PONDA apewe dhamana

PONDA apewe dhamana

Status
Not open for further replies.
Ponda anahatarisha usalama wa nchi!so mie nnaona sawa tu acha akae ndani tu mpaka kesi yake ihishe
 
Jaman hakuna haja ya kutumia nguvu nying kusambaratisha maandamano ya waislam Criminal Procedure Act inaelekeza makosa gani mtu hapewi thamana.pia mazingira ambayo mtu hapewi thamana. Ila kama kuna mazingira ambayo ponda hapewi thaman nafikiri uhuru kenyatta anayetuhumiwa kuua mamia ya watu asingekuwa kwenye kampen. Mpen Ponda bail akatunze familia yake.
Ponda anatakiwa abakie lupango kwa sababu ni mtu hatari kwa jamii. Anahamasisha watu kutotii utawala na kutaka kuishi kwa ubabaishaji kwa kupandikiza chuki za dini. Ni m'babaishaji na hatari kwa sababu licha ya kutokua na elimu ya dini yake (inadaiwa hajui kusoma kurani) lakini anajidai sheikh na kila wakati kujipachika uongozi kwa waislamu. Ni bora kuwa na utawala wa sheria hata kama ni chini ya CCM kuliko kila mtu kuchukua sheria mkononi.
 
Hivi gaidi anaweza kupewa dhamana kweli? Akipewa dhamana nitazidharau sheria za Tanzania
 
jamani huyu ponda si ndo Msangi amesemema asitolewe selo kwa ajili ya usalama wake? halafu nasikia ana kaharufu cha alshababy. Yaani wamwache kwanza apumnzike huko
 
Lazima tuwe makini sana kama tutashangilia kwa sheikh Ponda kunyimwa dhamna leo usi shangaa kesho Dr Slaa akikamatwa na kunyimwa dhamana, sheikh ponda alikamatwa kwa kuvamia kiwanja na kusababisha mali ya mwenye kiwanja kuibiwa na si vinginevyo hayo mengine yametoka wapi? na jua wakristo wengi wana hasira nae sana hasa ukizingatia ilifatia uchomaji wa makanisa mbalimbali lakini tuwe makini kushabikia tu....
 
Nakuunga mkono 100%,kama kashitakiwa na kosa aliloshitakiwa nalo linastahili dhamana kwa nini asidhaminiwe ? huwezi kumshitaki kwa uvamizi na uporaji wa kiwanja then dhamana ukaangalie habari za ugaidi
 
mkuu inaonekana, na njaa kali sana, maana ponda alikua dili kwako, tafuta kazi nyingine ya kufanya mkuu, kazi zipo nyingi tu za kufanya
 
huyu ponda ndiye yule aliyefukuzwa uarabuni kwa kosa la kushiriki mambo ya ugaidi? kama ni yeye basi hakuna haja ya dhamana ya aina yoyote
 
Lazima tuwe makini sana kama tutashangilia kwa sheikh Ponda kunyimwa dhamna leo usi shangaa kesho Dr Slaa akikamatwa na kunyimwa dhamana, sheikh ponda alikamatwa kwa kuvamia kiwanja na kusababisha mali ya mwenye kiwanja kuibiwa na si vinginevyo hayo mengine yametoka wapi? na jua wakristo wengi wana hasira nae sana hasa ukizingatia ilifatia uchomaji wa makanisa mbalimbali lakini tuwe makini kushabikia tu....

Huwezi linganisha hata kidogo Dr Slaa na Sheikh Ponda. Dr Slaa ni kiongozi wa chama cha kisiasa, Ponda anaongoza kitu gani ?
 
Lulu kauwa bila kukusudia kapewa dhamana, shehe Ponda kafanya nini kikubwa kisichstahili dhamana, dhamana ni haki ya kila mtu, apewe haki yakr

Lulu hana effect kwenye usalama wa nchi,bt shekhe Ponda ni Tishio kwa usalama wa nchi.now dar imepoa watu wana amani,enzi zile akiwa nje kila ijumaa ilikuwa ni mshike mshike!nachojiuliza mpaka kesho,why waislamu wanapenda kulazimisha wasio waislamu au wa imani yao kufata mambo ya imani yao?can someone tell me please?
 
Kwa sababu ni muislam,kila baya litakufuata hv sasa na ya uraia pia yamerudi tena,sasa sijui mwanzoni uchunguzi walioufanya walikosea,angekuwa padri huyu,tusingeona comment za namna hii. Acheni ubaguzi kila mtu lazima apewe haki yake na si kuzusha vitu visivyo na msingi ili anyimwe dhamana.

We unaongea upuuzi tu kwa hiyo kikwete anamtesa mwislamu mwenzake? mkuu wa polisi saidi mwema je si mwislamu?unadhani hana uwezo wa kumtoa ponda akitumia cheo chake, jaji mkuu je c mwislamu,wewe hujui unachoongea fot your information waislamu wenyewe wanatamani ponda afilie mbali fuatilia maelezo ya bakwata. Shehe mkuu kaongea nn kuhusu ponda waislamu wa kweli wanajua madhara ya ponda na hawataki kumwona uraiani tena,,acha nikuvunje moyo kwamba msahau kabisa ponda hukumu itakaposomwa utakaa chini ulie ponda akiachiwa huru nakuhakikishia mm nitaacha kazi ni kitu kisichowezekana ponda kutoboa kila kitu kiko sawa kumhusu na hili litakuwa fundisho kwenu alqaida wameanza na ponda subirini wengine mtamfuata kama mmemmisi, sikinde wee.
 
Nakuunga mkono 100%,kama kashitakiwa na kosa aliloshitakiwa nalo linastahili dhamana kwa nini asidhaminiwe ? huwezi kumshitaki kwa uvamizi na uporaji wa kiwanja then dhamana ukaangalie habari za ugaidi
Mbaya zaidi wengi wetu tunaangalia dini yake tuna sahau kuwa kinacho mtokea Ponda kina weza kumtokea mtanzania mwingine kesho na tutapanga kuandamna na kujidai kudai haki...
 
Huwezi linganisha hata kidogo Dr Slaa na Sheikh Ponda. Dr Slaa ni kiongozi wa chama cha kisiasa, Ponda anaongoza kitu gani ?
Nimetoa mfano tu lakini anaweza kuwa crashwise na crashwise sio kiongozi zaidi ya uongozi wa familia yake lakini kama kosa aliloshitakiwa nalo lina mruhusu kupewa dhamna kwanini anyimwe...kama ni udini wao CCM ndiyo wameulea mpaka hapa tulipo fika sasa ponda hayuko je udini hakuna au hata kule Geita ponda alikuwepo...
 
Kabla hajapewa dhamana aasiwe kwanza. Wenzie wamemruka sasa sijui anatetea umma upi?
Waswahili watu wabaya sana walimpump wee sasa wamemuachia kitanzi ajitoe mwenyewe.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kwa sababu ni muislam,kila baya litakufuata hv sasa na ya uraia pia yamerudi tena,sasa sijui mwanzoni uchunguzi walioufanya walikosea,angekuwa padri huyu,tusingeona comment za namna hii. Acheni ubaguzi kila mtu lazima apewe haki yake na si kuzusha vitu visivyo na msingi ili anyimwe dhamana.
Nilikuwa naongea za jamaa mmoja wa usalama akaaza kujitapa kuwa mwisho wake umefika kwani wamesha mfatilia kuwa si mtanzania bali ni mnyarwanda aliingia nchi akiwa mdogo akaishi huko kigoma nikajiuliza kwanini nchi hii ukiwa kinyume na watu walioko kwenye system lazima uambiwe wewe siyo mtanzania..lakini kwa kuwa nilikuwa nataka kujua mengi kutoka kwa huyo ---- wa usalama nilibaki kumsikiliza tu...
 
Lulu hana effect kwenye usalama wa nchi,bt shekhe Ponda ni Tishio kwa usalama wa nchi.now dar imepoa watu wana amani,enzi zile akiwa nje kila ijumaa ilikuwa ni mshike mshike!nachojiuliza mpaka kesho,why waislamu wanapenda kulazimisha wasio waislamu au wa imani yao kufata mambo ya imani yao?can someone tell me please?

Usibishane na domokaya kwani hujui tafsiri ya huyo domokaya mpuuze tu.
 
Kuna yule jamaa anayesema watu flani wachinjwe alitakiwa apelekwe huko haraka. anawezaje kuhamasisha watu

wachinje wengine kirahisi namna ile tena kupitia mihadhara, cd nk. Mtembezi ana cheka tu eti anakemea, anatakiwa

kuchukuwa hatua vinginevo makubwa yanakuja na atapata aibu kubwa hata huo mkakati wa ndoto ya ukatibu mkuu

UN...maana akili za mtembezi kuruka ruka analenga kuaaffect intenational relation, akilenga madaraka... - ni upuuzi tu!

Serikali imemchekea sasa tunaona mavuno mchungaji kachinjwa. Hawa watu wanatishia utanzania wetu si wa kuchekea

kabisa wao kwao ni huko mahabusu wasiruhusiwe kuja mitaani kunajisi amani yetu.
 
Kabla hajapewa dhamana aasiwe kwanza. Wenzie wamemruka sasa sijui anatetea umma upi?
Waswahili watu wabaya sana walimpump wee sasa wamemuachia kitanzi ajitoe mwenyewe.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Kwa kosa lipi sasa, tumeona vikundi mbalimbali vikipigania haki zao wanazo amini zimeporwa ni kama alivyo kuwa anafanya ponda kama ni uharifu mbona hata wanachama wa yanga mara ngapi wamekuwa wakivamia nyumbani kwa viongozi wao na kutishia kuua mbona sijaona kukamatwa kwani inatofauti gani na lichokuwa anakifanya ponda...
 
Nimetoa mfano tu lakini anaweza kuwa crashwise na crashwise sio kiongozi zaidi ya uongozi wa familia yake lakini kama kosa aliloshitakiwa nalo lina mruhusu kupewa dhamna kwanini anyimwe...kama ni udini wao CCM ndiyo wameulea mpaka hapa tulipo fika sasa ponda hayuko je udini hakuna au hata kule Geita ponda alikuwepo...

Mfano mfu huo mazee..! Madhara ya Ponda kuwa nje ni makubwa kuliko tunavyofikiria. Alitumika sana yeye na shekhe mmoja anaitwa Kudecha kupiga kampeni za CCM baadaye wakawa hakuna wa kuwagusa angalia shida tunayoivaa ya udini, tuanze sasa kushughulika na hawa magugu kwenye ngano kama Ponda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom