Hehehe!! Shukrani
kadoda11 kwa kunihusisha na uandishi huu kwenye makala ya Raila, lakini samahani sio mimi na zaidi huwa sihusiki kabisa kwenye kampeni za wanasiasa.
Japo pia inafaa ikuingie kwamba Wakenya wapo vizuri sana kwenye uandishi wa Kiswahili, kuna somo la insha na uandishi wa Kiswahili Kenya ambalo husomeshwa kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Hii imesaidia kwenye soko la ajira maana Wakenya wameajiriwa hadi nchi za bara Asia ambapo wapo huko wanafundisha Kiswahili.
Ukija Kenya jaribu ujipatie nakala ya gazeti la 'Taifa Leo', humo utaona uwezo, ujuzi na uelewa wa hali ya juu wa uandishi wa lugha ya Kiswahili, na pia habari za saa moja kwenye vituo vyote vya runinga hupeperushwa kwa Kiswahili kilichonyooka hadi basi.
Nikihitimisha, inafaa ifahamike kwamba Kiswahili ni lugha yetu ya taifa, kimetajwa kabisa kwenye katiba. Japo, ni vigumu kuwafungia Wakenya kwenye lugha moja, huwa tunaongea zetu za asili, halafu na Kiswahili na Kingereza pia.