Pongezi Balozi Wetu Sweden, Mobhare Matinyi. Alichofanya Kiigwe na Kifanywe na Balozi Zetu Zote

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe
Kwa muda mrefu nchi yetu Tanzania, imekuwa ikibagazwa na media za nje, haswa za kibeberu kwa kuripoti na kutoa taarifa za uongo, uzushi na wakati mwingine hata kututukana Tanzania kama nchi, kuwatukana viongozi wetu na kumdhalilisha mkuu wetu wa nchi na kuibagaza nchi yetu.

Yote haya yakitokea, Balozi zetu kwenye hizo nchi tunakobagazwa, zipo, lakini huwa ziko kimya, hazijibu chochote!.

Msemaji wetu wa serikali pia na yeye hukaa kimya, na mara moja moja akijitokeza kukanusha kwa kuitisha press conference kukanushia vyombo vya habari vya ndani na sio kule tuliko bagazwa!.

Mfano mzuri ni hii video jongefu ya CNN kuibagaza Tanzania, imerushwa CNN, imeonekana dunia nzima, msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akakanusha kwa press conference kwenye local media, nini kinatuzuia kukanushia kule kule walikotubagaza?.

Kwa muda mrefu nimekua nikiandika kuwa kauli zinaumba, uongo ukisemwa sana kuhusu Tanzania, kwenye media za nje, alafu ukaachwa bila kukabushwa, sio tuu dunia itauamini uongo huo kwa kuuona ni ukweli, bali kauli hizo za uongo, zitauumbia uongo huo kugeuka ukweli.

Moja ya uongo wa media za nje enzi ya Magufuli ni uongo kuwa Magufuli atafuta vyama vingi,
The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja Uongo huu ulinyamaziwa, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, vyama vingi vikafutika kweli Bungeni!.

Hoja za Nchi yetu kubagazwa, serikali yetu kubezwa na Rais wetu kudhalilishwa, nimeziandika sana humu

Nikashauri serikali yetu iwe proactive kujibu uongo wa media zozote za nje kuhusu Tanzania, na tukanushie kwenye hizo hizo media zinazotubagaza.

Kama CNN walivyo onyesha documentary ya vurugu za uchaguzi yenye uongo ndani yake, msemaji wa serikali awe na uwezo wa kuijibu CNN na kuwajibia huko huko CNN.

Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea.

Summary kwa hisani ya Mkuu mkata uzi
Hiki alichokifanya Balozi Matinyi, kiigwe na mabalozi wetu wote, Tanzania ikibagazwa, tusikae kimya, tujibu mapigo, kuanzia sasa, miongoni mwa sifa za mabalozi wetu, iwe ni pamoja na uwezo wa kujibu mapigo kuitetea nchi.

Big Up Sana Balozi Mobhare Matinyi.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Kazana , jaribu, utakumbukwa yeuzi zijazo.
70 yrs. Bado Dar hakuna maji
 
Wafunge ubalozi kabisa basi.
 
Kutetea upumbavu ni upumbavu!
 
Muhtasari wa alichokifanya Balozi Matinyi:

Balozi Mobhare Matinyi, Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, aliamua kujibu moja kwa moja na kwa uwazi taarifa za upotoshaji zilizoituhumu Tanzania kuwa haijaendelea kwa sababu ya Ujamaa na matumizi mabaya ya misaada. Baada ya gazeti la Aftonbladet la Uswidi kuchapisha madai hayo kufuatia uamuzi wa Uswidi kusitisha misaada, Balozi Matinyi aliandika majibu rasmi kwenye gazeti hilo hilo na kwa lugha ya Kiswidi.

Katika majibu yake:
  • Alikanusha madai kuwa Tanzania imeshindwa kimaendeleo kwa sababu ya Ujamaa.
  • Alitetea maendeleo ya Tanzania katika elimu, afya, miundombinu, nishati, uchumi na uwekezaji.
  • Alisisitiza kuwa Tanzania inahama kutoka kwenye utegemezi wa misaada kwenda biashara na uwekezaji

JE ALIYOYASEMA YANAENDANA NA HALI YETU HALISI ?
 
Matinyi sijui malinyi yuko vizuri, mwambie aende na ICC akayabagaze mabeberu ya Hague maana yako yamamalizia uchambuzi ili kuona kama Samia the Butcher ana cha kuyazuia yasimshughulikie.


Wewe mzee unazeeka vibaya sana
 
Thanks for this
P
 
“Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea”.

Kwa kusoma post yako iliyojaa ujinga, nina uhakika wa asilimia mia moja uwezi thibitisha serikali ya Sweden. Imesitisha misaada kwa sababu ulizozitaja.

Pili pamoja na kusifiana ujinga humu, hujui kuandika (walau unatakiwa kuwa mfano humu). Huwezi kuandika paragraph ambayo aina sentence hata mbili.

How you are supposed to a prominent writer, is beyond me. Only in Tanzania.

Deep down you are just shallow.

Mna namna yenu ya kusifiana ujinga humu.
 
Pascal Mayalla wewe ni MSƏNGE
 
Sweden wameamua tuu kuwa wastaarabu na kuwasitiri sababu ndiyo nature ya wazungu.

The truth is, Tanzania has long been in a politics of deceit, self enrichment, betrayal and corruption.

Huyo Balozi alichokifanya ni kumfurahisha bosi kwa kuwananga Sweden na pesa zao. Pesa zinaliwa na familia chache, viongozi wana ukwasi wa kutisha na matumizi ya anasa kwa pesa za wahisani.

Viongozi bongo hii wanaiba pesa, kujilimbikizia mali na kujipa mafao ya anasa kuwawezesha kuishi maisha ya anasa wao na vizazi vyao.

Tuwe wakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…