Pombe: Sumu inayoua zaidi kuliko vita na gonjwa lolote, lakini tunaiita burudani

Pombe: Sumu inayoua zaidi kuliko vita na gonjwa lolote, lakini tunaiita burudani

Baba yangu anakula Gongo na tumbaku ana miaka 90 yupo safi sijawahi ona. Itoshe kudanganya watu kama hujui ladha ya pombe tulia
Hii ni sawasawa na useme umeona cheche imeruka kwenye tenki la mafuta lililo wazi na halijalipuka moto na hivyo unaamini mara zote cheche ikiruka kwenye tenki la mafuta moto hauwaki........ iga afu uje kutueleza baada ya miaka 20
 
Kuna vitu duniani ukivisikia vinaua, unajua moja kwa moja havina mjadala.
Sumu ya panya? Unakimbia. Risasi? Unakimbia. Lakini pombe? Tunaweka mezani, tunaita “kutoa heshima” na tunamimina kwenye glasi.

Na tusidanganyane — pombe ni sumu. Sumu yenye jina la kitaalamu ethanol, inayotengenezwa na kimelea ili kuua vijidudu. Sisi binadamu tukasema, “hee, hii nzuri” na tukaanza kuinywa kwenye harusi, matanga, send-off na hata kwenye mikutano ya siasa.

Takwimu siyo mchezo
  • Duniani, pombe inaua watu milioni 3+ kila mwaka.
  • Hii ni zaidi ya waliouawa na vita, ugaidi na ajali za barabarani zikijumlishwa.
  • Tanzania, wastani wa 7% ya vifo vinavyohusiana na ini, moyo au ajali barabarani vinatokana na pombe.
  • Kuna uwezekano mkubwa msafara wa matanga unaouona leo, mmoja wa marehemu alichangia maisha yake kwa bia au spirit fulani.

Inavyokuua taratibu
Pombe ikishafika tumboni, haina huruma — inapita damu yote, inagonga ubongo, moyo na kila kiungo. Ini lako, ambalo ndiyo fundi wa kusafisha sumu, lina uwezo mdogo sana.
Kimea kimoja cha bia = dakika 5 za kazi.
Ukiamua “one for the road” — ujue umeacha sumu ikizunguka mwilini kabla hata hujatoka baa.

Madhara ya muda:
  • Kumbukumbu kushuka, akili kupungua kasi.
  • Ini kujaa mafuta, kuvimba, kisha kukauka kabisa (cirrhosis).
  • Saratani ya koo, tumbo, utumbo na hata matiti.
  • Moyo kufa taratibu.

Haikuhusu wewe peke yako
  • Ajali za barabarani zinazohusiana na pombe = 300,000+ vifo duniani kwa mwaka.
  • Nusu ya wahanga hawakunywa — walikuwa tu kwenye njia ya mtu aliyelewa.
  • Kesi za vipigo, mauaji, na hata ubakaji — pombe mara nyingi ipo mezani.
  • Watoto 600,000 huzaliwa kila mwaka na madhara ya pombe iliyokunywewa na mama akiwa mjamzito.

Uraibu wa kisiri
Watu wengi hudhani uraibu ni kwa walevi wa maskani pekee.
Lakini ukweli ni kuwa nusu ya waraibu wanaonekana watu wa “kawaida” — wavaa suti, wenye familia, wenye kazi.
Bia 3–4 kila siku? Unajiweka kwenye fast track ya magonjwa makubwa, hata kama unajisikia poa.

Kwa nini tunaendelea?
Kwa sababu pombe ina jibu la haraka kwa hofu ya kijamii — inaondoa aibu, inafungua mazungumzo, inafanya watu wapate ujasiri wa ghafla.
Lakini gharama yake? Maisha, afya, na familia nyingi zilizoharibika.

Vijana wanabadilika?
Vizazi vipya kama Gen Z wanakunywa pombe kidogo kuliko wazazi wao.
Lakini pia hawakutani sana, upweke umeongezeka, matatizo ya akili yanapanda.

Sasa swali ni hili: tukiondoa pombe, tutaweka nini badala yake kuunganisha watu?
Au tutabaki na pengo ambalo nalo litatuumiza kwa namna mpya?

Hitimisho
Pombe siyo tu kileo. Ni sumu yenye heshima.
Kama hatutakuwa wakweli, tutajikuta tunapiga vita dawa zingine za kulevya kwa nguvu zote, lakini tunaendelea kusherehekea hii “mnywaji mwepesi” anayetuua taratibu.
Asante mkuu umewakumbusha walevi lkn ni wabishi hao kuacha pombe mi niliacha 2023 siitaki tena
Unatumia nini mkuu mbadala wakee
Niliamua tu nilianza kuacha pombe kesho yake sigara nilikua nimeharibika kwa pombe namshukuru mungu situmii chochote kile
 
Asante mkuu umewakumbusha walevi lkn ni wabishi hao kuacha pombe mi niliacha 2023 siitaki tena

Niliamua tu nilianza kuacha pombe kesho yake sigara nilikua nimeharibika kwa pombe namshukuru mungu situmii chochote kile
Hongera mkuu
 
Shida ni hizi imani zilizokuja na ndege ndiyo zinawapa nguvu watu hoehae kimawazo kujiinua kutoka wajuako wao na mada zao mfu kuhusu vitu wasivyovijua .
Jamani kuna Al sasa hivi nenda hata huko muulize uzuri wa pombe atakuleta machapisho kibao mpaka ushangae ila ndiyo vile huyu rafiki pombe wanapenda kumuonea sana .

Ila kwakuwa marafiki zake tuko wengi hatutakubali
kama bima yako ina cover huduma ya kusafisha figo na damu basi kongole kwako, kama haifanyi hayo basi naweza kusema kitu kimoja tu "Asiyesikia la Mkuu......."
 
kama bima yako ina cover huduma ya kusafisha figo na damu basi kongole kwako, kama haifanyi hayo basi naweza kusema kitu kimoja tu "Asiyesikia la Mkuu......."
Ina cover lakini pia natamani nikutabilie ila naomba uniruhusu maana nimejaaliwa kuona ya sirini hasa kwa watu wanaopenda kunijibu vibaya mimi .
 
Mna kumbuka ule wimbo wa Marioo? Bia Tamu!
Mtoa mada ,uliza hiyo chatgpt itusanue!
Niliachana na pombe mwaka 2014 na hii dhana kwamba bia tamu wala sijawahi kuilewea, nilikua nakunywa kwasababu kampani yangu ilikua inakunywa, nilivyoachana na kundi la walevi na pombe ikapoteza nafasi kwangu
 
Najiuliza kama kweli nitaweza sumu na inaua kwa kiasi hicho mbona kuna watu wamekunywa maisha yao yote na kuishi kwa muda mrefu eengine miaka 100+ na bado wanakinywa? Unless you tell us pombe za sasa nyingi watu huchakachua kwa lengo la kumaximize profit na hapo ndio tatizo la sumu huingia.
Miili yetu imetofautiana, kuna watu hata walishwe sumu ya panya watapona tu ila wengi wetu sasa.....
 
Asante mkuu umewakumbusha walevi lkn ni wabishi hao kuacha pombe mi niliacha 2023 siitaki tena

Niliamua tu nilianza kuacha pombe kesho yake sigara nilikua nimeharibika kwa pombe namshukuru mungu situmii chochote kile
Mimi nakunywa kujifuraisha kuchangamka/ so nakunywaga kunywaga kimtindo
 
Ina cover lakini pia natamani nikutabilie ila naomba uniruhusu maana nimejaaliwa kuona ya sirini hasa kwa watu wanaopenda kunijibu vibaya mimi .
Sijakujibu vibaya, nimekupa tahadhari, uamuzi wa kile unachokiweka mwilini mwako ni wako na vyanzo vyote vya kukueleza madhara yake unavyo kiganjani mwako....... don't kill the messenger if you hate the message that he delivers
 
Shida ni hizi imani zilizokuja na ndege ndiyo zinawapa nguvu watu hoehae kimawazo kujiinua kutoka wajuako wao na mada zao mfu kuhusu vitu wasivyovijua .
Jamani kuna Al sasa hivi nenda hata huko muulize uzuri wa pombe atakuleta machapisho kibao mpaka ushangae ila ndiyo vile huyu rafiki pombe wanapenda kumuonea sana .

Ila kwakuwa marafiki zake tuko wengi hatutakubali
Hatukubariiiii tupo nae rafiki yetuuu huyuuu
 
Sijakujibu vibaya, nimekupa tahadhari, uamuzi wa kile unachokiweka mwilini mwako ni wako na vyanzo vyote vya kukueleza madhara yake unavyo kiganjani mwako....... don't kill the messenger if you hate the message that he delivers
Nimekuelewa kaka basi wewe ni mjanja sana kuna mtu nilisema nitabiri kuhusu yeye hapa hapa jamvini akasema tabiri the rest is history ,wewe umepona kwakuwa kumbe ulikuwa unanishauri na sio kunibeza .

Kaka lakini 2014 pombe nzuri nzuri zilikuwa bado hazizinduliwa mfano kuna pombe inaitwa Hanson choice ,vipi Magic moment yaani ungejaribu kunywa tena ungejutia uamzi wako wa kuacha kaka
 
Hii ni sawasawa na useme umeona cheche imeruka kwenye tenki la mafuta lililo wazi na halijalipuka moto na hivyo unaamini mara zote cheche ikiruka kwenye tenki la mafuta moto hauwaki........ iga afu uje kutueleza baada ya miaka 20
Mimi Nina miaka 50 na Sina tatizo lolote ila Kuna watu hawanywi pombe, soda Wala kula nyama lakini wanaumwa ini, moyo na Figo itoshe kudanganya watu tuache na asili zetu saiv naenda kuwa kibabu Cha kijadi na Nina gigida vinyo ya asili
 
Maana aliyeandika kaja na assumptions na sio fact kama zilivyoandika na vyuo mbalimbali vinavyoheshimika
vyombo vinavyoheshimika? una uhakika gani funding ya vyombo hivyo haitoki kampuni za pombe? unajua kwamba hata kampeni nyingi za utunzaji mazingira zinafadhiliwa na wachafuzi wakubwa wa mazingira i.e. BP oil inamwaga mafuta ya kutosha baharini lakini wakati huo huo itakuambia "usitupe mifuko ya plastic"
 
Back
Top Bottom