Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ponda anatakiwa abakie lupango kwa sababu ni mtu hatari kwa jamii. Anahamasisha watu kutotii utawala na kutaka kuishi kwa ubabaishaji kwa kupandikiza chuki za dini. Ni m'babaishaji na hatari kwa sababu licha ya kutokua na elimu ya dini yake (inadaiwa hajui kusoma kurani) lakini anajidai sheikh na kila wakati kujipachika uongozi kwa waislamu. Ni bora kuwa na utawala wa sheria hata kama ni chini ya CCM kuliko kila mtu kuchukua sheria mkononi.Jaman hakuna haja ya kutumia nguvu nying kusambaratisha maandamano ya waislam Criminal Procedure Act inaelekeza makosa gani mtu hapewi thamana.pia mazingira ambayo mtu hapewi thamana. Ila kama kuna mazingira ambayo ponda hapewi thaman nafikiri uhuru kenyatta anayetuhumiwa kuua mamia ya watu asingekuwa kwenye kampen. Mpen Ponda bail akatunze familia yake.
Lazima tuwe makini sana kama tutashangilia kwa sheikh Ponda kunyimwa dhamna leo usi shangaa kesho Dr Slaa akikamatwa na kunyimwa dhamana, sheikh ponda alikamatwa kwa kuvamia kiwanja na kusababisha mali ya mwenye kiwanja kuibiwa na si vinginevyo hayo mengine yametoka wapi? na jua wakristo wengi wana hasira nae sana hasa ukizingatia ilifatia uchomaji wa makanisa mbalimbali lakini tuwe makini kushabikia tu....
mi mtoa mada ni mkristo sina hulka ya ubaguzi. Naamin maandamano yatamtoa ponda jumatatu.
Lazima tuwe makini sana kama tutashangilia kwa sheikh Ponda kunyimwa dhamna leo usi shangaa kesho Dr Slaa akikamatwa na kunyimwa dhamana, sheikh ponda alikamatwa kwa kuvamia kiwanja na kusababisha mali ya mwenye kiwanja kuibiwa na si vinginevyo hayo mengine yametoka wapi? na jua wakristo wengi wana hasira nae sana hasa ukizingatia ilifatia uchomaji wa makanisa mbalimbali lakini tuwe makini kushabikia tu....
Lulu kauwa bila kukusudia kapewa dhamana, shehe Ponda kafanya nini kikubwa kisichstahili dhamana, dhamana ni haki ya kila mtu, apewe haki yakr
Kwa sababu ni muislam,kila baya litakufuata hv sasa na ya uraia pia yamerudi tena,sasa sijui mwanzoni uchunguzi walioufanya walikosea,angekuwa padri huyu,tusingeona comment za namna hii. Acheni ubaguzi kila mtu lazima apewe haki yake na si kuzusha vitu visivyo na msingi ili anyimwe dhamana.
Mbaya zaidi wengi wetu tunaangalia dini yake tuna sahau kuwa kinacho mtokea Ponda kina weza kumtokea mtanzania mwingine kesho na tutapanga kuandamna na kujidai kudai haki...Nakuunga mkono 100%,kama kashitakiwa na kosa aliloshitakiwa nalo linastahili dhamana kwa nini asidhaminiwe ? huwezi kumshitaki kwa uvamizi na uporaji wa kiwanja then dhamana ukaangalie habari za ugaidi
Nimetoa mfano tu lakini anaweza kuwa crashwise na crashwise sio kiongozi zaidi ya uongozi wa familia yake lakini kama kosa aliloshitakiwa nalo lina mruhusu kupewa dhamna kwanini anyimwe...kama ni udini wao CCM ndiyo wameulea mpaka hapa tulipo fika sasa ponda hayuko je udini hakuna au hata kule Geita ponda alikuwepo...Huwezi linganisha hata kidogo Dr Slaa na Sheikh Ponda. Dr Slaa ni kiongozi wa chama cha kisiasa, Ponda anaongoza kitu gani ?
Nilikuwa naongea za jamaa mmoja wa usalama akaaza kujitapa kuwa mwisho wake umefika kwani wamesha mfatilia kuwa si mtanzania bali ni mnyarwanda aliingia nchi akiwa mdogo akaishi huko kigoma nikajiuliza kwanini nchi hii ukiwa kinyume na watu walioko kwenye system lazima uambiwe wewe siyo mtanzania..lakini kwa kuwa nilikuwa nataka kujua mengi kutoka kwa huyo ---- wa usalama nilibaki kumsikiliza tu...Kwa sababu ni muislam,kila baya litakufuata hv sasa na ya uraia pia yamerudi tena,sasa sijui mwanzoni uchunguzi walioufanya walikosea,angekuwa padri huyu,tusingeona comment za namna hii. Acheni ubaguzi kila mtu lazima apewe haki yake na si kuzusha vitu visivyo na msingi ili anyimwe dhamana.
Lulu hana effect kwenye usalama wa nchi,bt shekhe Ponda ni Tishio kwa usalama wa nchi.now dar imepoa watu wana amani,enzi zile akiwa nje kila ijumaa ilikuwa ni mshike mshike!nachojiuliza mpaka kesho,why waislamu wanapenda kulazimisha wasio waislamu au wa imani yao kufata mambo ya imani yao?can someone tell me please?
Kwa kosa lipi sasa, tumeona vikundi mbalimbali vikipigania haki zao wanazo amini zimeporwa ni kama alivyo kuwa anafanya ponda kama ni uharifu mbona hata wanachama wa yanga mara ngapi wamekuwa wakivamia nyumbani kwa viongozi wao na kutishia kuua mbona sijaona kukamatwa kwani inatofauti gani na lichokuwa anakifanya ponda...Kabla hajapewa dhamana aasiwe kwanza. Wenzie wamemruka sasa sijui anatetea umma upi?
Waswahili watu wabaya sana walimpump wee sasa wamemuachia kitanzi ajitoe mwenyewe.
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Nimetoa mfano tu lakini anaweza kuwa crashwise na crashwise sio kiongozi zaidi ya uongozi wa familia yake lakini kama kosa aliloshitakiwa nalo lina mruhusu kupewa dhamna kwanini anyimwe...kama ni udini wao CCM ndiyo wameulea mpaka hapa tulipo fika sasa ponda hayuko je udini hakuna au hata kule Geita ponda alikuwepo...