Pongezi ziwafikie raia mwema (jina kapuni) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Timu yake ya Usalama kwa ushirikiano wao jana 5 Oktoba, 2024 ambapo, Saa 9.56 jioni nilipokea ujumbe wa simu kutoka kwa raia mwema mzalendo (jina kapuni) kuwa kwenye gari la abiria (bus) linalojulikana kama Kisbo lenye namba za usajili T408EFH lililokuwa linatokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kulikuwa na abiria binti mdogo aliyekuwa akilia na kuhangaika kwamba ateremshwe maana hajui anakoenda na amepakiwa tu kwenye gari na mtu ambaye hakusafiri naye.
Mara baada ya kupokea taarifa hizi, niliwasiliana na Mheshimiwa Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili afahamu na kuchukua hatua zake ambapo, mara moja alichukua hatua za kuwaelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kufikia majira ya saa 10.30 jioni bus hilo likiwa ndiyo linaingia stendi ya Nzega lilisimamishwa na kukaguliwa na Askari wakiwa na Mhe Mkuu wa Mkoa na binti huyo kubainiwa na mahojiano stahiki kufanyika. Pia rejea video fupi ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tabora hapa chini.
Binti huyo sasa yuko mikono salama chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku hatua zaidi za kubaini kisa mkasa zikiendelea.
PONGEZI; narudia tena kutoa Pongezi kwa raia mwema aliyejali na kuthubutu kutoa taarifa kwa kunitumia ujumbe huo. Hakika mlinzi wa kwanza wa jamii ni jamii yenyewe. Pongezi ziende kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa wepesi wake kwenye kuitikia taarifa niliyompa na kuchukua hatua mara moja. Pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza jukumu lao kikamilifu na kumuokoa binti huyu mdogo na kwa hatua wanazoendelea nazo.
WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.
WITO KWA WAHUDUMU WA USAFIRI; kuwa makini na abiria hususan watoto wadogo wanaopakizwa kwa maelekezo kuwa huko waendako watapokelewa na mtu fulani kwani, tunaishi kwenye nyakati ambazo watoto ni wahanga wakubwa wa ukatili mbalimbali ikiwemo kutoroshwa na kwenda kutumikishwa kinyume na umri wao.
Dr Gwajima siyo kwamba wanaenda kutumikishwa bali wanaenda kutolewa viungo for rituals. Uchaguzi umekaribia, tuwe tuwalinde watoto na ndugu zetu. Inaonekana albino si sili tena bali viungo vya binadamu wadogo ndo vinatakiwa.
Hongera sana Dkt. Gwajima D. Ingekuwa ni kwa matakwa yangu ulifaa sana kwenye Wizara ya Afya najua umebobea kwenye 'health management'. Ulifanya vyema kipindi cha hayati Magu na ziara zako watu walikuwa wahalali kuweka mambo sawa.
Chacha tunampongeza kivipi? Yaani anapongezwa mtu kwa kutimiza wajibu wake, tena kwa issue kama hiyo ambayo ilitakiwa imalizwe na trafiki tu
Kwamba alitoka Tabora kwenda Nzega(km 120) kwa ajili hiyo au issue ilimkuta akiwa Nzega?
Kazi nzuri... Ipo haja ya kuwa na kanuni za kutilia mkazo usafirishwaji wa watoto ili kukabiliana na kadhia hii.
Mfano, anayesafiri na mtoto ahakikiwe ipasavyo na kujiridhisha anakotokea na anakokwenda na ikiwa hakuna jambo baya linalolengwa dhidi ya mtoto husika.
Hongera sana Dkt. Gwajima D. Ingekuwa ni kwa matakwa yangu ulifaa sana kwenye Wizara ya Afya najua umebobea kwenye 'health management'. Ulifanya vyema kipindi cha hayati Magu na ziara zako watu walikuwa wahalali kuweka mambo sawa.