Pombe: Sumu inayoua zaidi kuliko vita na gonjwa lolote, lakini tunaiita burudani

Pombe: Sumu inayoua zaidi kuliko vita na gonjwa lolote, lakini tunaiita burudani

Niliachana na pombe mwaka 2014 na hii dhana kwamba bia tamu wala sijawahi kuilewea, nilikua nakunywa kwasababu kampani yangu ilikua inakunywa, nilivyoachana na kundi la walevi na pombe ikapoteza nafasi kwangu
Hata mimi nilikuwa mlevi wastani.Nilikuwa nakunywa smart gin (visungura) Kila nikilala usiku.Lengo lilikuwa ni kuitumia kama dawa ya usingizi.Aisee bila kujua nikawa mlevi.

Nilihangaika kuacha bila mafanikio hadi siku moja nikabuni kinywaji mbadala. Kinywaji hicho ni juisi ya ndimu. Aisee ndani ya siku 10 tu kiu ya pombe ikakata. Hadi Leo sijagusa pombe.

Aisee hiki kitu tusiguse tena.
 
Ila unakufa pia.

Hoja ya msingi ni kuishi ukiwa unateseka, unaishi ukitibu sukari, au figo. Hii ya kufa sio hoja maana ulizaliwa na utakufa.
Haya mambo ni magumu sana kuyaelewa. Kuna ndugu zangu wengi wameteseka na matatizo ya ini na figo, na hata pombe hawajawahi nusa katika maisha yao. Mie baba yangu mkubwa, ambaye ametwaliwa akiwa na umri wa miaka 96, maisha yake yote amekunywa gongo kule kijijini mpaka uzee wake. Anavuta bangi anamkia shambani analima mpaka jioni. Akirudi anapiga gongo yake analala. Lakini waliokuwa hawanywi, mfano baba yangu mzazi, alifariki mapema tu kabla ya kaka yake. Ni vigumu sana kuhusianisha suala la kufeli kwa viungo, au kufa mapema na unywaji wa pombe. Nadhani kuna mambo mengi zaidi yanayochangia.
 
Haya mambo ni magumu sana kuyaelewa. Kuna ndugu zangu wengi wameteseka na matatizo ya ini na figo, na hata pombe hawajawahi nusa katika maisha yao. Mie baba yangu mkubwa, ambaye ametwaliwa akiwa na umri wa miaka 96, maisha yake yote amekunywa gongo kule kijijini mpaka uzee wake. Anavuta bangi anamkia shambani analima mpaka jioni. Akirudi anapiga gongo yake analala. Lakini waliokuwa hawanywi, mfano baba yangu mzazi, alifariki mapema tu kabla ya kaka yake. Ni vigumu sana kuhusianisha suala la kufeli kwa viungo, au kufa mapema na unywaji wa pombe. Nadhani kuna mambo mengi zaidi yanayochangia.
Upo sawa. Ila pombe ni adui wa figo japo miili inatofautiana.
 
Kuna vitu duniani ukivisikia vinaua, unajua moja kwa moja havina mjadala.
Sumu ya panya? Unakimbia. Risasi? Unakimbia. Lakini pombe? Tunaweka mezani, tunaita “kutoa heshima” na tunamimina kwenye glasi.

Na tusidanganyane — pombe ni sumu. Sumu yenye jina la kitaalamu ethanol, inayotengenezwa na kimelea ili kuua vijidudu. Sisi binadamu tukasema, “hee, hii nzuri” na tukaanza kuinywa kwenye harusi, matanga, send-off na hata kwenye mikutano ya siasa.

Takwimu siyo mchezo
  • Duniani, pombe inaua watu milioni 3+ kila mwaka.
  • Hii ni zaidi ya waliouawa na vita, ugaidi na ajali za barabarani zikijumlishwa.
  • Tanzania, wastani wa 7% ya vifo vinavyohusiana na ini, moyo au ajali barabarani vinatokana na pombe.
  • Kuna uwezekano mkubwa msafara wa matanga unaouona leo, mmoja wa marehemu alichangia maisha yake kwa bia au spirit fulani.

Inavyokuua taratibu
Pombe ikishafika tumboni, haina huruma — inapita damu yote, inagonga ubongo, moyo na kila kiungo. Ini lako, ambalo ndiyo fundi wa kusafisha sumu, lina uwezo mdogo sana.
Kimea kimoja cha bia = dakika 5 za kazi.
Ukiamua “one for the road” — ujue umeacha sumu ikizunguka mwilini kabla hata hujatoka baa.

Madhara ya muda:
  • Kumbukumbu kushuka, akili kupungua kasi.
  • Ini kujaa mafuta, kuvimba, kisha kukauka kabisa (cirrhosis).
  • Saratani ya koo, tumbo, utumbo na hata matiti.
  • Moyo kufa taratibu.

Haikuhusu wewe peke yako
  • Ajali za barabarani zinazohusiana na pombe = 300,000+ vifo duniani kwa mwaka.
  • Nusu ya wahanga hawakunywa — walikuwa tu kwenye njia ya mtu aliyelewa.
  • Kesi za vipigo, mauaji, na hata ubakaji — pombe mara nyingi ipo mezani.
  • Watoto 600,000 huzaliwa kila mwaka na madhara ya pombe iliyokunywewa na mama akiwa mjamzito.

Uraibu wa kisiri
Watu wengi hudhani uraibu ni kwa walevi wa maskani pekee.
Lakini ukweli ni kuwa nusu ya waraibu wanaonekana watu wa “kawaida” — wavaa suti, wenye familia, wenye kazi.
Bia 3–4 kila siku? Unajiweka kwenye fast track ya magonjwa makubwa, hata kama unajisikia poa.

Kwa nini tunaendelea?
Kwa sababu pombe ina jibu la haraka kwa hofu ya kijamii — inaondoa aibu, inafungua mazungumzo, inafanya watu wapate ujasiri wa ghafla.
Lakini gharama yake? Maisha, afya, na familia nyingi zilizoharibika.

Vijana wanabadilika?
Vizazi vipya kama Gen Z wanakunywa pombe kidogo kuliko wazazi wao.
Lakini pia hawakutani sana, upweke umeongezeka, matatizo ya akili yanapanda.

Sasa swali ni hili: tukiondoa pombe, tutaweka nini badala yake kuunganisha watu?
Au tutabaki na pengo ambalo nalo litatuumiza kwa namna mpya?

Hitimisho
Pombe siyo tu kileo. Ni sumu yenye heshima.
Kama hatutakuwa wakweli, tutajikuta tunapiga vita dawa zingine za kulevya kwa nguvu zote, lakini tunaendelea kusherehekea hii “mnywaji mwepesi” anayetuua taratibu.
If you don't drink beer, at least own a house or a car. Have something to show for your "good behavior". Not being a sober brokee
 
If you don't drink beer, at least own a house or a car. Have something to show for your "good behavior". Not being a sober brokee
It's not a matter of economics my brother but health
Although an exception, I've known a drunkard who was exceptional with money management
 
Unajua ni kwa nini Mungu Alimuumba mbu - kiumbe mkorofi ambaye anaua binadamu wengi kuliko kiumbe mwingine ye yote?

Unajua ni kwa nini plagues na pandemics hutokea mara moja moja katika historia na kuishia kuua mamilioni ya watu?

Ukipata jibu basi mjumlishe na binadamu humo humo. Na usiishie katika pombe tu. Kuna sigara na bidhaa zingine za tumbaku - bidhaa zinazomletea kansa za kila aina. Nenda mpaka kwenye soda na ultra processed foods. Mavita yake anayopigana. Na mwisho wa maneno ni masilaha ya nyuklia ambayo yanaweza kumwangamiza kabisa.

Acha watu wanywe. Ni njia mojawapo ya nature kujibalansi yenyewe. Watu bilioni nane sasa. Bila kifo dunia karibu itaelemewa ndiyo maana kila mwanasayansi anaamini dunia iko overdue kwa pandemic ambayo itapunguza watu bilioni kadhaa. Au tukio kubwa kama njaa ya dunia nzima au hata dunia kugongwa na jiwe kubwa mf. Apophis; na mabadiliko makubwa ya mfumo wa hali ya hewa na mengineyo.

Acha watu wanywe pombe. Wavute sigara. Anopheles wazaliane kwa wingi. Mabomu ya nyuklia yaripuke...it is just mother nature taking care of herself.
Na ndio opportunities huzalishwa, hence ecosystem balances
 
Back
Top Bottom