Pongezi nyingi kwa Prof. Eliamani Sedoyeka kwa Mapinduzi ya Maendeleo (IAA Mkuu WA Chuo)

Pongezi nyingi kwa Prof. Eliamani Sedoyeka kwa Mapinduzi ya Maendeleo (IAA Mkuu WA Chuo)

Slim

Senior Member
Joined
Nov 12, 2008
Posts
183
Reaction score
271
Leo natamani kutoa pongezi zangu za dhati kwa kaka yangu, Prof. Eliamani Sedoyeka, kwa kazi kubwa na ya mfano anayoifanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Kumbukumbu zangu zinarudi nyuma mbali sana, wakati ninaingia Kidato cha Kwanza katika shule ya ufundi ya Moshi Technical School (Moshi Tech), yeye akiwa Kidato cha Nne.

Tangu enzi hizo alikuwa ni mtu wa maono, lakini mapinduzi makubwa anayoyafanya sasa hivi katika sekta anazozitumikia ni ya kupongezwa na kila mtanzania. Kazi zake, ubunifu, na juhudi zake katika kuleta maendeleo ya vitendo zinaonekana wazi. Ni mtu anayeacha alama popote anapokanyaga na kuleta mabadiliko ya kimkakati yenye tija kwa taifa.

Kupitia jukwaa hili, rai yangu kwa Serikali yetu sikivu ni hii: Watu wenye weledi, uzalendo, na kasi ya namna hii kama ya Prof. Sedoyeka wanapaswa kuendelea kuangaliwa, kuaminiwa, na kupewa nafasi kubwa zaidi. Nchi yetu inahitaji vichwa kama hivi vinavyowaza maendeleo na mabadiliko chanya ya haraka ili kusukuma mbele gurudumu la taifa letu.

Hongera sana Kaka Prof. Eliamani Sedoyeka, tunajivunia sana juhudi zako na tunakuombea kila la heri katika utumishi wako! ila Mpande dah



 
Leo natamani kutoa pongezi zangu za dhati kwa kaka yangu, Prof. Eliamani Sedoyeka, kwa kazi kubwa na ya mfano anayoifanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Kumbukumbu zangu zinarudi nyuma mbali sana, wakati ninaingia Kidato cha Kwanza katika shule ya ufundi ya Moshi Technical School (Moshi Tech), yeye akiwa Kidato cha Nne. Tangu enzi hizo alikuwa ni mtu wa maono, lakini mapinduzi makubwa anayoyafanya sasa hivi katika sekta anazozitumikia ni ya kupongezwa na kila mtanzania. Kazi zake, ubunifu, na juhudi zake katika kuleta maendeleo ya vitendo zinaonekana wazi. Ni mtu anayeacha alama popote anapokanyaga na kuleta mabadiliko ya kimkakati yenye tija kwa taifa. Kupitia jukwaa hili, rai yangu kwa Serikali yetu sikivu ni hii: Watu wenye weledi, uzalendo, na kasi ya namna hii kama ya Prof. Sedoyeka wanapaswa kuendelea kuangaliwa, kuaminiwa, na kupewa nafasi kubwa zaidi. Nchi yetu inahitaji vichwa kama hivi vinavyowaza maendeleo na mabadiliko chanya ya haraka ili kusukuma mbele gurudumu la taifa letu. Hongera sana Kaka Prof. Eliamani Sedoyeka, tunajivunia sana juhudi zako na tunakuombea kila la heri katika utumishi wako! ila Mpande dah



A very wise man,
Amenifundisha IFM.
Aisee naona mengi sana anayafanya hapo IAA, kuna ioe program ya masters ya one year naona hata TIA wameiga baada ya kuona wanapigwa bao la ujazo mkubwa na IAA!! Congrats Prof.
 
Back
Top Bottom