Unajua nimekaa na kujiuliza hivi uwepo wa mwanadada yule machachari kule US katika zama hizi na haya yanatokea ni coincidence tu au Mungu ana makusudia yake?
Binafsi nimegundua hili jambo halijatokea kwa bahati mbaya tu bali ni mpango wa Mungu kwani haya yote yanayotokea leo hii yeye alishayajua kabla hivyo akaandaa mtu wake kwa ajili ya kusaidia wengine kimawazo, kielimu,n.k katika kukabiliana na hali hii tulioyonayo leo hii.
Katika zamu hizi ambazo uhuru wa kutoa maoni na hata kuabarishana ni jambo la harari,Mungu aliona kuna umuhimu wa kuwapo mtu atakaeweza kusema kwa uhuru na ujasiri kwa niaba ya walio wengi na akamteua huyo binti na kumpa hilo jukumu.
Wako watakaohiji inakuwaje Mungu amtumie mtu mwenye lugha kali kama mwanadada yule?Jibu lao hapa ni kuwa, wakati mwingine Mungu humtumia hata shetani kutimiza alichokipanga maana ni yeye alieruhusu shetani kumjaribu mwanae mpendwa (Yesu Kristo)
Ukweli ni kwamba unaweza kuwa nje ya nchi ila ukakosa ujasiri alionao huyu dada na hata kama utakuwa na huo ujasiri basi commitment aliyonayo dada huyu mtu mwingine unaweza usiwe nayo kabisa maana kushinda mtandaoni huku kila siku unatumiwa mambo mbalimbali ya kuyaweka mitandaoni ni kazi ngumu na inahitaji kujitoa hasa.
Leo hii dada huyu kaamshe wengi hasa wakina mama ambao wengi wao ni wapenzi wa habari za udaku na si habari wanasiasa na siasa ambazo zinazogusa na kuathiri maisha yao ya kila siku moja kwa moja.
Dada huyu kafanya watu wengi zaidi wafuatile siasa;kasaidia ku-create awareness ya mambo siasa na uchumi kwa kiasi kikubwa; kasaidi watu kupata taarifa ambazo pengine wasingezipata kabisa; kawa kiungo kati ya wanasiasa na wananchi; n.k
Tukubali,tukatae;dada huyu ni mpango wa Mungu na ana msaada wa Mungu tofauti na watu wengine wanavyofikiri au kudhani.