Pongezi kwa Sekretatieti ya Ajira kwa kuyachukua maoni yetu na kuyafanyia kazi

Benjamin10

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2016
Posts
409
Reaction score
598
Habarini za usiku wadau,

Ninapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza PSRS kwa hatua ambazo wamechukua juu ya maoni yetu sisi wasaka tonge.

Kwan jion ya leo nimejaribu kuingia kwenye tovuti yao nikakutana na PDF za kutosha kwa watu walioitwa kwenye usahili.

Kwani nimekuta utofauti kidogo.

Majina wameyagawa kwa kanda nne..

1. Zanzibar
2. Dar es Salaam
3.Dodoma
4. Mwanza
5. Mbeya

Na wamewapangia wasailiwa maeneo ya kufanyia usahili kulingana na postal addres yako ilielekeza unatokea maeneo gani.

Naomba niwapongeze kwa hilo
 
Wamefanya vyema,ni wajibu wa interviewers kufanyia fair interviewees... upendeleo usishike hatamu.
 
Na kanda ya kaskazini watukumbuke, Arusha pia tuwekewe usaili wetu.

Arusha mpk Dodoma ni parefu ikumbukwe Arusha pia ni jiji.

Nauli ya chuga to dom 25k times 2, mbali lodge siku 3 mpk nne, mbali kula.

Aisee wangetufikiria na sisi.
 
Sasa wanaenda kwenye kanda zao.. imekua nafuu kidogo..

Wa kagera,kigoma shinyanga simiyu katavi wakutane mwanza..

Arusha singida kilimanjaro moro manyara iringa.. karibuni dodoma..

Ruvuma songwe.. rukwa katavi wakutane mbeya...
Kwa utaratibu huu ulio orodhesha bado haijakaa vyema ndugu.
Singida, manyara wafanye Dodoma.
Tanga, kilimanjaro wafanye Arusha

Nyengine nafikiri zipo sawa
 
Sisi watu wa Moro Dodoma tukafanye nini,tunakwenda Dar,ndio karibu zaidi bloangu,πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰
 
Nmepita Leo asubuhi nimeshangazwa sana.
Hii inafaida nyingi sana.
 
Daahh, kwa hiyo kale kaupepo cha CIVE ndio basi tena....!

Hatua nzuri
Kale kaupepo ukikataka.. tumia adress ya dodoma yaan P.O Box.... dodoma.
Uta
Kwa English hii hao PSRS Wanawakati mgumu sana.

Yaani Grammer ni zero
Saanaa hili suala la grammer ni suala la kitaifa labda awe ameomba kaz ya kufundisha english.
 
Na kanda ya kaskazini watukumbuke, Arusha pia tuwekewe usaili wetu.

Arusha mpk Dodoma ni parefu ikumbukwe Arusha pia ni jiji.

Nauli ya chuga to dom 25k times 2, mbali lodge siku 3 mpk nne, mbali kula.

Aisee wangetufikiria na sisi.
Huu ni mwanzo tu.. naimani wataliona hilo na watalifanyia kaz
Kwa utaratibu huu ulio orodhesha bado haijakaa vyema ndugu.
Singida, manyara wafanye Dodoma.
Tanga, kilimanjaro wafanye Arusha

Nyengine nafikiri zipo sawa
Yeah.. nadhani itakua hivyo.. mimi nilitolea kama mfano
Sisi watu wa Moro Dodoma tukafanye nini,tunakwenda Dar,ndio karibu zaidi bloangu,πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰
Morogoro huichukulia kama ipo kanda ya kati.. maana dodoma to moro ni kama km 256 hivi
 
Watu wa Lindi, mtwara, ,mara,kigoma, KAZI wanayo
 
Naona mnapongeza labda tu hamjapitia documents vizuri mkaona
Bado kuna shida naomba mpitie ile KANDA YA MBEYA angalieni walicho kifanya kwenye sehemu ya usahili wa MAHOJIANO kwa baadhi ya kada, wameweka kituo cha usahili wa mahojiano kwamba ni DODOMA
Sasa kwa akili ya kawaida wamewasaidia nini hao watu wa mbeya, hamuoni kwamba bado ni shida? Mtu atoke katavi aende mbeya akae siku 2 baadae ndani ya siku 1 aende dodoma, huo ni utaratibu wa kijinga sana tena ni usumbufu
 
Daah Dah umeongea kweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…