Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,528
- 3,352
Ahlanbik:
Kongole kwa kocha zoran maki kwa kupata ushindi wake wa kwanza katika ligi kuu ya NBC hapo nchini Tanzania dhidi ya Geita Gold. Pia pongezi nyingi kwake kwa kumtoa nje kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika ,the so called "legend" ,Jonas Mkude.
Ni muda mrefu sasa mchezaji huyo mlevi asiyejituma uwanjani amekuwa akijiona kuwa ni untouchable katika kikosi cha simba kitendo kinachompelekea kucheza kifadha uwanjani.
Mkude amekuwa na uchezaji wa kizamani, uchezaji wa kidingi,kupoozesha mpira,kutokukimbia na kukaba kwa macho,vitendo vinavyochangia kuidhohofisha simba na kuifanya isifikie kilele cha mafanikio katika bara la Africa.
Zoran Maki amekuja na falsafa ya mpira wa kasi ambao ni mlima mrefu kwa kiungo mvivu mvivu kama Jonas Mkude. Zoran anahitaji kuona movements za wachezaji wake pindi wakiwa na mpira na wasipokuwa na mpira,kitendo ambacho amekuwa hakioni kwa mtu kama Jonas Mkude. Muda umefika sasa kwa mkude kuachana na simba na kwenda kwenye timu za chini kama Azam au Kmc.
Simba haihitaji aina ya viungo kobe, ambao ni wazito kukimbia wawapo na mpira ama wasipokuwa na mpira. Muda wa mabadiliko ndio huu.
Salamu zimfikie mshambuliaji namba nne wa klabu wa simba, Babu John Bocco na ndugu yake kutoka kigoma, Mzamiru Yasin. Wakati wenu wa kuendelea kuitumikia Simba umekwisha ,simba inahitaji mabadiliko.
Nikiripoti kutoka ktk jiji la Bergamo nchini Italy ni mimi mchambuzi wenu wa masuala ya soka, Tipstiptor.