Pombe sio chai. Nililala mwenyewe nimeamka na Mama mwenye nyumba, tunashangaana!

Pombe sio chai. Nililala mwenyewe nimeamka na Mama mwenye nyumba, tunashangaana!

Tunapata sana fedheha kwenye pombe, tukiamka asubuhi tunaapa kuacha ila ikifika jioni tumo tena tunapiga vitu. Dah hii kitu ni utumwa sana.
Ila mkuu najiuliza kwa mfano huyo mama angekuwa na mme wake au mchepuko ndio ukukute upo kitandani si ungekufa kifo siyo chako? Kama hutaacha Pombe mkuu utakuwa umerogwa!😁😁😁
 
Nianzie mbali kidogo. Moja ya maazimio yangu kufikia January 1 mwaka huu ilikuwa ni kuacha kabisa pombe na kampani ya walevi. Pombe imenisababishia madhila kibao katika maisha ikiwamo kushusha heshima yangu kazini na jamii inayonizunguka huko mtaani, kunitenga na Mungu wangu kiroho, kunirudisha nyuma kiuchumi, mafarakano na Mke wangu na aibu nyingine kede kede.

Ilifika January mosi na kweli nilifanikiwa kuacha pombe kwa takribani mwezi mzima wa January. Kimbembe kilikuja ilipofika mwezi February tarehe ya kuazimisha siku yangu ya kuzaliwa! Hapo ndo kama nilizaliwa upya na pombe huko uchagani nikiwa na kina Shirima, Lyimo, Shayo, Minja, Urassa na Mshana. Toka siku hiyo nimekuwa mraibu mkubwa sana wa haya mapombe ila naamini ipo siku nitaacha, ngoja kwanza nianze kujitenga na kampani za wanywaji kina Mshana Jr

Niende moja kwa moja kwenye point sasa.
Jana majira ya saa6 mchana nilitua uwanja wa ndege wa JNIA nikitokea bara Uropa kwa kazi fulani iliyochukua kama wiki moja. Nilipokelewa airport na rafiki yangu Bwana Lyimo na tukaenda moja kwa moja katika mghahawa fulani maeneo ya external kupata ugali nyama choma kabla ya kuanza kupiga vyombo. Baada ya msosi tuligonga vyombo viwili vitatu kusogeza muda.

Majira ya saa 12 hivi jioni tulihamia Julliana maeneo ya Africana Mbezi huku nikiwaalika wanywaji wengine 6 jumla tukawa nane.
Kiufupi nilikuwa na vidola kadhaa nilivyolipwa kwa safari ile nikaona sio mbaya tukinywa na marafiki huku tukipiga story mbili tatu za maisha. Watu walilewa vya kutosha kufikia saa8 usiku kila mmoja akaanza kutoroka bila kuaga.

Majira ya saa11 kasoro alfajiri tulikuwa tayari tumeshapauka vya kutosha mimi na Bwana Lyimo hivyo tukaona ni wakti muafaka wa kurejea nyumbani kulala.

Kwa kuwa kwa Bwana Lyimo ni maeneo jirani tu amepanga katika moja ya apartments fulani Mbezi Makonde niliona sio mbaya nikipumzika kwake then mchana nikishakaa sawa niondoke kuelekea Kigamboni.

Lyimo alinionesha chumba cha kulala nikaingia kupumzika. Dakika chache niliamka kwenda kuchukua simu niliisahau kwenye gari.

Mle kwenye gari kulikuwa pia na chupa kadhaa za vyombo tulivyoshindwa kumaliza tukavibeba. Uroho wa pombe nikaanza tena kuvipiga pale pale. Eh kidume kichwa kikawaka nikasahau hata nyumba ya Lyimo ni ipi nikajikuta nimeenda kuingia nyumba nyingine ambayo mwenyeji wake alisahau kufunga mlango kwa kuwa naye alikuwa vyombo.

He he he! Ishu iko hivi, mwenye nyumba niliyoingia ni mwanamke, mama mtu mzima kidogo ila anaishi na dada wa kazi na wanae wawili wadogo.
Huyu mama huo usiku alikuwa ametoka kwenye shughuli ya harusi, na huko naye alipiga vyombo vya kutosha akawa ndwiii! Alipofika kwake kwa hali ya ulevi alijibwaga chumbani akaacha milango bila kuilock na funguo. Mimi huyooo hata sijitambui, nikafungua wa sebuleni, nikafungua wa chumbani nikakuta jimama jeupe, limenona vyema. Eh pombe sio chai wakuu, nikapanda kitandani nikamvuta na yeye bila hiyana akanikumbatia tukalala fofofo! Saa 1 dakika 40 asubuhi simu yangu inaita nikashtuka, mama naye akashtuka.

Eh tukabaki tunaangaliana tumeduwaa. Mimi sijijui nipo wapi, yule mwanamke simjui, nashindwa kukumbuka imekuwa kuwaje mpaka tupo pale pamoja.

'Wewe! Umeingia ingiaje kwangu? We ni nani? He wewe?'- Aling'aka yule mama akiwa ameduwaa. Akiwa ameshashuka chini kasimama pembeni ya kitanda anatetemeka alinifokea nitoke ndani kwake haraka sana.

Hapo akili zikiwa zimeanza kurudi moja moja nilimjibu kwa upole kuwa mi mgeni wa Lyimo, na hapo nipo kwa Lyimo, ninachokumbuka ni kuwa nilikuwa nimelala mwenyewe, nikaamka kwenda kwenye gari kufata simu, nikaongeza na pombe na hapo ndo mwisho wa kumbukumbu zangu hata nashangaa imekuwaje nipo tena ndani na mwanamke. Akaniuliza kama tumesex nikamjibu sidhani, akajikagua kuhakikisha.

Hapo bado nina pombe, Lyimo ameshaamka, mkewe ameshaamka yupo hapo nje, watoto wameshaamka, kiufupi ni aibu!

Yule mama akatoka akaenda kuongea na Lyimo na mkewe, sijui waliongea nini Lyimo akanifata ananicheka hana mbavu.

Basi bwana nikatoka nayumba yumba na wenge la pombe. Kwa aibu na fedheha nikamsalimia mke wa Lyimo, nikamwambia "Shemeji utanisamehe sana kwa hili, sikuwa na nia mbaya ni matokeo ya mapombe tu haya, hatujafanya kitu. Naomba kwanza niende, pombe zikiniisha tutazungumza."

Basi Bwana nikaenda chumbani kuvaa shati na viatu kisha tukaondoka na Lyimo Kwenda pub fulani jirani kutia vyombo viwili vitatu huku nikimueleza kuwa nilitoka kufata simu kwenye gari na baada ya kunywa tena ndipo nilipojikuta naamka nyumba nyingine tena nikiwa na mwanamke kitandani na wakati hapo awali nilikuwa mwenyewe.

Lyimo akaniambia nimechanganya nyumba, na huyo mama ni mjane, mumewe alifariki kwa ajali mwaka jana. Huwa hatumii sana vilevi ila huo usiku inaonekana alionja viwili vitatu kwenye harusi.

Nilimueleza kuwa sijagonga na akirudi home anisaidie kuniombea msamaha kwa shemeji asinielewe vibaya, sikudhamiria.
Bora mamaa
Ungeamka na babamweny.....??hatareee
 
Pombe inategemea una kunywa je mimi toka nianze kunywa pombe haijawahi kunidhalilisha ni vile naiishi kwa nidhamu tu siwezi kukaa bar mpaka asubuhi labda itokee mara moja sana ndio ntakaa mpaka asubuhi,

Sasa mtu unakunywa beer 10 au 8 zote hizo za nini, Kunywa Beer kiafya Beer tatu umezidisha sana beer nne kinachoendelea kunywa maji mengi, na beer ina sehemu zake za kunywa sio kila mahala wewe unaenda kunywa tu,

Tafuta bar au lounge zisizo na makelele mengi za maaana ndo unaenda kunywa beer binafsi pombe siwezi kuacha kwa sasa pombe imenipa michongo mingi sana ya maana, imenikutanisha na watu wengi wa maana labda itokee huko mbeleni kwa kuamua tu
 
Sasa mtu unakunywa beer 10 au 8 zote hizo za nini, Kunywa Beer kiafya Beer tatu umezidisha sana beer nne kinachoendelea kunywa maji mengi, na beer ina sehemu zake za kunywa sio kila mahala wewe unaenda kunywa tu
Duh bia 8? 10?
Zinafika tumboni hizo au zinaishia kwenye koo?
Bia tunaongelea 20 mpaka 35 au 40 ndo standard.

Hata hivyo kwa sasa tungi naelekea kuacha kabisa.
Kutoka kunywa kila siku mpaka kunywa ijumaa tu ya kila wiki na wakati mwingine mara moja kwa wiki mbili.
Kuliko kunywa bia3 bora ninywe pepsi
 
Kazi ya valuuuuu! Inasafisha memori. Kuna siku nimetwika valuu, konyagi na Serengeti. Sikumbuki nilifikaje geto na mguu unavuja dam huku mlango sikuufunga hata Kwa pazua.

Pole mkuu Kwa fedheha hiyo.
Hatimaye nimetimiza zaidi ya wiki mbili sasa sijanywa pombe.

Huu ni mwanzo mzuri kwa mwaka 2024.
Nimepitia fedheha na aibu nyingi sana katika ulevi.

Ngoja nipumzike kwa muda, maana najua kuna siku huko mbeleni nitarudi kunywa, ila unywaji wa miaka hiyo utakuwa wa kistaarab maana umri umenikimbia sasa naangaliwa na jamii
 
Hatimaye nimetimiza zaidi ya wiki mbili sasa sijanywa pombe.

Huu ni mwanzo mzuri kwa mwaka 2024.
Nimepitia fedheha na aibu nyingi sana katika ulevi.

Ngoja nipumzike kwa muda, maana najua kuna siku huko mbeleni nitarudi kunywa, ila unywaji wa miaka hiyo utakuwa wa kistaarab maana umri umenikimbia sasa naangaliwa na jamii
Hongera sana mkuu jitahidi hivo hivo utaacha tu
 
Namshukur Mungu nakunywa pombe ila hazijawahi kuni control... Huwa nakunywa weekend tu, na nikianza kujisikia kulewa siongezi hata kidogo...
Pombe tamu sana ukiweza kuji control, mimi nikiwaambia watu nakunywa pombe hawaamini... Sinywi pombe za offer au promotion, sinywi pombe kwa kufuata marafiki...
Siachi pombe
 
Najitahidi sana kunywa bia ila naishia mbili, nikizidisha hapo lazima nitapike nahisi wife ananihujumu kwenye hii tasnia. Naomba ushauri wenu walevi wenzangu nifanyeje nisitapike hata nikinywa kreti lote?
 
Nipo napitia machapisho mbalimbali kuhusu mbinu za kuacha pombe.

Tukumbuke madhila ambayo tumepata yakisababishwa na pombe, tuichukie kwa kutupelekea kupata madhila hayo.

Tuweke nia thabiti ya kuachana nayo kabisa.

Tukubali kutenga baadhi ya marafiki, kampani ya pombe.

Tukatae katu katu kwenda mazingira yenye ushawishi wa pombe (Bar, clubs etc)

Tutafute cha kufanya kama mbadala wa pombe mathalani kukaa idle humpelekea mtu kuwaza kwenda tena bar kusogeza muda hivyo ni vyema ukajikita katika usomaji vitabu, watching movies nk.

Tukumbuke pia madhara ya pombe kiafya.


Mimi naanza na kuwakataa marafiki wa pombe, maana ndo kikwazo
Sio kweli.
Ni lazima ufikie point ya kuacha bila shuruti.
 
Nakumbuka siku moja niko Redstone moshi akaja malaya mmoja ilikua mida ya sa kumi alfajiri vibe ni kama lilikua linaanza upya... nakumbuka tuliagiza tena pombe na kwa tamaa nikampanga ...nilijisikia kwenda haja ndogo ile nimeenda washroom nimenawa na uso ni kama ilikujaga akili kua we fala unafanya nini mpaka saivi.....[emoji23][emoji23] Aiseee nilipotoka mlango wa washroom niliunganiaha kwenye gari wala sikurudi kwa yule malaya..... nimefika home nikalala nimekuja kuamka majira ya sa 11 jioni hivi akili inaniambia kua wee boya ungeloteza hela kizembe ..nikajicheka sana kimoyomoyo...Mida ya jioni nikaenda zangu Hugo's Garden kutoa lock.
 
Pombe si chai,
Siku jimama moja limeniita kwake ndani nyumba hiyohiyo upande tofauti.likasema tupige vyombo grants kula vyombo likasaula.
Mzee nikalamba wezere chap.
Bado tunapumua na kuongeza monde kaja rafiki yake jimama flani naye akamiminiwa kwenye glass.
Ebo kilichotokea baadae ni sodoma na gomora
 
Watu wanasema wanaupa moyo pole, sasa kama huna shida kama mtoa mada, unaumwagilia moyo kwa nn wakati huna ukame??? hahahaha, kwakwel, mamelod bingwa, bao la Aziz ki halikua halali, lilidunda kwenye mstari na kutoka nje.
 
Pombe si chai,
Siku jimama moja limeniita kwake ndani nyumba hiyohiyo upande tofauti.likasema tupige vyombo grants kula vyombo likasaula.
Mzee nikalamba wezere chap.
Bado tunapumua na kuongeza monde kaja rafiki yake jimama flani naye akamiminiwa kwenye glass.
Ebo kilichotokea baadae ni sodoma na gomora
Kivipii mkuu. Uliyala yote mawili
 
Back
Top Bottom