Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Chacha tunampongeza kivipi? Yaani anapongezwa mtu kwa kutimiza wajibu wake, tena kwa issue kama hiyo ambayo ilitakiwa imalizwe na trafiki tu
Kwamba alitoka Tabora kwenda Nzega(km 120) kwa ajili hiyo au issue ilimkuta akiwa Nzega?
Alikuwa ziara nzega na baada ya taarifa hii akapokea na kutoa kipaumbele kubadili mwelekeo.

Nami nikuulize: kwani mfanyakazi Bora anapopongezwa si huwa ametimiza majukumu yake pia? Au ukipongeza mtu mmoja wa familia yako kwa bidii fulani huwa inakuwaje? Au mtu akifaulu mtihani si inakuwa alitakiwa afaulu tu na ni jukumu lake kusoma? Au
 
Kazi nzuri... Ipo haja ya kuwa na kanuni za kutilia mkazo usafirishwaji wa watoto ili kukabiliana na kadhia hii.

Mfano, anayesafiri na mtoto ahakikiwe ipasavyo na kujiridhisha anakotokea na anakokwenda na ikiwa hakuna jambo baya linalolengwa dhidi ya mtoto husika.
Napokea maoni kwa ajili ya kujumuisha mbele ya meza ya wadau. Ahsante Sana
 
Kama serikali kwa ujumla wake ingekuwa inafanya kazi na kuwajibika namna hii I'm sure robo ya changamoto za taifa hili zizingekuwepo.
Tunamshukuru mh Rais kwa kupendelea kumwamini waziri gwajima, ametufaa mno katika taifa hili, na hii wizara ipo kwa mtu anaye stahili kabisa .
 
Alikuwa ziara nzega na baada ya taarifa hii akapokea na kutoa kipaumbele kubadili mwelekeo.

Nami nikuulize: kwani mfanyakazi Bora anapopongezwa si huwa ametimiza majukumu yake pia? Au ukipongeza mtu mmoja wa familia yako kwa bidii fulani huwa inakuwaje? Au mtu akifaulu mtihani si inakuwa alitakiwa afaulu tu na ni jukumu lake kusoma? Au

Mama yangu!

Hautakaa kamwe umtoshe kila mtu!

Ukweli wengine tumekubali kazi hii njema yako,trafiki na RC bila kumsahau raia aliyetoa taarifa.

Sasa wengine watatafuta mapungufu kwenye hili,hata usijibu hao,wewe sehemu yako umefanya na mtoto yuko salama!

Mama nakutakia jumapili njema yenye amani.
 
WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.
Upo sahihi kabisa Dakitari ila viongozi wengi siyo wepesi kupokea au kutoa ushirikiano kwa simu kama wewe, you are different from them Madam, wananchi wema wapo na nia njema ya kuifikishia serikali taarifa wanayo, kizingiti ni vipi wanawafikishia taarifa na wakabakia safe? Wachache wenye namba zenu za simu ndiyo wanafanikisha haya yaliyoshuhudiwa humu.

Napendekeza Wizara zote ziwe na central phone number ambayo raia wema watafikishia taarifa nyeti huko ili maagizo ya utekelezaji yatokee juu kama ulivyofanya Dada yetu, wewe unafanikiwa sana kwakuwa una karama ya transparence tofauti na viongozi wengine, tunatamani hata Wizara zingine zingeiga utendaji wako wa kazi.

Mungu akubariki sana
 
Shirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi ili kuwa na majibu na kuondoa wasiwasi kwa wananchi,kuhusiana na mambo yanayohusu wananchi kwa ujumla.

Kwa Sasa hivi mambo yamekuwa ndivyo sivyo kuanzia watoto,vijana na hata Wazee kujihusisha na Imani mbovu za kishirikina na Imani z kupata Mali na madaraka.

Badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye kuzuia maandamano,tungekaa na watendaji wa vijiji wananchi wa kawaida kila kata,kila kiongozi haya mambo ya geisha kabisa kama sio kupunguza.

Na elimu itolewe hakuna mtoto kusafiri kama mzigo au Bahasha lazima aambatane na mtu mzima na ijulikane uhusiano wake na ikibidi barua ya huko atokako na namba za simu za huyo aliyeidhinisha barua, Ahsante.
 
Hongera sana Dkt. Gwajima D. Ingekuwa ni kwa matakwa yangu ulifaa sana kwenye Wizara ya Afya najua umebobea kwenye 'health management'. Ulifanya vyema kipindi cha hayati Magu na ziara zako watu walikuwa wahalali kuweka mambo sawa.​
Utumishi wa umma tena wa siasa hauna makao ya kudumu, popote pale kazi. Sasa wengine tumetumika Sana ni wakati wenu sasa kutumika. Nakutakia Kila heri
 
Watoto wawe wanahojiwa sana kwenye mabasi, details zote zipatikane na atakae kiuka achukuliwe hatua
Hili linaweza kumkuta mtoto yeyote hata wa kwetu
Wengi wanaibiwa au kuchukuliwa bila ridhaa hata za wazazi
Mama Dr G hongera sana 🙏 na Mungu akubariki sana
 
Pongezi ziwafikie raia mwema (jina kapuni) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Timu yake ya Usalama kwa ushirikiano wao jana 5 Oktoba, 2024 ambapo, Saa 9.56 jioni nilipokea ujumbe wa simu kutoka kwa raia mwema mzalendo (jina kapuni) kuwa kwenye gari la abiria (bus) linalojulikana kama Kisbo lenye namba za usajili T408EFH lililokuwa linatokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kulikuwa na abiria binti mdogo aliyekuwa akilia na kuhangaika kwamba ateremshwe maana hajui anakoenda na amepakiwa tu kwenye gari na mtu ambaye hakusafiri naye.

Mara baada ya kupokea taarifa hizi, niliwasiliana na Mheshimiwa Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili afahamu na kuchukua hatua zake ambapo, mara moja alichukua hatua za kuwaelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua na kufikia majira ya saa 10.30 jioni bus hilo likiwa ndiyo linaingia stendi ya Nzega lilisimamishwa na kukaguliwa na Askari wakiwa na Mhe Mkuu wa Mkoa na binti huyo kubainiwa na mahojiano stahiki kufanyika. Pia rejea video fupi ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tabora hapa chini.

Binti huyo sasa yuko mikono salama chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora huku hatua zaidi za kubaini kisa mkasa zikiendelea.

PONGEZI; narudia tena kutoa Pongezi kwa raia mwema aliyejali na kuthubutu kutoa taarifa kwa kunitumia ujumbe huo. Hakika mlinzi wa kwanza wa jamii ni jamii yenyewe. Pongezi ziende kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa wepesi wake kwenye kuitikia taarifa niliyompa na kuchukua hatua mara moja. Pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kwa kutekeleza jukumu lao kikamilifu na kumuokoa binti huyu mdogo na kwa hatua wanazoendelea nazo.

WITO KWA JAMII; tuendelee kushirikiana kwenye kubaini na kutoa taarifa za matukio ambayo hayaeleweki na yanaleta maswali kwenye maisha ya jamii kila siku kwani, ni kwa jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano ndiyo tunaweza kuwadhibiti wafanya uovu kwa watoto wetu kabla ya kutimiza nia zao ovu.

WITO KWA WAHUDUMU WA USAFIRI; kuwa makini na abiria hususan watoto wadogo wanaopakizwa kwa maelekezo kuwa huko waendako watapokelewa na mtu fulani kwani, tunaishi kwenye nyakati ambazo watoto ni wahanga wakubwa wa ukatili mbalimbali ikiwemo kutoroshwa na kwenda kutumikishwa kinyume na umri wao. Jumapili njema kwenu wote🇹🇿
Waziri Gwajima, mimi nadhani uongozi ni kuangalia mambo kwa upana na urefu. Nina maana kuwa badala ya ku deal na tatizo moja moja, uongozi uwe ni kuzuia matatizo na kuwe na mifumo maalum ya ku deal na matatizo. Napongeza kabisa ulichokifanya, lakini mimi naona tukio kama hili limetokea kwa sababu ya ku-fail kwa uongozi wa nchi. Je tunaweza kukubali kuwa nchi yetu mifumo yetu ya uongozi ime-fail na tukubali kukaa na kusuka mifumo yetu upya? Je, huko kwenye baraza la mawaziri na CCM kwa ujumla mnaweza kuungana na kuhakikisha Samia baada ya kumaliza muda wake 2025 hapati tena urais kwa sababu hana uwezo wa kuongoza?
 
Sasa haya ndio maneno. Sio kuishia kupongezana tu
 
Mifumo ipo, ni kama tu mifumo mfano ya afya kuhusu kuzuia magonjwa kwa ujumla, bado kuna mifumo ya vituo vya tiba kwa watakaoshindikana kuzuia wakaugua wapokelewe. Pia huko vituo vya tiba wengine watapata dawa watapona wengine wakiwa kwenye dawa hizo hizo hawaponi. Hivyo ni combination. Hata hivyo, Maoni yako yamepokelewa, maboresho ni endelevu daima. Shukrani
 
Back
Top Bottom