Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Paschal, waandishi wa habari wenzako wanatekwa na kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.Wewe umeona uje kivyako ili kunusuru maisha yako. Hatakama ni woga, wako umevuka mipaka. Ulicho andika huku mitaani tunakiita: Sifa za kijinga.
 
Kiukweli kunahitajika elimu kwa Watanzania kusoma ripoti. Mwaka 2000-2011 was the data collection period, unaweza kukuta kwa data hizo, kwa mwaka huo, wala Tanzania haikuongoza. Date of publication ndio hii ya Dec, 2019. Hii maana yake Tanzania ndio inayoongoza sasa kwa ripoti ya mwaka huu.

Mimi nina watoto 10!. Tukifanya research ya members wa jf wenye watoto wengi kwa mwaka huu wa 2019, naweza kuongoza. Ikichapishwa Ripoti ya "Wana JF Wenye Watoto Wengi 2019", jina langu likaongoza. Ukiangalia niliwapa lini, huwezi kuja na hoja kuwa tangu 2015 tayari nilikuwa na watoto 10, hivyo hiyo rekodi ni 2015!. Ripoti ikitoka mwaka huu, mimi nikaongoza kuwa na watoto wengi, haijalishi walizaliwa lini, bingwa wenu nitakuwa ni mimi, unless aje mwenye watoto 11!.

Sasa katika ripoti ya mwaka huu ya WB kuhusu kiwango cha kupungua umasikini duniani, Tanzania ndio tumeongoza sio kwa nchi za East Africa, Sio kwa nchi za Bara la Africa, bali tumeongoza kwa dunia nzima!. Haijalisi data zilikuwa collected lini, bali ripoti ndio imechapishwa sasa na ni ripoti ya mwaka huu!.
P
 
Paschal, waandishi wa habari wenzako wanatekwa na kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.Wewe umeona uje kivyako ili kunusuru maisha yako. Hatakama ni woga, wako umevuka mipaka. Ulicho andika huku mitaani tunakiita: Sifa za kijinga.
Waandishi hao ni wangapi tanzania?
Usiseme waandishi bali tuambie ukweli kwamba wale ni mamluki na wanakumbana na madhara ya umamluki tu!

Mao ze dong kule china ali akiwa anaijenga China,alikuwa akiwatandika shabaekeza hadharani wasaliti na mamluki wote na ndio matokeo ya china hii tuionayo sasa!

Nyinyi hapa mnaendekeza mitandao ya kusaka madaraka na kujipanga kuturudisha kulekule kwenye wizi.

The truth ni kwamba JPM NDIE MKOMBOZI WA WATANZANIA 2025 [emoji1241][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mayalla. Wewe ni msomi na watu wengi wanakuheshimu. Hizo Data zinaonesha ni za mwaka 2000 hadi 2011 . Unajua hakika kua wakati huo JP Magufuli alikuwa hajakuwa Raisi. Inakuwaje hizo Pongezi huzipeeki kwa wanaohusika? Au tuseme ni Propaganda au ni upotoshaji a maksudi?
 
Mkuu Tirampulaizesheni, kiukweli issues za data analysis ni moja ya maeneo magumu sana kwa sisi Watanzania, na sio data analysis tuu bali hata news analysis.
Kwenye data collection, kuna kitu kinaitwa comparative analysis, japo hizo data kwa Tanzania zmekuwa collected 2000-2011, data hizo zingechakatwa kwa mwaka huo, ungekuta labda wala Tanzania haikuongoza, lakini kwa data hizo hizo kwa ripoti ya 2019 sasa ndio Tanzania inaongoza dunia!. The report ni ya mwaka huu 2019.
P
 
Namuheshimu sana mleta Uzi.......ila kwa hili hapana.....kama upo dasalama tu sawa ila jaribu kutoka eneo na ufike interior of Tz utaona hali halisi ya WaTz
 
Huyu jamaa hajatembea mikoani aangalie watoto wakiokota ukoko majalalan ili nafsi imsute aje kufuta uzi wake huu kuna watanzania wenzetu wanaishi maisha ambayo hayaelezeki jamani acheni kusifia kila jambo jamani Daaah
Namuheshimu sana mleta Uzi.......ila kwa hili hapana.....kama upo dasalama tu sawa ila jaribu kutoka eneo na ufike interior of Tz utaona hali halisi ya WaTz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka P. Ni sawa date of publication ni 2019 na ni sawa pia data ni ya 2000-2011. Tatizo linakuja pale unaposema au unapojaribu kusema huo ndio ukweli kwa mwaka huu wa 2019. Ili iwe kweli basi lazima kuwe na njia ya kufanya prediction kutumia hiyo data kutoka data collection time to the current time. Wewe kama mleta uzi ulitakiwa ujiridhishe kwamba kitu kama hicho kimefanyika vinginevyo ulitakiwa uwatahadharishe wasomaji wako kuhusu ukweli huo. Sasa wewe ulivyoiweka inaonyesha kama mambo hayo ni kweli kwa 2019 na bahati mbaya hata kama ni kweli hiyo haikuwa awamu ya Magufuli. Hapo ndio umejipalia mkaa.

Ningekuwa wewe badala ya kuwalaumu watanzania nige reflect, na kama wako sawa basi hakuna ubaya kujisahihisha au kukubali umekosea. Ukishupaza shingo hii itakula kwako kama mtu mwenye heshima zake hapa JF. Wish you all the best in this.
 
aisee HUNA AKILI WEWE! pumbavu kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…