Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe
Kwa muda mrefu nchi yetu Tanzania, imekuwa ikibagazwa na media za nje, haswa za kibeberu kwa kuripoti na kutoa taarifa za uongo, uzushi na wakati mwingine hata kututukana Tanzania kama nchi, kuwatukana viongozi wetu na kumdhalilisha mkuu wetu wa nchi na kuibagaza nchi yetu.
Yote haya yakitokea, Balozi zetu kwenye hizo nchi tunakobagazwa, zipo, lakini huwa ziko kimya, hazijibu chochote!.
Msemaji wetu wa serikali pia na yeye hukaa kimya, na mara moja moja akijitokeza kukanusha kwa kuitisha press conference kukanushia vyombo vya habari vya ndani na sio kule tuliko bagazwa!.
Mfano mzuri ni hii video jongefu ya CNN kuibagaza Tanzania, imerushwa CNN, imeonekana dunia nzima, msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akakanusha kwa press conference kwenye local media, nini kinatuzuia kukanushia kule kule walikotubagaza?.
Kwa muda mrefu nimekua nikiandika kuwa kauli zinaumba, uongo ukisemwa sana kuhusu Tanzania, kwenye media za nje, alafu ukaachwa bila kukabushwa, sio tuu dunia itauamini uongo huo kwa kuuona ni ukweli, bali kauli hizo za uongo, zitauumbia uongo huo kugeuka ukweli.
Moja ya uongo wa media za nje enzi ya Magufuli ni uongo kuwa Magufuli atafuta vyama vingi,
The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja Uongo huu ulinyamaziwa, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, vyama vingi vikafutika kweli Bungeni!.
Hoja za Nchi yetu kubagazwa, serikali yetu kubezwa na Rais wetu kudhalilishwa, nimeziandika sana humu
Nikashauri serikali yetu iwe proactive kujibu uongo wa media zozote za nje kuhusu Tanzania, na tukanushie kwenye hizo hizo media zinazotubagaza.
Kama CNN walivyo onyesha documentary ya vurugu za uchaguzi yenye uongo ndani yake, msemaji wa serikali awe na uwezo wa kuijibu CNN na kuwajibia huko huko CNN.
Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea.
Summary kwa hisani ya Mkuu mkata uzi
Big Up Sana Balozi Mobhare Matinyi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali

- Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?
- Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!
- Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
- Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!
- The Economist kuhusu Tanzania: Jarida linaona mapungufu tu kuihusu Tanzania!, Hivi kweli Tanzania hakuna mazuri yotote ya kuyaangazia?!.
- Tanzania yaitwa Rot!, Wapinzani Wahongwa Milioni 60! Zitto Tishio kwa JPM, Wasomi Wetu Waitwa "Sycophantic Academics"!, is This True?, Is it Fair?.
- Rais Magufuli ametukanwa tena na Jarida la Economist. Tukiendelea kunyamaza, itafika siku Uongo huu utageuka Ukweli!
- Jarida la The Economist Kwa Uongo Limekubuhu, Laja na Uongo Kuhusu EAC Ladai TZ na Kenya Hazielewani. PK na YM Hawaivi, Burundi Kando!.
- Jarida la Economist lamwaga mboga kuhusu muungano: The status of Zanzibar, Imperfect union
- GE2020 - Uongo na Upotoshaji huu wa BBC London kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni una maana gani? Sio mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa ki-BBC?
Nikashauri serikali yetu iwe proactive kujibu uongo wa media zozote za nje kuhusu Tanzania, na tukanushie kwenye hizo hizo media zinazotubagaza.
Kama CNN walivyo onyesha documentary ya vurugu za uchaguzi yenye uongo ndani yake, msemaji wa serikali awe na uwezo wa kuijibu CNN na kuwajibia huko huko CNN.
Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea.
Summary kwa hisani ya Mkuu mkata uzi
Muhtasari wa alichokifanya Balozi Matinyi:
Balozi Mobhare Matinyi, Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, aliamua kujibu moja kwa moja na kwa uwazi taarifa za upotoshaji zilizoituhumu Tanzania kuwa haijaendelea kwa sababu ya Ujamaa na matumizi mabaya ya misaada. Baada ya gazeti la Aftonbladet la Uswidi kuchapisha madai hayo kufuatia uamuzi wa Uswidi kusitisha misaada, Balozi Matinyi aliandika majibu rasmi kwenye gazeti hilo hilo na kwa lugha ya Kiswidi.
Katika majibu yake:
- Alikanusha madai kuwa Tanzania imeshindwa kimaendeleo kwa sababu ya Ujamaa.
- Alitetea maendeleo ya Tanzania katika elimu, afya, miundombinu, nishati, uchumi na uwekezaji.
- Alisisitiza kuwa Tanzania inahama kutoka kwenye utegemezi wa misaada kwenda biashara na uwekezaji
JE ALIYOYASEMA YANAENDANA NA HALI YETU HALISI ?
Hiki alichokifanya Balozi Matinyi, kiigwe na mabalozi wetu wote, Tanzania ikibagazwa, tusikae kimya, tujibu mapigo, kuanzia sasa, miongoni mwa sifa za mabalozi wetu, iwe ni pamoja na uwezo wa kujibu mapigo kuitetea nchi.Taarifa ya Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, kujibu uongo huo kwa kuukanisha kwa kuelezea ukweli wa mafanikio ya Tanzania kwenye maendeleo ya uchumi kwa miaka 60 iliyopita, kwa kuijibu taarifa ya upotoshaji kwenye gazeti la Aftonbladet la Sweden iliyochapishwa kwa lugha ya Kiswidi, na Balozi Mobhare Matinyi akaijibu kwa lugha hiyo hiyo ya Kiswidi kwenye gazeti hilo hilo.
Serikali ya Uswidi baada ya kupitia vipaumbele vyake vya sera za mambo ya nje na changamoto za kiusalama, ilitangaza uamuzi wa kufuta misaada yake ya ushirikiano wa maendeleo na nchi tano ikiwemo Tanzania, kabla ya mwisho wa mwaka 2026, na hivyo kuhitimisha misaada iliyodumu kwa miongo kadhaa.
Hata hivyo, wakati Uswidi ikiwa na demokrasia ya vyama vingi na kujali ustawi katikati ya ubepari, Tanzania ilichagua kufuata mfumo wa demokrasia ya chama kimoja kinachofuata Ujamaa wa Kiafrika ambayo ilisisitiza kujitegemea.
Tangazo la hivi majuzi la Serikali ya Uswidi, bila kukusudia, liliibua simulizi iliyoipotosha taswira ya Tanzania na mafanikio yote ya ushirikiano huu wa fahari. Ilidaiwa kuwa nchi zilizotajwa "zimekuwa zikifuata Ujamaa mno" kwa miongo mingi na matokeo yake "hazijaendelea".
Balozi Matinyi alisema "Niseme wazi vizuri kabisa: Kauli hiyo haiendani na Tanzania kwa namna yoyote ile, hata kwa fikra tu"
Aliendelea, "Hebu tuangalie ukweli: Mwanzoni mwa miaka ya 1960 Tanzania ilikuwa na chuo kikuu kishiriki kimoja tu, lakini leo ina vyuo vikuu 36 vilivyosajiliwa na vyuo vikuu vishiriki 16. Uswidi, kwa upande wake, leo ina vyuo vikuu 18 vilivyosajiliwa na vyuo vikuu vishiriki 12. Kwa hakika, ikiwa na takribani watu milioni 70, Tanzania bado inahitaji vyuo vikuu zaidi ikilinganishwa na Uswidi yenye watu milioni 10.7.
Wakati huo Tanzania ilikuwa na vituo kutolea huduma za afya 1,343 zikiwemo hospitali 96 na vituo vya afya 22. Leo Tanzania ina vituo vya aina zote vya kutolea huduma za afya 13,606 zikiwemo hospitali 473 na vituo vya afya 1,348.
Balozi Matinyi ameshukuru kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Karolinska ya jijini Stockholm na Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyo pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.
Ikiwa katika ukanda wa kimkakati wa mwambao wa Afrika Mashariki, Tanzania inahudumia nchi kadhaa zisizo na bandari kupitia bandari zake kuu nne za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga na Zanzibar, na hivi karibuni itaanza ujenzi wa bandari kubwa ya Bagamoyo. Pia kuna bandari kadhaa kwenye maziwa makuu matatu ya Afrika, Victoria, Tanganyika na Nyasa. Mtandao mkubwa wa barabara na reli wa Tanzania ni miongoni mwa mitandao yenye ufanisi mkubwa barani Afrika na unaendelea kukua.
Tunaipongeza Serikali ya Uswidi kwa kuunga mkono kwa njia mbalimbali mradi wetu wa reli ya kisasa (SGR), reli ya kwanza inayotumia umeme Afrika Mashariki na Kati. Kwa sasa reli hiyo inafanya kazi kati ya Dar es Salaam na mji mkuu Dodoma. Miradi zaidi ya reli katika maeneo ya kaskazini na kusini mwa nchi, ambayo kimsingi itaunganisha nchi zaidi na bahari ya Hindi, iko mbioni.
Baada ya miaka michache, Tanzania itakuwa kitovu kikubwa cha nishati baada ya kukamilisha mradi wa gesi asilia na kampuni ya Norway, Equinor, wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 42. Aidha, mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki linaloanzia Uganda hadi bandari ya Tanga unakaribia kukamilika.Vilevile, Tanzania, ambayo inazalisha maelfu ya megawati za umeme kwa kutumia mitambo ya nguvu za maji, imejiandaa vizuri kutumia vyanzo vingine vya nishati mbadala kama jotoardhi, upepo na jua. Kadhalika, Tanzania ina akiba kubwa ya makaa ya mawe inayokadiriwa kufikia tani bilioni 1.9.Mtazamo wa uchumi wa Tanzania pia ni wa kuvutia.
Ingawa Pato lake la Taifa linakaribia dola bilioni 90, ukuaji wa uchumi kama inavyoshuhudiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Mikopo ya Mauzo ya Nje la Uswidi (EKN) umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 5-7 kila mwaka tangu mwaka 2000. Nchi zingine zenye uchumi imara kama Uswidi, yenye Pato la Taifa la dola bilioni 630, imepata ukuaji hasi mara mbili ndani ya miaka mitano iliyopita. Mnamo Julai 2020, Tanzania ilihitimu kutoka nchi za kipato cha chini na kuingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati, ambayo kwa mujibu wa Benki ya Dunia inaashiria maendeleo makubwa ya uchumi na utulivu kwa miongo miwili. Haya ni matunda ya mageuzi ya mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambayo yaliipeleka nchi katika uchumi mchanganyiko, na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, mchakato unaohitaji miongo kadhaa kukomaa.
Tanzania ilipokea korona za Uswidi milioni 560 mwaka 2024, takriban dola milioni 60 za Marekani, kama msaada kutoka Uswidi. Lakini Tanzania sasa inahama kutoka kwenye misaada kwenda kwenye biashara na uwekezaji; hivyo, inakaribisha wawekezaji wa Uswidi katika sekta muhimu kama viwanda, huduma, madini, utalii, kilimo na teknolojia.
Ni dhahiri kuwa, katika mwaka unaoishia Septemba 2025, Tanzania ilikusanya dola bilioni 4.43 kutokana na dhahabu, bidhaa inayoongoza kwa mauzo ya nje nchi, huku ikitarajia utalii utaleta dola bilioni 6.0 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025. Tanzania kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa utalii wa mbugani kwa mwaka wa tatu mfululizo, ikijivunia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro na fuko maridadi za Zanzibar.
Tanzania ina hifadhi kubwa ya madini muhimu ikishika nafasi ya tatu barani Afrika na ya sita duniani. Ufini inatusaidia katika utafutaji na utafiti wa utajiri huu wa kipekee, ambao kwa hakika utainua uchumi wetu. Uswidi inahimizwa kutumia fursa za kujenga mitambo ya kuchenjua madini nchini.
Mwaka 2024 pekee, Tanzania ilivutia uwekezaji wa moja kwa moja wenye thamani ya dola bilioni 9.31 kutokana na miradi 901 iliyosajiliwa, na nchi hii inajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 140.
Pamoja na mafanikio haya, serikali ya sasa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mikakati zaidi ili kuwaletea Watanzania maendeleo thabiti na endelevu.
Hivyo basi, kwa dhati kabisa, kwa uchumi wenye sekta nyingi na unaofuata soko huria huku ukionesha ukuaji stahimilivu wa kuvutia, kuibagaza Tanzania kwamba "imelowea kwenye Ujamaa usio na maendeleo" si sahihi na ni upotoshaji.
Big Up Sana Balozi Mobhare Matinyi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali