Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Nipo hapa local bar namalizia glass ya mwisho ili niondoke, lakini Kuna muda pombe ni mbaya sana, yaani faida ni ndogo sana kuliko hasara.nimejikuta najikumbusha kisa kimoja kilinikwamisha sana.
Mwaka fulani baada ya kumaliza chuo, sikubahatika kupata kazi mapema, hivyo nikawa natumwatumwa tu pale kwa faza mkubwa, naenda sokoni, namsaidia mama kazi za ndani kama kufua n.k
Lakini kuhusu kulala nikawa silali pale tena, nilikuwa naenda kwa washikaji zangu fulani wawili ambapo tulijiita Triple D, maana majina yetu yalifanana herufi za mwanzo, si majina tu hata akili zetu ziliendana, na pia wote tulimaliza mwaka mmoja japo vyuo tofauti, Sasa bwana kwenye ujana, mambo ni mengi, tulianza kujifunza vitu vingi ikiwemo starehe.
Ilikuwa ni kawaida kwenda night club hata kama hatuna pesa kihivyo lengo likiwa ni kuenjoy na kuzilaghai nafsi zetu.
Tulijifunza kunywa pombe japo Mimi nilikuwa Expert, maana mkoani kwangu pombe tuliijua tukiwa bado wadogo, basi maisha yalienda huku kitendo cha kukaa bila kazi kilitutesa kwani starehe na mademu vilihitaji pesa na sisi tukawa hatuna kazi tena.
MUNGU si mwanadamu, Kuna mwanetu yeye alipenda sana kitu Cha Canada, eeeh mjani kwa sana, japo Mimi sikuwahi kupenda maana harufu yake ilikuwa ikinizingua.
Basi tulipiga stori za kijobless weeee, Kisha mwanetu akatoka kwenda kufuata vitu vyake japo tulimuasa akamalizie hukohuko maana binafsi sikupenda harufu yake.
Tukiwa tumepitiwa na usingizi, mwanetu alirudi na kutuamsha huku akiwa na uso wa furaha akitwambia Kuna dili, dili gani? Tukauliza.
Akafunguka namna alivyokutana na Don mmoja mwenye mawe, ambaye tulimfahamu, akatuambia kazi hiyo ipo Nje ya nchi, nchi gani, ni Norway.
Duh wote wawili tuliguna, Kisha tukamtizama hakuwa akitania uso wake ulizungumza, Kwakuwa alitwambia hayupo mbali, tukatoka mbiombio tukikata chochoro tukatokea barabara kuu, tukamkuta yule Don kazungukwa na vijana wengi ambao haiba zao hazikuwa nzuri, uteja, na pombe kali viliwaathiri.
Alivyomuona jamaa yetu, alifurahi.Ooh Denis , umerudi Tena ndiyo Hawa ndugu zako eehhh,
Hawa sawa Hawa tunaweza kupiga nao kazi, tena huyu namfahamu kabisa naye {akimaanisha Mimi}
Mzee Mimi umenijuaje, mbona Mimi sikufahamu niliuliza.
Wewe si unakaa kwa mzee {akitaja jina}na hapa lazima nitaongea naye jamaa yangu maana hii dili siwezi kuwapa watu baki kuliko nyie wanangu, je mpo tayari kupiga kazi nje ya nchi?
Kwa pupa tukaitikia hata Sasa hivi, akatujibu sawa kwakuwa ni nchi za watu lazima Kuna vitambulisho kibao lazima tuwe navyo, na yeye atahusika kuandaa vitu vyote.
Ikiwemo masuala ya ndege huku akituambia ndani ya wiki tatu Kila kitu kitakaa sawa na sisi nikujiandaa na safari, lakini tukaomba tuijue kazi maana Dunia si yetu, akachukuaya kikamera fulani kinaonesha video akatuonesha hiyo kazi kupitia ile camera ambayo kwangu ilikuwa Mara ya kwanza kuiona.
Tukawaona watu wakiwa sehemu ya bandari maana makontena yalikuwa mengi japo haikuwa Norway kama alivyosema mwanzo.
Loading...... .. ....