Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,951
- 19,766
Salaam jamiiforum.
Pombe ni burudani ambayo ipo tangu enzi za manabii,ikiwa ni moja ya burudani nzuri,yenye kukutanisha marafiki,wachapakazi pamoja na wazalendo.
Sisi wenyewe ni mashahidi ni mara nyingi makampuni kadhaa ya pombe yamekuwa yakipewa sifa na tuzo Kwa kuwa rekodi nzuri kwenye pato la taifa,hata hapa Nchini kwetu bado pombe ina nafasi kubwa kwenye ukuaji wa pato la Tanzania.
Lakini je pombe hii,au burudani hii inatumika namna gani?
Inatumiwa na watu gani?
Je watumiaji Wana Elimu sahihi ya matumizi ya pombe?
Wanajua kutofautisha Aina za pombe?
Kuna mtu anakunywa spirit au whisky vinywa vyenye ethanol yenye kiwango kikubwa ,huyu mtu leo atakunywa beer,Kesho atakunywa spirit Kesho atakunywa pombe nyingine,yeye shida yake ni kulewa tu,hajui kwamba hivi mambo hunywewa Kwa viwango siyo kubwia tu.
Lingine wapo watu hunywa pombe Kali Kwa sifa wawapo sehemu za starehe.wameweka matabaka kabisa kwamba pombe fulani ni za kike,na mara nyingi mtu ukikutwa unakunywa unaonekana,huna kichwa cha pombe huku wao wakiagiza pombe Kali ili tu waonekane ni wanaume au watu strong
Hivi leo kumekuwa na lundo la pombe Kali mitaani,zikiuzwa Kwa bei cheap kabisa,tena Hadi nusu yake ipo mtu anapimiwa na maisha yanaendelea.pombe hizi za bei rahisi zina wateja wake maalumu,wengi wao Wana vipato vya chini huku asilimia 70 hivi wakiwa ni vijana
Watu wengi hawawezi kuafford kuingia bar kutumia 30k Kwa pamoja.
Ndipo mtu anapoangukia kwenye hizi pombe na kujikuta anakuwa mlevi kupindukia kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu yake kiusahihi.
Pombe ni burudani Safi lakini isipotumiwa vizuri ina madhara kimwili,kiasi cha kuzalisha wagonjwa wengi ambao pengine hawajajitambua kama wanaumwa na badala yake wanaendelea kunywa tu siku zote.
Zipo njia kadhaa amvazo mnywaji na mdau wa maendeleo inapaswa ujue.
1.Kula vizuri kabla hujaanza kunywa.
Hili ni jambo la msingi na la lazima,hata ukiwa bar kama hiyo sehemu kuna chakula basi ni vema kula chakula cha kutosha ndipo uanze na mbilinge zako.
2.Jitambue kuanzia uzito na urefu wako
Kama ilivyo hospital mtu hupimwa uzito na urefu ili kujua MLs za dawa ndivyo hata pombe inavyotakiwa ,bahati mbaya hatuna Elimu sahihi na wanaotuuzia huenda wanaangalia zaidi vipato kuliko afya za watu.
3.Acha pombe za sifa na mashindano
Panga ni kiasi gani cha pombe utakunywa,hii itasaidia kuimarisha afya yako na hata kusave pesa,kuliko kuona mtu kajaza meza na wewe ukaona watu wasikuchukulie poa na wewe unaiga mwishowe,unaharibu bajeti na kujiweka kwenye hatari zaidi.
4.ukiamka na pombe tafuta chakula haraka.
Pombe ukiizidisha Sana hupelekea mtu kukosa appetite ya kula hivyo inaweza kukutengenezea uchovu wa muda mrefu kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu Kwa usahihi.
Hivyo mchemsho,supu ya kongoro na vitu vingi ambavyo vina uzito vikiingia tumboni waweza kutumia ili kujiweka mazingira mazuri haswa suala zima la utimamu wa mwili.
La muhimu zaidi
POMBE SI KWAAJILI YA MTU MASIKINI
Yaani ulewe huku huna uhakika wa kuamka na buku mbili .
Pombe kwako ni za nini sasa mwanakwetu.