Niweke wazi bandiko langu kuhusu ukak
Nianze kwa kukushukuru mheshimiwa kwa kuchukua wakati wako kuijibu post yangu ambayo niliandika kwa nia njema.
Hii si post yangu ya kwanza kuhusiana na niyaonayo kupelekeshwa kisiasa huku maisha ya watu yakipotea bure.
Kwamba kuna sheria nzuri au mbovu zinazopelekea kupoteza maisha ya watu ambayo yangeweza kuepukika?
Kulikuwa na huu uzi humu:
Serikali ina wajibu wa kuzuia matangazo ya kibiashara ya kidini/imani kwenye vyombo vya habari kulinda raia wake
Na hii hapa ilikuwa post yangu kwenye uzi huo:
View attachment 3116612
Sheria nzuri au mbaya isiyotusaidia ni ya nini?
Tunakupongeza sana tu kwenye mengi mazuri unayofanya kwenye wizara hii. Laiti kungekuwa na wizara mahsusi kwa ajili ya haki, hakika ungetufaa mno huko.
Ila hii ya kuachia miti shamba, maombezi, nk kwa sababu yoyote huku watu wakiangamia; hata wewe mheshimiwa, kwenye karne hii, uhalali wake uko wapi?
Misahafu inasema: "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maalifa."
Hii ndiyo ilikuwa hoja yangu pekee ya dhati hapa.