingi pia uchawi upo na hisi maana kuwatu utawakuta Kila uchwao kwenye mabaa utazani wamelogelezewa....

Mwenyez MUNGU naomba uniepushe na izo njia....
 
Pombe mbaya sana,uliyoyasema ni Mimi kabisa kasoro ilo la mikopo,ila tatizo linalonisumbua ni Kutumia pesa ovyo kwenye pombe na Malaya nikishalewa plus urafiki na watu nisiowajua baada ya kulewa plus kuwapa offer,aisee uwa najuta sana ikifika asubuhi na pombe zimeisha kichwani,ni kama Nina Pepo uwa linaniambia nenda sehemu fulani ata pawe ni mbali ntafunga safari,nilipokuwa university pesa yangu nyingi ya boom ilipotea kwenye pombe na Malaya,maana nikishalewa nakuwa sijielewi natumia pesa vibaya sana mungu anisaidie niache huu ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…