Inapendeza... Kila la kheri...

Hiyo inaitwa usitukane mamba... wakati bado hujavuka mto...


Cc: mahondaw
 
Hujiulizi alivyo kuwa mwepesi kwako hatakuwa na mwepesi kwa wengine. Singe maza wanafaa kama huna uwezo wa kupata wanawake wa kawaida.
 
Kuna facts ambazo zipo wazi;

1 . Uwepo wa huyo mtoto ni changamoto kwenye uhusiano mpya ( hili hutaliona sasa ) kuna legal and social implications
2. Wewe si Baba Mzazi wa huyo mtoto na kamwe hutakuwa Baba kwa huyo mtoto, haijalishi utatumia muda na pesa kiasi gani kwenye malezi ya huyo mtoto

3. Uhusiano wako na huyo mama automatically utakufanya mtoto akuzoee na kukuchukulia kama baba, hii itajenga bonding kati yako na mtoto ila kumbuka kinachowaunganisha ni mapenzi yako na huyo mama, siku ikitokea uhusiano wenu ukivunjika hutakuwa na namna ya kuwa tena karibu na huyo mtoto haijalishi utakuwa umemzoea na kumpenda kiasi gani , hii itamuathiri sana huyo mtoto kisaikolojia

4. Kama baba mzazi wa huyo mtoto yupo hai itazidisha ugumu kwenye mahusiano unayotaka kuanzisha, kumbuka kisheria huyo baba ana haki zote za kumuona na kumhudumia mtoto kama akiamua kufanya hivyo hutaweza kumzuia kisheria!

5. Utapata wakati mgumu sana kwenye kumlea huyo mtoto haswa kwenye kumuadhibu atakapokosea, ipo siku mama yake atakuambia MWACHE MTOTO WANGU, hutakuwa na la kufanya maana huyo SI MTOTO WAKO

6. Omba / sali sana huyo mtoto akikua na kuanza kujitambua aendelee kukuheshimu, huwa inatokea akishajua wewe si baba yake mzazi atakutamkia hivyo haswa akifika umri wa balehe hutakuwa na mamlaka ya kumuadhibu
 
Sidhani kama single mother ni jina ama tusi. Tena neno hili sio la kibongo na halijaanzia huku, nashauri njia pekee kuliepuka ni kuacha kuza nje ya ndoa.
 
Siku zote mwanzo wa penzi huwa kuna raha sana unaweza jihisi upo peponi. Na hapa kuna baadhi walibadili dini, wengine waligombana mpaka na wazazi wao. Usije ukafiri siku zote ndiyo itakuwa hivyo. Ndoa za siku nyingi zinavunjika sana sababu wengi wanafikiri ndoa ni ngono na kuambiana i love you. kuna single mother wapo wazuri sana na wengine pasua vichwa
HONGERA KWA MKE NA KWA ZAWADI YA MTOTO. BUY ONE, GET ONE FREE
 
Wala usitetereke na comments za humu..

Nimeona watu wanaingia ndoa ya pili au ya tatu na watoto wao,tena watoto wanajua kabisa huyu ni step dad/mom na wana share malezi,hivyo sioni ugumu wa single mothers kuwa na uhusiano,for any relatiship kitu important ni Chemistry ama Compatibility..ukipata mtu ana great personality anakufanya uwe na furaha then kuwa nae, mtoto chukulia kama ndugu tu wa mkeo,kama unaheshimu na kuwajali ndugu wa mkeo then tatizo liko wapi ukimjali mtoto wa mkeo?
 
Ahsante sana, ila wiki tu unatangaza ndoa? OK all the best
 
Mwaya Mungu awalinde mfikie malengo. Wangekuwa wazungu hapa ungepewa hongera Ila kwa kuwa umeleta swala lako kwa wachawi wasiopenda furaha za watu a.k.a wabongo utakatishwa tamaa wee. Kwani single mother Hana K?? Hana ubongo?? Watu daily wanatoa mimba ili wasionekane wamezaa na tunawajua. Sasa hao Ndio bora? Mwaya km unaona umependa oaa
 

Mbona unamtabiria negative?? Why usimtabirie positive??
 
Huyo aliyemzalisha akamwacha ana akili kweli? Kumwacha mdada mzuri hvyo..beautiful with brain
 
Ahsante sana, ila wiki tu unatangaza ndoa? OK all the best
....Hapo ndio nami pamenishitua Mkuu.
Wiki tu baada ya kufahamiana na bibie ndugu yetu anaona aanze kuzungumzia Mambo ya Ndoa??
WIKI??? [emoji15][emoji15][emoji15]
 
Yote hayo ndani ya mwezi.. Karibu mjini mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…