POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

InshaAllah!... Hii nimeacha kwa nia moja mkuu na sio kwamba namaisha magumu sasaivi, kama ni pesa ya matumizi hainipigi chenga kama ningekuwa na nia ya kulewa nisingeshindwa kunywa kila siku
Sawa Allah akuongoze katika njia iliyonyooka
 
Usiache pombe sababu ya umaskini acha pombe sababu umeamua nakuhakikishia yeyote anaecha sababu amekosa pesa siku akizipata itakuwa hatari mara 11.....mimi mlevi hayo yote nayapitia sio siri ila life goes on......drink responsible
Kila kitu kina sababu yake alafu mimi sijaacha pombe kwa sababu ya amasikini pesa ya kunywa bado ninayo ila nimeona siwezi kujicontrol kwenye pombe na uhakika sitarudi maana nilijaribu kuicontrol ili niendelee lakini nilishindwa bali yenyewe ndio ilinicontrol so sitarajii kurudi tena kwenye kitu ambacho kilishanishinda.
 
Umeandika pumba shehe ungejikita kujibu hoja zake na sio hizi taarabu uNazoleta acha ujinga jibu maswalibyake kama unaaweza
Binti yangu na wewe umekuja kumsaidia mwenzako... Usiingilie vitu katikati usivyo vijua utapasuka... Pumba unazo wewe matakoni... Karibuni nipo hapa kwajili ya wapumbavu gays kama nyinyi, leo nitawanyoosha
 
Kama sina pesa baa sigusi, japo kweli marafiki wanashawishi mno.
Hata kama huna kitu utaambiwa we njoo mambo yote ipo huku.

Ninapowakubali walevi wengi sio wanafki kama ambao hawanywi. Mkilewa pale ni rahisi mtu kuropoka utumbo kama alikua hakukubali atakuchana makavu mtateteana pale mchezo unaisha kesho amani amani(wengi niliokutana nao wako hivi).

Usiache ila punguza, ukiona mpaka inakupeleka puta unachukua malaya bila kupenda na wakati mfuko hairuhusu hilo ni tatizo jicontrol tu.
 
"E="Haya_Land, post: 42492584, member: 469833"]
Je sisi wenye mademu wawili na Bado kabla ya kulala tunajichuwa yaani hatuliziki kingono na huku X wangu anaitafuta kwa Nguvu na huku kaolewa ndoa takatifu Pentakosti .. Je Mimi Ni Nani #Mtuombee
duuh.kumbe tupo wengi.
[/QUOTE]"
 
Kama ulishawahi kusoma nyuzi zangu mbili tatu hapa JamiiForum utagundua kabisa mimi ni cha pombe. Nikwambie tu mada zote nlizowahi kuzileta hapa ni za ukweli isipokuwa huwa nabadili kidogo maudhui ili kuepuka wazee wa kuunga dots, bado sijawa tayari kujiweka wazi mimi ni nani maana mengi ni ya aibu kwangu na jamii inayonizunguka na mengi nilikuwa nayafanyia gizani ukija mtaani kwangu mimi ni mtu mstaarabu na mpole sana.

Leo nimekuja tena na mada hii ya pombe lakini si kwa kuipa sifa za kijinga kama ilivyokuwa kwenye mada zile bali kuelezea jinsi nilivyoamua kuacha pombe, naamini sitarudi tena huko kwa bidii zangu na uwezo wake Allah (SW).

Kuna sababu nyingi zimenifanya kuacha pombe lakini kubwa zaidi ni madeni. Pombe iliniingiza kwenye madeni makubwa sana ambayo hadi leo hii bado kuna ambayo sijayamaliza, bado kuna watu nawalipa taratibu maana yalikuwa ni madeni haswa sio videni, kwa kipato changu kudaiwa 3,000,000 (milioni tatu) ya riba kubwa na mtu au watu ni jam kubwa sana na hapa sijaweka deni la taasisi ambalo natembea nalo mwaka wa pili huu sasa, nafikiri kwa sasa ngoma itakuwa bado inasoma kama 30 something million hivi au chini kidogo ya hapo.

Waajiriwa wengi na wafanyabiashara huchukua mikopo bank na huwa na manufaa sana kwao kwani husaidia kutimiza malengo yao kwa wakati lakini kwangu imekuwa kimeo sababu mkopo niliochukua nilitimiza malengo machache sana ya msingi na kubwa kuuza sura kwenye maeneo ya starehe na kulipa madeni (yani deni kwa deni!)

Mtu unaweza kujiuliza pombe inasababishaje kuingia kwenye madeni ya mamilioni?! Kama wewe ni mlevi, mpenda starehe na sifa bila kujali kipato chako huwezi kunishangaa ila kama wewe una sifa hizi na bado unanishangaa basi mshukuru Mungu kukupa uwezo huo wewe ni mlevi mwenye kujitambua. Hapa sijakataa kuwa wapo walevi wastaarabu wasiofuja pesa japokuwa hata kwao huwa haikosekani hata ile kidogo ya kujilaumu kutumia pesa tofauti na malengo.

Lakini usilewe sifa kimsingi walevi wengi ni wa hasara sema tu walevi huwa na tabia moja; Maumivu na mateso wanayopitia huwa hawapendi yawe wazi, maranyingi hupenda kuonekana wao ni watu wanaofurahia maisha kuliko yeyote hapa duniani na siku zote utawasikia “Basi pombe inamaliza hela ndugu yangu!... Mimi nikiwa hata na elfu kumi nalewa na nnarudi zangu nyumbani”. Weeeee!!!.... usijaribu ndugu yangu hakunaga mlevi wa hivyo na kama rafiki yako mlevi anakuambiaga yuko hivi anakudanganya.

Pombe imebeba mzigo mkubwa sana nyuma yake, usione mtu bar na bia yake mezani akinywa huku akitabasamu pekeake, akipiga story kwa uchangamfu na rafiki zake au akisimama na kucheza kwa furaha ukadhani mtu huyo ni mwenye kufurahia sana maisha na pombe inaishia hapo tu. Elewa kabisa nyuma ya pazia kuna mengi. Uzinzi, ufujaji pesa, kutoa ofa hovyo hata kwa usiowafahamu, kula hovyo (barbeque) hatakama huna njaa na kukopa hovyo ilimradi siku hiyo utimize lengo. Vyote hivi vipo nyuma ya pombe.

***Uko nyumbani kama mgonjwa sababu ya kuwaza pesa uliyoharibu jana kwenye pombe, huna raha kabisa maana unawaza ile pesa uliyochezea ungeweza hata kufanya kitu fulani cha maana. Mara inaingia simu toka kwa swahiba wako mlevi mwenzako.

“We Gee uko wapi?” inasikika sauti ya kilevi.

“Home Mazee” unajibu kinyonge kama mgonjwa sababu upo kitandani huna usingizi ila umelala na kujipindua pindua ukiwa umesongwa na mawazo.

“Aaaaah hahahaaa!!!.... we mjinga umelala nini? Acha ujinga wewe njoo hapa Machakani Lounge tupige vitu” anaongea jamaa yako akionekana mwenye furaha sana huku pembeni ukisikia shangwe la kutosha toka kwa wadau wengine.

Kwakuwa unajua shoo za mdau wako huyu unakurupuka kitandani bafuni fasta piga mswaki unaoga na kuvaa chap huku ukijiliwaza.

“Bora niende huko nipunguze stress maana nikikaa hapa nyumbani nazidi kuchanganyikiwa”

Unatoka ukimuaga mkeo na kumuomba akuazime 20 (toka kwenye hela za matumizi ya nyumbani) maana unaona kwenda mikono mitupu kabisa ni aibu lolote linaweza kutokea.

Unafika bar kweli jamaa wamewaka, vibe la kutosha kwenye meza ya duara kuna watoto wakali kama wanne hivi na washkaji wapo watatu tu, baada ya utambulisho unagundua kabisa mmoja umeachiwa wewe na kawaida ya walevi utasikia;

“We vuta kiti pale, wewe njoo huku alafu huyu akae hapa”

Unasogezewa zigo kiulaini bila hata kutumia nguvu, niwaambie tu jamani walevi maranyingi huwa hawatongozani mambo huwa yanajipanga yenyewe kama game tu. Ukiwa hujalewa vitendo hivi utaona vya kawaida kabisa wala havikuchukulii muda sana tena kuna wakati unajisemea moyoni

“Leo mimi nimekuja kulewa habari za wanawake sitaki, kwanza sina hela kabisa sitaki mambo mengi leo”

Ganzi ikianza kukuingia upuuzi unaanza pia. Dem ulikuwa unamuona wa kawaida mara unaanza kumuona Cleopatra na hivi wakati huo kakulalia pegani kichwa kinakujaa mwanaume unaanza kupiga hesabu kichwani. Mfukoni una 20 tu kuna watu wanakunywa wine hapo, 20 haitoshi. Fasta unamcheki mdau wako wa pesa za moto (za riba umiza) na walivyo hawa jamaa huwa wanaamini sana walevi (wenye vyanzo) hata ukimuomba laki3 wakati huohuo anakuletea, hii inanikumbusha jamaa mmoja aliwahi comment kwenye uzi wangu akisema kwamba alipokuwa mlevi alikuwa hakosi pesa kabisa tofauti na alipoacha. Huu ndio ukweli walevi huwa na mipango mingi ya pesa sema pesa zenyewe huwa za moto🤣 . Mzigo ukifika bata linaendelea....***

Unafikiri asubuhi utaamkaje tena? Juzi umechezea pesa ukaamka unajilaumu, jana rafiki zako wanakushawishi ukanywe unaona ni sawa ili upunguze mawazo lakini baada ya kulewa unajikuta unafuja tena pesa!! Umeamka pombe imeisha na pesa imeisha na deni juu! Kweli pombe ni ganzi yenye maumivu tena maumivu makali sana.

Hii ni sababu kubwa iliyonifanya kuacha pombe, rafiki zangu wengi hawajaamini kama nimeacha na wengine wanafikiri nimetumia dawa au nilipewa dawa na ndungu zangu bila mimi kujua lakini ukweli ni kwamba nimeamua mwenyewe kuacha na InshaAllah sitarudi tena huko. Ili kukaa mbali na pombe nikaamua kuwa karibu na Allah sasaivi nafanya ibada maana ibada hutuweka mbali na maasi. Ukiwa na hofu ya Mungu utafata maamrisho yake.

Makosa yetu na ya watu wanaotuzunguka yawe funzo na si kuzidi kujaza kurasa chafu kwenye kitabu cha maisha yetu.

Wasalaam.View attachment 2210931
Uloyasema yote ni kweli.binafsi nilihangaika na pombe sana nkatumia madawa za kienyeji za kuacha pombe zenye garama lakini sikufanikiwa.kuna siku nimetoka dar ad karatu kwa mganga lakini bado sikufanikiwa.nilibakiwa na wazo moja tu KUJINYONGA ,Nilipokua nasubiri siku nijinyonge nlikutana na fundi mmoja mshona viatu cha pombe mnywa gongo na bumburi , ameacha pombe,sikuamini nkasema mm itawezekana? Basi nkashea stor yangu na huyu mzee na akanihakikishia nitaacha pombe na tukaagiza dawa tena kwa garama ndogo.amini usiamini mimi na pombe atuendan kabsa na mm huwa muwaz kwa washkaji kua skuacha bure nilitumia dawa.3 years now i dont drink beer na kwa msemo wako.sitorudi tena kwa pombe bora nife.kwa sasa kuepuka maswali mengi kwa wadao nawaambia tu bia napiga na ninaagiza brand kabisa isiopatikana eneo husika.KWA POMBE KUNA MAJONZI MENGI NYUMA YA PAZIA ASIKWAMBIE MTU
 
Daa kuna mshikaji wangu mmoja amenizoea kupitia magroup tokea nimemjua 3yrs ago mwana mm ndio nazungusha round aisee halafu ikifika ijumaa utasikia mwanangu biriani vp ibungu kiumri kanipita sana he is 40plus kuna siku tuko mahali jioni tunakula vyombo kaita manzi there after anaitumia meseji ya mzinga anaomba hela akamp....... yule mwanamke kuanzia siku hiyo nimempunguza wanaozungusha round wachache sana siku hizi
 
Kila kitu kina sababu yake alafu mimi sijaacha pombe kwa sababu ya amasikini pesa ya kunywa bado ninayo ila nimeona siwezi kujicontrol kwenye pombe na uhakika sitarudi maana nilijaribu kuicontrol ili niendelee lakini nilishindwa bali yenyewe ndio ilinicontrol so sitarajii kurudi tena kwenye kitu ambacho kilishanishinda.
Wewe uko sawa na mimi,sikuwa nakunywa kivile,bia 2 au 3 kwa siku,cha ajabu nilikuwa nikinywa kiu ya hawa wenzetu ilikuwa inanitesa sana,nikaamua tu bora niache ...
 
Kila kitu kina sababu yake alafu mimi sijaacha pombe kwa sababu ya amasikini pesa ya kunywa bado ninayo ila nimeona siwezi kujicontrol kwenye pombe na uhakika sitarudi maana nilijaribu kuicontrol ili niendelee lakini nilishindwa bali yenyewe ndio ilinicontrol so sitarajii kurudi tena kwenye kitu ambacho kilishanishinda.
mkuu mi nakamilisha mwezi wa tatu huu ,nimeamua sifanyi kosa tena as long huo mwanya wa kuacha nimepata.
 
Jambo la msingi sana mkuu, mi niliacha mwanzoni mwa January 2022
 
Kama ulishawahi kusoma nyuzi zangu mbili tatu hapa JamiiForum utagundua kabisa mimi ni cha pombe. Nikwambie tu mada zote nlizowahi kuzileta hapa ni za ukweli isipokuwa huwa nabadili kidogo maudhui ili kuepuka wazee wa kuunga dots, bado sijawa tayari kujiweka wazi mimi ni nani maana mengi ni ya aibu kwangu na jamii inayonizunguka na mengi nilikuwa nayafanyia gizani ukija mtaani kwangu mimi ni mtu mstaarabu na mpole sana.

Leo nimekuja tena na mada hii ya pombe lakini si kwa kuipa sifa za kijinga kama ilivyokuwa kwenye mada zile bali kuelezea jinsi nilivyoamua kuacha pombe, naamini sitarudi tena huko kwa bidii zangu na uwezo wake Allah (SW).

Kuna sababu nyingi zimenifanya kuacha pombe lakini kubwa zaidi ni madeni. Pombe iliniingiza kwenye madeni makubwa sana ambayo hadi leo hii bado kuna ambayo sijayamaliza, bado kuna watu nawalipa taratibu maana yalikuwa ni madeni haswa sio videni, kwa kipato changu kudaiwa 3,000,000 (milioni tatu) ya riba kubwa na mtu au watu ni jam kubwa sana na hapa sijaweka deni la taasisi ambalo natembea nalo mwaka wa pili huu sasa, nafikiri kwa sasa ngoma itakuwa bado inasoma kama 30 something million hivi au chini kidogo ya hapo.

Waajiriwa wengi na wafanyabiashara huchukua mikopo bank na huwa na manufaa sana kwao kwani husaidia kutimiza malengo yao kwa wakati lakini kwangu imekuwa kimeo sababu mkopo niliochukua nilitimiza malengo machache sana ya msingi na kubwa kuuza sura kwenye maeneo ya starehe na kulipa madeni (yani deni kwa deni!)

Mtu unaweza kujiuliza pombe inasababishaje kuingia kwenye madeni ya mamilioni?! Kama wewe ni mlevi, mpenda starehe na sifa bila kujali kipato chako huwezi kunishangaa ila kama wewe una sifa hizi na bado unanishangaa basi mshukuru Mungu kukupa uwezo huo wewe ni mlevi mwenye kujitambua. Hapa sijakataa kuwa wapo walevi wastaarabu wasiofuja pesa japokuwa hata kwao huwa haikosekani hata ile kidogo ya kujilaumu kutumia pesa tofauti na malengo.

Lakini usilewe sifa kimsingi walevi wengi ni wa hasara sema tu walevi huwa na tabia moja; Maumivu na mateso wanayopitia huwa hawapendi yawe wazi, maranyingi hupenda kuonekana wao ni watu wanaofurahia maisha kuliko yeyote hapa duniani na siku zote utawasikia “Basi pombe inamaliza hela ndugu yangu!... Mimi nikiwa hata na elfu kumi nalewa na nnarudi zangu nyumbani”. Weeeee!!!.... usijaribu ndugu yangu hakunaga mlevi wa hivyo na kama rafiki yako mlevi anakuambiaga yuko hivi anakudanganya.

Pombe imebeba mzigo mkubwa sana nyuma yake, usione mtu bar na bia yake mezani akinywa huku akitabasamu pekeake, akipiga story kwa uchangamfu na rafiki zake au akisimama na kucheza kwa furaha ukadhani mtu huyo ni mwenye kufurahia sana maisha na pombe inaishia hapo tu. Elewa kabisa nyuma ya pazia kuna mengi. Uzinzi, ufujaji pesa, kutoa ofa hovyo hata kwa usiowafahamu, kula hovyo (barbeque) hatakama huna njaa na kukopa hovyo ilimradi siku hiyo utimize lengo. Vyote hivi vipo nyuma ya pombe.

***Uko nyumbani kama mgonjwa sababu ya kuwaza pesa uliyoharibu jana kwenye pombe, huna raha kabisa maana unawaza ile pesa uliyochezea ungeweza hata kufanya kitu fulani cha maana. Mara inaingia simu toka kwa swahiba wako mlevi mwenzako.

“We Gee uko wapi?” inasikika sauti ya kilevi.

“Home Mazee” unajibu kinyonge kama mgonjwa sababu upo kitandani huna usingizi ila umelala na kujipindua pindua ukiwa umesongwa na mawazo.

“Aaaaah hahahaaa!!!.... we mjinga umelala nini? Acha ujinga wewe njoo hapa Machakani Lounge tupige vitu” anaongea jamaa yako akionekana mwenye furaha sana huku pembeni ukisikia shangwe la kutosha toka kwa wadau wengine.

Kwakuwa unajua shoo za mdau wako huyu unakurupuka kitandani bafuni fasta piga mswaki unaoga na kuvaa chap huku ukijiliwaza.

“Bora niende huko nipunguze stress maana nikikaa hapa nyumbani nazidi kuchanganyikiwa”

Unatoka ukimuaga mkeo na kumuomba akuazime 20 (toka kwenye hela za matumizi ya nyumbani) maana unaona kwenda mikono mitupu kabisa ni aibu lolote linaweza kutokea.

Unafika bar kweli jamaa wamewaka, vibe la kutosha kwenye meza ya duara kuna watoto wakali kama wanne hivi na washkaji wapo watatu tu, baada ya utambulisho unagundua kabisa mmoja umeachiwa wewe na kawaida ya walevi utasikia;

“We vuta kiti pale, wewe njoo huku alafu huyu akae hapa”

Unasogezewa zigo kiulaini bila hata kutumia nguvu, niwaambie tu jamani walevi maranyingi huwa hawatongozani mambo huwa yanajipanga yenyewe kama game tu. Ukiwa hujalewa vitendo hivi utaona vya kawaida kabisa wala havikuchukulii muda sana tena kuna wakati unajisemea moyoni

“Leo mimi nimekuja kulewa habari za wanawake sitaki, kwanza sina hela kabisa sitaki mambo mengi leo”

Ganzi ikianza kukuingia upuuzi unaanza pia. Dem ulikuwa unamuona wa kawaida mara unaanza kumuona Cleopatra na hivi wakati huo kakulalia pegani kichwa kinakujaa mwanaume unaanza kupiga hesabu kichwani. Mfukoni una 20 tu kuna watu wanakunywa wine hapo, 20 haitoshi. Fasta unamcheki mdau wako wa pesa za moto (za riba umiza) na walivyo hawa jamaa huwa wanaamini sana walevi (wenye vyanzo) hata ukimuomba laki3 wakati huohuo anakuletea, hii inanikumbusha jamaa mmoja aliwahi comment kwenye uzi wangu akisema kwamba alipokuwa mlevi alikuwa hakosi pesa kabisa tofauti na alipoacha. Huu ndio ukweli walevi huwa na mipango mingi ya pesa sema pesa zenyewe huwa za moto[emoji1787] . Mzigo ukifika bata linaendelea....***

Unafikiri asubuhi utaamkaje tena? Juzi umechezea pesa ukaamka unajilaumu, jana rafiki zako wanakushawishi ukanywe unaona ni sawa ili upunguze mawazo lakini baada ya kulewa unajikuta unafuja tena pesa!! Umeamka pombe imeisha na pesa imeisha na deni juu! Kweli pombe ni ganzi yenye maumivu tena maumivu makali sana.

Hii ni sababu kubwa iliyonifanya kuacha pombe, rafiki zangu wengi hawajaamini kama nimeacha na wengine wanafikiri nimetumia dawa au nilipewa dawa na ndungu zangu bila mimi kujua lakini ukweli ni kwamba nimeamua mwenyewe kuacha na InshaAllah sitarudi tena huko. Ili kukaa mbali na pombe nikaamua kuwa karibu na Allah sasaivi nafanya ibada maana ibada hutuweka mbali na maasi. Ukiwa na hofu ya Mungu utafata maamrisho yake.

Makosa yetu na ya watu wanaotuzunguka yawe funzo na si kuzidi kujaza kurasa chafu kwenye kitabu cha maisha yetu.

Wasalaam.View attachment 2210931
Hongera sana mkuu

tangu umeacha unamuda gani
 
Back
Top Bottom