Pongezi kwenu Single Mothers
Mkuu mbona inaonekana umependa sana then kwa kasi ya 4G, kiwango cha upendo ulichonacho kwa sasa je na uyo singo maza wako amefikia kiwango cha upendo ulichonacho ww kwa sasa isije ukachukua maamuz ya haraka alaf mwenzako yupo 2G, utateseka

Namuelewa vizuri mkuu. Ananiskiliza ile mbaya hata nikimwambia jambo gani anafanya, juzi ametoka kunambia tuchange pesa tunnue kiwanja cha kujengea nyumba. Kiufupi ni wife material
 
Thats exactly my point.

Kama being single sio ubaya, then 'single mother' sio mbaya pia.
Ushawah kumtambua mtu kwa relationship status yake hata siku moja?

Au ndugu yako ambae hana mahusiano ushawa kumuita we single boy/girl as their name?
 
Then why usimuite single parent? Do u real need to describe her as single mother?
 
Habari za saa hizi Wanajamvi.

Leo kuna jambo fulani nataka kushare nanyi, jambo ambalo huenda mnalifahamu au hamlifahamu lakini kwa vyovyote najua kwa mjadala huu mtafahamu zaidi.

Tunatofautiana mitazamo. Kuna mitazamo tofauti tofauti kuelekea swala la kuoa Singo maza (naomba nitohoe najua inapaswa kuwa 'Single mother' ila sipendi kuchanganya lugha).

Kuna watu tumejizatiti hatutaoa singo maza ila hii kitu ni rahisi zaidi kuzungumza kuliko kuweka katika matendo. Kwanini ?

Mara nyingi kumpenda mtu hutokea bila hiari. Bila kuamua na kupatanisha maamuzi yako na mtazamo wako hiyo ndiyo sababu baadhi yetu tumejikuta tukienda kinyume na mitazamo yetu linapokuja swala la kuoa singo maza.

Kwa mtu mwenye malezi mazuri hawezi kukurupuka kupenda kwa sababu ya sifa za nje. Wako wanawake wengo warembo lakini si kila mwanamke ni wife material, wengine wameumbwa kuipamba dunia tu.

Acha nieleze jinsi nilivyozama kwa Singo Maza na kujikuta napuuza mtazamo wangu.

Mwishoni mwa mwezi wa tisa nilipewa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za harusi fulani ya swahiba wangu sana.
Ilikuwa siku ya Jumamos usiku wa hiyo sherehe, wakati sherehe inaendelea na sisi (mimi na kampani fulani ya rafiki yetu) tumekaa kwenye meza ile kwenye meza jirani palikuwa na msichana fulani. Mweupee, mzuri kweli kweli, shape kama la Wema Sepetu. Nilipomuona nikamstua nikampa hi kisha nikakausha maana niliamini sio hadhi yangu ile . Najijua life langu 'dongotee' kula kwa kuunga unga na mishe ziende vizuri ndo nivae. Watoto wazuri kama wale wanataka matunzo.

Basi nikiwa naendelea kushusha bia, nikapaliwa. Bia ikanimwagikia kwenye shati. Shati likachafuka, miongoni mwa watu waliniona hili likitokea ni yule mrembo, rafiki zangu walipoona hili walinicheka sana ila yule mrembo (acha nimwite Asha) aliinuka alipokuwa na kunifata akanipa pole akatoa kitambaa chake akanipa nijifute. Nikakataa akanibembeleza nikaona sooo nikachukua ila sikujifutia chake niliinuka nikaenda msalani. Ila mpaka hapo akawa amenigusa kwa kiasi fulani nikaanza kumuona wife material.

Ama ulikuwa umelewa, ama hujui mke w ndoa anapatikanaje.

Niliporudi nikamuomba namba akanipa. Niliporudi home nilimpigia simu aiseee! tulizungumza mpaka asubuhi, akanambia anaomba alale nikamuacha ila nikamuomba tukutane siku hiyo hiyo (jumapili) akasema sawa tutakutana jioni. Kweli jioni hiyo tukaweza kukutana maeneo fulani hivi ya ubungo tukaenda Bar fulani hivi. Kwanza kujiamini kuliniisha maana toto zuri vile linakubali appointment na mie tena sehemu km ile ila nikajikaza mpaka nikafanikiwa kumtongoza.

Hujui kuwa thamani ya mwanamke ni bikira yake? Sasa huyo aliyezalishwa akaachwa unadhani anajiona mwenye thamani tena? Mbona hata wahuni husema mwanamke akijidai mjanja mzalishe tu, ndio mwisho wa kuringa?

Halafu unaomba namba tu hapo ulevini anakupa!! Wife materiak hawi cheap namna hiyo mkuu, hapo wewe ndio dhaifu wala si yeye. Kacheza na saikolojia yako tu, kakumaliza. Ushahidi ni hapo unaposema ulipojilinganisha naye ulijiona sio wa hadhi yako, tena uliishiwa hata pumzi ya kutongoza, hivyo hukusimama kwenye nafasi yako kama mwanamume.

Hakukataa wala hakunambia chochote ila akasema ntakujibu siku nyingine. Nikaona 'Sawa.' mazungumzo yakaendelea ila sasa katika mazungumzo yake alikuwa mwepesi sana kusema maneno fulani yakuonesha kuwa yeye ni mtu wa dini.

Huyo alishakubali, ila alihitaji kukufanyia hivyo baada ya kukuona ni mgeni wa mapenzi. Hakuna jipya hapo. Hiyo kutaja taja mistari ya kidini ilikufanya uamini ni mcha Mungu, lakini kuna tatizo kubwa. Mcha Mungu asingekubali kukutana nawe baa!! Afu huyo Mungu alimjua kabla ama baada ya kupata mimba? Huyo alikuwa desperate wa kupata ndoa, alikuwa akitafuta mwanamume yeyote amuoe.

Lakini pia alikuwa mwenye ushauri chanya sana na kuonesha uzoefu mkubwa wa maisha jambo ambalo lilinifanya nione huyu ni 'wife material.' Istoshe hakuaguza pombe wala soda ila maji tu na akanambia atalipia yeye, nikasema mke si ndo huyu sasa.

Ni hatari kubwa kuoa mke mwenye uzoefu wa maisha. Aliupata wapi huo uzoefu? Halafu kukulipia bia ndio sifa ya mke wa ndoa?

Baada ya kama wiki moja hivi toka tuanze kuwasiliana mahusiano yakawa yameanza rasmi na kwakuwa nilishazama na KUDATA kwake sana nikaona sasa ni wasaa rasmi wa kupanga maswala ya harusi maana ni wife material haswa: hana lawama, hana mizinga, ata ukimwambia njoo saa nane usiku anaweza akaja, mshauri mzuri na mzoefu sana wa maisha istoshe ni MZURI MNO wa muonekano mpaka shape yaani kama ya wema.

Yaani baada ya kuonana wiki moja tu, unapangandoa!! Nadhani tatizo lakk ni kubwa zaidi. Wewe ni dhaifu wa mapenzi. Wife material haswaa kwa mahusiano ya wiki moja, hujajua hata habari zake mwenyewe, alipataje huyo mtoto, kwa nini baba wa mtoto alimtosa, wazazi wake ni kin nani, anafanya shughuli gani haoo mjini n.k. Wife material unamwita saa nane usiku anakuja, hii ni zaidi ya hatari!! Halafu hiyo shape ya Wema ndio uchafu gani? Ni heri basi ungemsaka wema tu awe mkeo, yaani wewe umedata kwa Wema kuliko huyo mkeo, jitafakari utagundua hilo. Unampima mkeo kwa kupitia Wema, yaani huyo ndio SI unit yako!!

Waswahili wanasema usione vyaelea vimeundwa, tukiwa katika mazungumzo akanambia kuna kitu nataka nikwambie, nikamwambia niambie, basi nilijua anaomba hela(maana hivyo ndivyo nnavowajua wanawake kwa uzoefu wangu) kumbe na tofauti kabisa na hilo. "Mimi nna mtoto," unasemaje ? niliuliza "Nna mtoto ana miaka mitatu, Nimeona bora nikwambie mapema kabla hatujaingia kwenye ndoa".

Miaka mitatu single mama alikuwa anasubiri mwanamume wa aina yako, hongera mkuu. Hakika umepata mke, nikutakie maisha marefu kwenye ndoa yako.

Sasa ndo tunarudi kwenye mada hii, unaweza kuwa na mtazamo fulani kuhusu wanawake wenye watoto, kwamba labda hutooa mwanamke mwenye mtoto katika maisha yako lakini mi nakwambia mwanaume mwenzangu unasema hivyo kwa sababu hujawai PENDA mwanamke mwenye mtoto.

Huko ni kukurupuka kwenye mapenzi kwa kiwango cha SG, bado unahitaji mwongozo zaidi kujua mapenzi ni nini. Ama umri wako ni mdogo bado, ama hukuwa na maelekezo mazuri kuhusu maisha.

Mimi nilikuwa na mtazamo huo huo lakini mpaka kufikia hatua hii ambayo nimependa kiasi hiki, mtazamo wangu nauona wa Kipumbavu sana, najiuliza kwanini nilikuwa naona si vizuri kuoa mwanamke mwenye mtoto ? Hapa saa hizi nawaza namna maisha yatakavyokuwa nitakapokuwa na familia yangu mpya na mtoto wa nyongeza, nna mtazamo mzuri sana kuelekea singo maza wangu na nataka nimpende mwanae kama mwanangu wa kumzaa kwa sababu sasa nimebaini nguvu ya upendo.

Asiyejua maana haambiwi maana, hongera kwa kutoka kwenye upumbavu na kuingia kwenye daraja la werevu. Hongera pia kwa mtoto wa nyongeza, uzazi mgumu siku hizi.

Kama hupendi kuoa singo maza sawa huo ni mtazamo wako, ila Mtazamo wako waweza badilika siku moja ukikutana na mwanamke utakaempenda kweli kweli kama mimi ilivonitokea kwahiyo nikushauri usiseme wala kukashifu watu waliooa masingo maza kama hujui nguvu ya upendo, huenda nawe ukajikuta katika njia hii hii.

Jifunze kuyatawala mapenzi, usiwe mtumwa wa papuchi. Hapo hakuna cha mapenzi wala nini, ni tamaa tu ama lust. Unahitaji msaada kabla hujapotea kabisa.

Singo maza wote jamani nyie watu mna mbinu sana maana leo nimejikuta nakana nilichokishikilia kwa mda mrefu.

Na hizo mbinu ndio zimekunasa, umepoteza hadhi yako kama mwanamume sasa wewe ndio unaolewa hapa.

Mnisamehe wote niliowakwaza kwa kushea swala hili lililonikuta kwa kweli acha tu nikiri kuwa nimedata, na nimebadili mtazamo wangu.

Ila ushauri kwa wanaume wenzangu, usikashifu wala usiweke itikadi ya SITAOA singo maza, maana utajikuta unakana mtazamo wa kukolea kwa singo maza fulani, hii imenitokea kama mipango itakwenda vizuri basi tutaalikana kwenye harusi.

Mnisamehe kwa kuandika maneno meengi. Karibuni kwa mchango wenu.

Story yako wala haisadifu hoja, ingawa unajitahidi kujenga mazingira ya kuoa single mother. Jaribu utunzi wenye ubunifuzaidi ya hiki kituko ulichoandika. Hakuna anayekashifu single mother ila ukweli utasemwa. Nakushauri usome thread inayosema wanaume walioharibika akili, itakupa mwanga kidogo.
 
Kwa kuwa umekiri kuwa ulikuwa mzodoaji mkubwa wa singo madhas, naomba
1. Kujua BABA WA MTOTO yupo hai au amekufa
2. Mama ana mawasiliano wa Baba mtoto
3. Kwanini hakuolewa na aliyemzalisha
4. Nini sababu ya kuzaa kabla ya kuolewa
Majibu yatasaidia kujua hadhi na haiba ya mchumbako!
Bazazi!

1. Yuko hai.

2. Hawana mawasiliano kwa sababu huyu msichana alimuacha yule mzazi mwenzio kwa kuwa msichana hakutaka kutoa mimba.

3. Sababu ya kuzaa kabla ya kuolewa ni uzinzi tu huwa inajulikana hivyo.
 
utakuja kuijutia hii kauli tena unatuponda na kututenga wanaume wenzako tupo hapa ngoja tusubiri mrejesho
Inaonekana unaongozwa na mihemko

Nijutie nini tena mkuu. Huyu ni wife material kabisa tena kitabia anawazidi wanawake wengi sana wasio na watoto
 
Huwez fanya maamuz kwa muda mfupi hv, wanawake ni wajanja sana wakat wa kubembeleza ndoa, ukishamwoa anabadilika kiwango kikubwa mpk utashangaa, nakushauri kaa naye kwa angalau miaka miwili ukimjua in and out (toa mahari, mchumbie), baada ya kuish miaka kadhaa ndyo ufanye maamuzi, vngnevyo utasaga meno.
Asante kwa ushauri ila mkuu huyu msichana ni wife material kabisa yani
 
Ni kweli si neno zuri hata kidogo. Pia tuwe wastaarabu na wenye kujiheshimu kwa kutowazalilisha wanawake wote wenye kulea watoto bila baba wa watoto(bila mzazi mwenzake).
Heshima inaanzia kwa kwako kujitambua na kujiheshimu, kwa mawazo yako, na maneno yako unayoyatamka au kuyaandika, au kuyaongea.
Huko ndiyo kunatwa kuwa na "utu".

Jina au neno "single mother " nashauri lisitumike, Bali jina la mhusika itapendeza zaidi na kuleta heshima kwa kila mmoja wetu.
Niwe mkwel silipend hili neno "Single Mother" nahis kama ni kuwapa ulemavu usiostahili.
 
Huwez fanya maamuz kwa muda mfupi hv, wanawake ni wajanja sana wakat wa kubembeleza ndoa, ukishamwoa anabadilika kiwango kikubwa mpk utashangaa, nakushauri kaa naye kwa angalau miaka miwili ukimjua in and out (toa mahari, mchumbie), baada ya kuish miaka kadhaa ndyo ufanye maamuzi, vngnevyo utasaga meno.
Asante kwa ushauri ila mkuu huyu msichana ni wife material kabisa yani
 
Kwa upande wangu naona upo sahihi kupendana na huyo single mama,ila ushauri wangu umefanya mapema sana kutangaza ndoa

Ni kweli mkuu. Ila sina wasi wasi nae kabisa, anajitambua sana. Huwa ananambia wanaume wengi wanatuogopa kwa sababu wanahisi tutawacheat na ma x wetu jambo ambalo linategemea na akili na utashi wa mtu.
 
Back
Top Bottom