Hakuna cha ku-promote demokrasia au uongozi bora bali ni kupigania maslahi ya Marekani kiuchumi.
Marekani anajaribu kupambana na China ambayo kwa sasa imejenga Addis-Djibouti railway ili kusafirisha bidhaa mpaka bandari ya Djibouti ambapo iko karibu na Pakistani kwenye Arabian Sea ambapo pia China inajenga reli (Silk Road) kutoka bandari ya Gwandar-Pakistani mpaka China(China-Pakistan Economic Corridor-CPEC)
Senegal anaenda kwa sababu ya kambi za kijeshi za Marekani "zinayopambana na Islamic terrorist" katika nchi za Magharibi mwa Afrika.
Angola anaenda kwa sababu ya malighafi kama mafuta na almasi ambazo makampuni ya Marekani kama ExxonMobil na Chevron yanapambana kuhakikisha nchi ya Ufaransa na Ureno hainufaiki nazo.
Rais wao, Abraham Lincoln aliwahi kusema, "You can fool all the people some of the time and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time".
Hiyo nchi ya Ethiopia juzi tu imepitisha sheria kali ya mitandao ambayo kifungo chake ni miaka 5. Sasa huyu Pompeo tunayeambiwa anaenda ''ku-promote demokrasia na utawala bora'' upi kwenye nchi kama Ethiopia?
View attachment 1357877