MD SPECIAL
JF-Expert Member
- Jul 4, 2025
- 1,161
- 2,812
Huyu mama hasafishiki hata kwa dawa wananchi wampende, keshaloa damu za watanzania.
Leo tarehe 29 October, 2026 ni kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kilichotokea October 29, 2025. Mimi naiadhimisha siku hii kwa kutafakari kwa kuyatembelea mabandiko yangu, ya post October 29, 2025.Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe
Nikashauri serikali yetu iwe proactive kujibu uongo wa media zozote za nje kuhusu Tanzania, na tukanushie kwenye hizo hizo media zinazotubagaza.
Kama CNN walivyo onyesha documentary ya vurugu za uchaguzi yenye uongo ndani yake, msemaji wa serikali awe na uwezo wa kuijibu CNN na kuwajibia huko huko CNN.
Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea.
Hiki alichokifanya Balozi Matinyi, kiigwe na mabalozi wetu wote, Tanzania ikibagazwa, tusikae kimya, tujibu mapigo, kuanzia sasa, miongoni mwa sifa za mabalozi wetu, iwe ni pamoja na uwezo wa kujibu mapigo kuitetea nchi.
Big Up Sana Balozi Mobhare Matinyi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali