Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe
Nikashauri serikali yetu iwe proactive kujibu uongo wa media zozote za nje kuhusu Tanzania, na tukanushie kwenye hizo hizo media zinazotubagaza.
Kama CNN walivyo onyesha documentary ya vurugu za uchaguzi yenye uongo ndani yake, msemaji wa serikali awe na uwezo wa kuijibu CNN na kuwajibia huko huko CNN.
Nchi ya Sweden imetangaza kuifutia Tanzania misaada ya Sweden kwa kutoa sababu za uongo kuwa Tanzania hatutumii vizuri misaada ya Sweden kwasababu ya Siasa ya Ujamaa na kujitegemea.
Hiki alichokifanya Balozi Matinyi, kiigwe na mabalozi wetu wote, Tanzania ikibagazwa, tusikae kimya, tujibu mapigo, kuanzia sasa, miongoni mwa sifa za mabalozi wetu, iwe ni pamoja na uwezo wa kujibu mapigo kuitetea nchi.
Big Up Sana Balozi Mobhare Matinyi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali