Pongezi kwa Mkenya aliyemwandikia Raila hotuba hii

kadoda11

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
21,453
Reaction score
20,746
Aliyeandika hii lazima atakuwa ni mkenya anayeimudu vizuri sana lugha adhimu ya kiswahili au atakuwa ni mtanzania aliyepata kandarasi maalum ya kumuandika mzee raila(BABA) masuala yanayohitaji uwasilishaji wa lugha ya kiswahili.

na kama ni mkenya, basi labda atakuwa ni MK254. Kiswahili safi sana.

isome neno kwa neno.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119]


Hii hotuba nadhani aliitoa akiwa maeneo ya pwani ya Kenya
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119]


Hii hotuba nadhani aliitoa akiwa maeneo ya pwani ya Kenya
bado mkenya wa pwani hawezi kuandika kiswahili safi kama hiki.hapo lazima kutakuwa na mkono wa mtz au ni mkenya aliyeishi sana dar es salaam.[emoji23]
 
Ila wenyewe huwa wanasema kiswahili chetu ndi kina makosa.
 
bado mkenya wa pwani hawezi kuandika kiswahili safi kama hiki.hapo lazima kutakuwa na mkono wa mtz au ni mkenya aliyeishi sana dar es salaam.[emoji23]
Huyu kweli kapata mafunzo tz, japo bado vijineno vichache vya kikenya havipotei!


Jasiri haachi asili
 
Sioni kosa kwenye hilo sentensi.

Kosa ulilofanya ni hili hapa

"Wakenya wengi tu wana uwezo wa kuandika kiswahili aina hicho, mimi nikiwemo mmoja wa magwiji wa lugha hili huku Kibera"
 
Hehehe!! Shukrani kadoda11 kwa kunihusisha na uandishi huu kwenye makala ya Raila, lakini samahani sio mimi na zaidi huwa sihusiki kabisa kwenye kampeni za wanasiasa.
Japo pia inafaa ikuingie kwamba Wakenya wapo vizuri sana kwenye uandishi wa Kiswahili, kuna somo la insha na uandishi wa Kiswahili Kenya ambalo husomeshwa kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Hii imesaidia kwenye soko la ajira maana Wakenya wameajiriwa hadi nchi za bara Asia ambapo wapo huko wanafundisha Kiswahili.

Ukija Kenya jaribu ujipatie nakala ya gazeti la 'Taifa Leo', humo utaona uwezo, ujuzi na uelewa wa hali ya juu wa uandishi wa lugha ya Kiswahili, na pia habari za saa moja kwenye vituo vyote vya runinga hupeperushwa kwa Kiswahili kilichonyooka hadi basi.

Nikihitimisha, inafaa ifahamike kwamba Kiswahili ni lugha yetu ya taifa, kimetajwa kabisa kwenye katiba. Japo, ni vigumu kuwafungia Wakenya kwenye lugha moja, huwa tunaongea zetu za asili, halafu na Kiswahili na Kingereza pia.
 
Huyu kweli kapata mafunzo tz, japo bado vijineno vichache vya kikenya havipotei!


Jasiri haachi asili
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Jasiri haachi asili wallah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…