Pongezi mbalimbali za viongozi kwa Ushindi wa Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti mpya CHADEMA

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Wakuu

Viongozi mbalimbali wameendelea kutuma salamu za pongezi kwa Tundu Lissu baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Taifa.


Kupitia ukurasa wake wa X, Luhaga Mpina amesifu namna CHADEMA wameweza kumpata Mwenyekiti wao.

Ameandika “Hivi ndivyo mwenyekiti wa chama anavyopatikana. Kuna funzo kubwa sana kwetu.”



Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, na wengine wamempongeza Freeman Mbowe kwa ushindani ulioutoa katika mchakato wote wa Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA na amempongeza zaidi Mbowe yeye binafsi kwa mchango wake mkubwa katika siasa za mageuzi za Tanzania na CHADEMA





 
Kiukweli kabisa, Kwa yeyote kama una akili TIMAMU na sio Chawa, utakubali kua kilichofanyika Dodoma ulikua ni UHUNI.

Na Kwa mara ya kwanza kabisa, CCM INASIMAMISHA WAGOMBEA WASIOKUA NA MVUTO KWA RAIA.
 
Akionesha kutoridhika na utaratibu wa upatikanaji wa Mwenyekiti wa Chama chake bwana Luhaga Mpina amempongeza Lisu akisema wataendeleza Kwa undani mazungumzo Yao na kwamba eti Vyama vingine vijifunze huko Kwa kina Chadema wa juzi.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFHorfVN-Lf/?igsh=dWswamt0dnlrMDF1
My Take
Bwana Mpina aambiwe ukweli tuu kwamba kama haridhiki ajiengue CCM kuliko kuishi kinafikia nafiki kama Mchawi 😆😆

View: https://www.instagram.com/reel/DFCZ2fPMzUe/?igsh=NzFrMzFncDJ5bHF4
 
Zitto ni mnafiki!
Hata salamu zake ni za kinafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…