Labda me nitoe ushuhuda kidogo kwa sababu nilikuwepo siku aliyokamatwa shekh ponda na nililishuhudia tukio la kukamatwa kwake mwanzo mpaka mwisho..
Kwa kweli sikumbuki siku wala tarehe ila ilikuwa ni pale temeke katika msikiti wa tungi, kwa wanaoufahamu msikiti huu kwa huku temeke unaitwa msikiti wa harakati, kwa maana harakati nyingi za kiislam hususani za jumuiya na taasisi kwa huku temeke huwa zinaanzia hapa.
Pale msikitini pia kuna kambi ya wanafunzi wakidato cha nne na cha sita ambao wanajiandaa na mitihani so, na mimi nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi ambao walijiunga katika kambi msikiti huo ili kujiandaa na mtihani wa kidato cha nmne mwaka jana, 2012.
Ilikuwa kama mida ya saa sita hivi kuelekea saa saba, kumbuka tayari tulikuwa katika kipindi cha mitihani ya mwisho ya kitaifa hivyo katika muda huu tulikuwa tunajisomea na kuna baadhi ambao walikuwa wameala, kambini kwetu kulikuwa na wanafunzi takribani 84. Katika muda huo kuna watu wawili ambao waliingia mule ndani msikitini kwa kasi ya ajabu, huku mmoja akipiga makelele "vijana amkeni tujitetee" "vijana amkeni tujitetee", kiukweli kwa kasi ambayo waliigia nayo na hayo makele hakuna mtu ambaye aliendelea kusoma wala kulala.
kumbe wale wawili mmoja alikuwa ni shekh ponda ambaye sura yake tulianza kuionaa akijuika nasi pale msikitini katika mida ile mibovu kama siku tatu nyuma hivi, huyu mmoja mwengine alikuwa ni dereva wa pikipiki ambaye ndo alikuwa anamuendesha shekh kutoka huko walikotoka(eneo la markaz, chang'ombe) na sasa walikuwa wanafukuzwa na polisi, baada ya wao kuingia ndani huko nje tukawa tunasikia sauti za amri "fungua geti haraka"(polisi wakimuamrisha mlinzi wa geti la msikiti ambaye alifunga geti baada ya shekh kupita na pkipiki yao)
Sasa mule ndani kukawa battle field kati ya polisi na tuliokuwepo ndani, polisi hawakuwa wanajua kama mle msikitini kuna kambi ya wanafunzi hivyo kipindi shekh anatuamsha tujitetee polisi walidhani sisi ni walinzi wa shekh.
Alisikika polisi mmoja akisema "wakileta vurugu piga risasi" mwengine "lala chini" kwa hiyo kukawa pata shika nguo kuchanika. kitu kingine kilichotuweka kwenye wakati mgumu ni kwamba polisi hawakuwa wanamtambua shekh ponda kwa sura na ukizingatia ilikuwa usiku basi hali ikawa mbaya zaidi.
Polisi walikuwa wameandamana na bwana mmoja mwenye asili ya kiarabu ambae ndo inasemekana yeye alimtambua shekh ponda na ndiye aliyekuwa akifuatilia nyendo zake tangu harakati za kule markaz zilipoanza.
Tukiwa wanafunzi wote chini ya ulinzi wa polisi na yule bwana akifanya kutupekuwa kwa sura mpaka pale walipompata mtuhumiwa wao, jamaa walimchukua katika mazingira magumu sana. Yule bwana(shekh ponda) amebobea katika michezo ya karate hivyo haikuwa rahisi sana kumkamata kama kuku wa kizungu. kwa macho yangu nilishuhudia polisi kama watatu kama si wanne wakienda chini kwa mapigo yenye ufundi wa hali ya juu, lakini mwishoni waliweza kumdhibiti na kuondoka nae.
my take: ule utaratibu wa polisi kuja kuwakamata mashekh msikitini kisha mkaingia na viatu mpaka ndani huwa mnaamsha hisia kali sana toka kwa waumini kama nilivyoshuhudia katika tukio lile.