NI MWIKO.
Hii ni code ya enzi za mababu. Kwa zama hizi vijana hawapewi tena a,b,c za maisha, basi wanajiendea tu.
Single mama wapo toka enzi na enzi. Na walikuwa wanaolewa sana, lakini kuna miiko iliwekwa ili kutoharibu "nature of things".
Mwanaume ukioa single mama, hakikisha hana mtoto wa kiume, na kama itashindikana sana, ikatokea ni lazima umuoe, basi hakikisha huyo mtoto habebi ubini wako wala humchukui. Abaki either kwa babu zake au baba yake amchukue.
Hii ni kwa sababu watoto wa kiume ndiyo "wenye miji", hivyo ukikaribisha damu isiyo yako ndani mwako lazima ije na nguvu hasi, maana kwa vyovyote vile energy yake na yenu zitaanza kushindania utawala.
Kwa upande wa watoto wa kike, hao hawana madhara yoyote hata wakibeba ubini wako au hata ukiwalea. Watoto wa kike ni wa "miji ya watu", ikimaanisha kwamba mtoto wa kike nyumbani kwako haleti msigani wowote ule katika mambo ya nature of things.
View attachment 3260576
View attachment 3260577