Pombe na ilivyosababisha nikaikosa nyumba

Pombe na ilivyosababisha nikaikosa nyumba

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Nipo hapa local bar namalizia glass ya mwisho ili niondoke, lakini Kuna muda pombe ni mbaya sana, yaani faida ni ndogo sana kuliko hasara.nimejikuta najikumbusha kisa kimoja kilinikwamisha sana.

Mwaka fulani baada ya kumaliza chuo, sikubahatika kupata kazi mapema, hivyo nikawa natumwatumwa tu pale kwa faza mkubwa, naenda sokoni, namsaidia mama kazi za ndani kama kufua n.k

Lakini kuhusu kulala nikawa silali pale tena, nilikuwa naenda kwa washikaji zangu fulani wawili ambapo tulijiita Triple D, maana majina yetu yalifanana herufi za mwanzo, si majina tu hata akili zetu ziliendana, na pia wote tulimaliza mwaka mmoja japo vyuo tofauti, Sasa bwana kwenye ujana, mambo ni mengi, tulianza kujifunza vitu vingi ikiwemo starehe.

Ilikuwa ni kawaida kwenda night club hata kama hatuna pesa kihivyo lengo likiwa ni kuenjoy na kuzilaghai nafsi zetu.

Tulijifunza kunywa pombe japo Mimi nilikuwa Expert, maana mkoani kwangu pombe tuliijua tukiwa bado wadogo, basi maisha yalienda huku kitendo cha kukaa bila kazi kilitutesa kwani starehe na mademu vilihitaji pesa na sisi tukawa hatuna kazi tena.

MUNGU si mwanadamu, Kuna mwanetu yeye alipenda sana kitu Cha Canada, eeeh mjani kwa sana, japo Mimi sikuwahi kupenda maana harufu yake ilikuwa ikinizingua.

Basi tulipiga stori za kijobless weeee, Kisha mwanetu akatoka kwenda kufuata vitu vyake japo tulimuasa akamalizie hukohuko maana binafsi sikupenda harufu yake.

Tukiwa tumepitiwa na usingizi, mwanetu alirudi na kutuamsha huku akiwa na uso wa furaha akitwambia Kuna dili, dili gani? Tukauliza.
Akafunguka namna alivyokutana na Don mmoja mwenye mawe, ambaye tulimfahamu, akatuambia kazi hiyo ipo Nje ya nchi, nchi gani, ni Norway.

Duh wote wawili tuliguna, Kisha tukamtizama hakuwa akitania uso wake ulizungumza, Kwakuwa alitwambia hayupo mbali, tukatoka mbiombio tukikata chochoro tukatokea barabara kuu, tukamkuta yule Don kazungukwa na vijana wengi ambao haiba zao hazikuwa nzuri, uteja, na pombe kali viliwaathiri.

Alivyomuona jamaa yetu, alifurahi.Ooh Denis , umerudi Tena ndiyo Hawa ndugu zako eehhh,
Hawa sawa Hawa tunaweza kupiga nao kazi, tena huyu namfahamu kabisa naye {akimaanisha Mimi}

Mzee Mimi umenijuaje, mbona Mimi sikufahamu niliuliza.

Wewe si unakaa kwa mzee {akitaja jina}na hapa lazima nitaongea naye jamaa yangu maana hii dili siwezi kuwapa watu baki kuliko nyie wanangu, je mpo tayari kupiga kazi nje ya nchi?

Kwa pupa tukaitikia hata Sasa hivi, akatujibu sawa kwakuwa ni nchi za watu lazima Kuna vitambulisho kibao lazima tuwe navyo, na yeye atahusika kuandaa vitu vyote.

Ikiwemo masuala ya ndege huku akituambia ndani ya wiki tatu Kila kitu kitakaa sawa na sisi nikujiandaa na safari, lakini tukaomba tuijue kazi maana Dunia si yetu, akachukuaya kikamera fulani kinaonesha video akatuonesha hiyo kazi kupitia ile camera ambayo kwangu ilikuwa Mara ya kwanza kuiona.

Tukawaona watu wakiwa sehemu ya bandari maana makontena yalikuwa mengi japo haikuwa Norway kama alivyosema mwanzo.

Loading...... .. ....
 
Kipindi flani nilipanga ghetto Malakuwa Mwenge siku hiyo nimelewa tokea asubuhi kwa mangi nikaenda lala mchana sasa lile joto la Dar nikavua nguo zote na choo ni cha nje nimeshtuka mida ya saa moja usiku nikajua itakua saa 8 usiku nikatoka nje uchi kwenda kukojoa asee nimetokea uani tu nakutana na wamama wanapika nje wote walikimbilia vyumbani kwao.
Aisee we jamaa ni shidaaaa
 
Chapter 02

Tulirudi geto kwa furaha sana, Mimi nikatoka nikaenda kwa Baba mkubwa nikamwambie habari, japo alisita kidogo lakini nilipomwambia huyo mtu huenda mnafahamiana akasema basi itatakiwa aje tumuone na tumkabidhi ili ukipatwa na jambo baya yeye atawajibika.

Wenzangu Sina uhakika kama walimuaga mtu maana walikuwa moto na hiyo safari na kama wangekatazwa na walezi wao sidhani kama wangewasikia,

Basi yule mzee alikuja home kwa faza, kumbe kitambo wanajuana ikawa urahisi Mimi kwenda ng'ambo
Wiki moja baadaye yule mzee tulikutana naye, huku akitusimulia mambo mengi kuhusu huko namna watu weusi walivyo aminika kuwa ni wapiga kazi, lakini pia akituasa kutojiunga na makundi yasiyofaa kwani kwa kufanya hivyo tutashindwa kutimiza ndoto zetu.

Akatuambia mkataba ni miezi mitatu tu, kama utataka kuendelea unakula mkataba mwingine. Kiasi alichotutajia kama ujira kilizidu kutupagawisha na kuzidi kuona mbona siku hazikaribii watu tupande pipa,akatuachia laki na nusu kwamba kama hatuna nguo viatu tukafanye shopping, kipindi hicho laki ni nyingi sana, tulivyifika geto , kila mtu alikuwa na nguo na viatu vikali Mimi ndiyo usiseme, nani anunue nguo, za Nini?

Tukapiga pasu kila mtu aishi na fifty yake, ni nyingi wakuu elfu hamsini, kesho yake haooo club, lengo Kila mmoja apate demu mkali pesa si ipo? Basi Mimi hata sikuchelewa nipo zangu napiga bia huku mziki fulani mnaita Country music ukipigwa taratibu, wenzangu washapata mademu muda huo, Mimi bado Kila demu akipita namuona mbovu.

Basi Kuna pisi moja matata iliingia , wanangu wote wakanikonyeza kwamba Sasa demu ndiyo huyo ukimkosa basi, na ukizingatia muda ulishaenda nikamfuata kumsalimia akakataa salamu akionesha hataki mazoea nikajiongeza huenda ana mtu wake lakini Cha ajabu alikaa akiagiza kinywaji Tena maji tu karibu dakika ishirini alikuwa peke yake huku kila wanaume wakimuomba Kampani akiwakataa. kwa ujasiri nikamfuata kama vile muhudumu, nikamuuliza ,
Samahani dada tofauti na hayo maji, unatumia kinywaji gani?
Kwanza akaniangalia Kisha akacheka kwa dharau, Kisha akataja kinywaji Cha bei ambayo huenda alijua sitaimudu , nikamwashiria waiter akaleta Kisha nikirudi zangu kwenye meza yangu. Huku nikiona wivu wanangu wanavyopigana mabusu na wapenzi wao.

Wakati nawaza yule dada alikuja bwana, akionesha ananiheshimu kwani Kila nilichoongea aliitikia huku akionesha anataka kunijua zaidi lakini nikawa nampoteza, akataka tucheze music tukainuka tukaserebuka dadeki alinyonga kiuno nikajiuliza huko kitandani itakuwaje?
Lodge tulichukua saa ngapi sikujua, tuliongozana na nani sikujua, huku nikishangaa Binti yupo uchi mbele yangu akiwa ananivua Shati
acha ugoigoi na wewe, unalala saizi saa kumi alfajiri unataka unilaumu eti sikukukupa eeeeh. Alilaumu yule demu.

Nilimvamia huku alilalamika mapenzi gani bila romance lakini sikujali , nilichotaka nipige zaidi ya bao tatu kabla hakujapambazuka japo nikifeli kwani hata demu aliniambia anawahi akinilaumu kwa uzembe wangu mwenyewe nikaishia mbili tu.akaniambia yeye ni mtangazaji wa redio hivyo nikimtaka
Nitamuulizia, masikini alinielekeza sijui alijua Nina hela, nikavuta suruali nikachukua kiasi fulani nikampa akakataa akidai kama nampenda nitamtafuta kwani ashanielekeza akaondoka

Tukiwa geto na wanangu tulisimuliana huku kila mmoja akijisifu kivyake namna alivyomchakata demu japo Mimi nilijikuta nimezingua na washikaji nikawaficha.
Zikaja stori za maisha Sasa tukitoka na mzigo ughaibuni tutafanyia Nini kama kile kiasi tajwa ndani ya miezi mitatu mbona ni nyingi.
Tuliongea mengi Mara biashara, Mara Nini lakini wote tukakubaliana Bora kujenga nyumba,
Kwanza bado vijana wadogo biashara pasua kichwa tu, Bora nyumba utakuwa unakula Kodi za wapangaji tu,

lakini bado yule demu Mimi nilimuelewa sana, licha ya wanangu kunikanya, kuwa kwa muda huo tuachane na mademu tuangalie safari yetu Mimi sikuwaelewa hata kidogo nilimtafuta yule manzi nikampata akanikaribisha kwake, penzi likaanza kuchipua rasmi hata baada ya kugundua kuwa Sina pesa lakini dada wa watu alinielewa tu.

Basi wiki nzima nilifungiwa kwake, anatoka ananikuta, akawa anaburudika atakavyo ratiba ya vipindi vyake ikiwa ni saa tatu asubuhi mpaka saa tano, baada ya hapo ana kazi nyingine tu mpaka saa kumi alasiri anarudi

Siku narudi nakuta geto limefungwa Tena kufuli mpya siyo ile na Kuna pazia tu, Kuna dada akajitokeza akaniambia yeye ndiye kaachiwa chumba na mdogo wake Denis.
Nikatoka nikaenda kwa faza akanikoromea kuwa nilikuwa wapi na ndege imeondoka usiku wa siku hiyo hivyo safari nimeikosa akidai wenzangu walizurula huko na huko hawakunipata hakukuwa na simu wangenipataje?.

Nilichukia sana nikamchukia na yule demu lakini haikusaidia ni ujinga wangu mwenyewe

Baada ya miezi Saba washikaji walirudi wakinikuta ni dereva namuendesha mwarabu mmoja hivi angalau nipate hela ya kula, walipata shilingi ngapi, sikujua ila kila mmoja aliinua nyumba ya maana Kwa wakati huo, hakika niliumia.
Niliumia mno tena sana. Tena walivyo na bahati na a pesa si walikuwa nayo wakapata kazi haraka mno huku Mimi nikiwa bado napambania hela ya kula.[emoji23][emoji23][emoji23]

Wakawa hawataki Tena Kampani na Mimi kwani hata pombe wakawa hawatumii , Sasa mtu anakwambia kakaa miezi sita bila kugusa pombe mbona ni rahisi kuachana nayo?

Maisha haya acha tu.
 
Huelewi kabisa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nashindwa elewa kabisa besty...maana raha ya mihangaiko ya kusaka pesa ni ili upate kustarehe na warembo wakali. Warembo nao wanataka kugonga savannah na desparados. Sasa sijui wanataka tufanye starehe gani nyingine nje ya hapo
 
Back
Top Bottom