Post zingine bwana...Au ndio vyakula vya skukuu vinaanza kutoka mwilini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Post zingine bwana...Au ndio vyakula vya skukuu vinaanza kutoka mwilini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli kunahitajika elimu kwa Watanzania kusoma ripoti. Mwaka 2000-2011 was the data collection period, unaweza kukuta kwa data hizo, kwa mwaka huo, wala Tanzania haikuongoza. Date of publication ndio hii ya Dec, 2019. Hii maana yake Tanzania ndio inayoongoza sasa kwa ripoti ya mwaka huu.Labda kama ulitumia tamathali za sema kufikisha ujumbe tofauti na huo uliotuwekea hapa. Chapisho ni la mwaka 2019, lakini takwimu ni miaka kabla ya 2015. Maana yake, hii ni taarifa ya mwaka huu inayoelezea mafanikio ya kipindi hicho (2011-2015) ambacho kilikuwa chini ya JK kuwa Tanzania iliongoza kupunguza umasikini. Ripoti itakayokuja ndio itakayoipima serikali ya JPM.
Awamu ya MkapaMkuu Pascal Mayalla 2000 to 2011 ni utawala wa awamu gani?
Waandishi hao ni wangapi tanzania?Paschal, waandishi wa habari wenzako wanatekwa na kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.Wewe umeona uje kivyako ili kunusuru maisha yako. Hatakama ni woga, wako umevuka mipaka. Ulicho andika huku mitaani tunakiita: Sifa za kijinga.
mayalla. Wewe ni msomi na watu wengi wanakuheshimu. Hizo Data zinaonesha ni za mwaka 2000 hadi 2011 . Unajua hakika kua wakati huo JP Magufuli alikuwa hajakuwa Raisi. Inakuwaje hizo Pongezi huzipeeki kwa wanaohusika? Au tuseme ni Propaganda au ni upotoshaji a maksudi?Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.
Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.
Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778![]()
Year in Review: 2019 in 14 Charts
These charts highlight some remarkable achievements and the serious challenges that remain as we head into 2020.t.newsletterext.worldbank.org
Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.
Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.
Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.
Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.
Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.
Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Hivi suala la machacha mguuni na usafi nalo tunategemea serikali ije iwasafishe watu kweli...?
Mkuu Tirampulaizesheni, kiukweli issues za data analysis ni moja ya maeneo magumu sana kwa sisi Watanzania, na sio data analysis tuu bali hata news analysis.Hapana kwenye hili umepotosha mkuu. Ni sawa kumsifia Magufuli kwa kile alichofanya kwa kipindi cha miaka mi-nne yaani 2015 Nov -2019 Nov. Lakini kwa taarifa uliyoleta yenye jedwali linalohusu utafiti wa mwaka 2000-2011, jedwali hilo haliwezi kuhuishwa na uongozi wa 2015-2019. Sifa hizo zinakwendwa kwa Rais mstaafu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwanini tusiwe wakweli tu jamani. Kwanini usikubali tu kwamba data ni za kipindi cha 2000-2011 ila taarifa imetoka mwaka 2019 na haihusu watu ambao waliozaliwa mwaka 2012 na kuendelea.
Tunawapenda ma-Rais wetu na serikali zetu zote zilizopita na hii iliyopo, ila kuna WATU MNAJIPENDEKEZA SANA kwa serikali ya sasa na kusahau serikali zilizopita. Nadhani mnasababu tusizozijua za kujipendekeza kwenu.
PEACE BE UPON YOU!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hauhitaji kuappologize kwa yoyote yule linapokuja suala la Raisi Magufuli na mema ya nchi yetu,
😄Katika hali ya kutekwa tekwa kwenye nchi inabidi kuandika chochote ili usitiwe kwenye Noah nyeusi .
Namuheshimu sana mleta Uzi.......ila kwa hili hapana.....kama upo dasalama tu sawa ila jaribu kutoka eneo na ufike interior of Tz utaona hali halisi ya WaTz
Kaka P. Ni sawa date of publication ni 2019 na ni sawa pia data ni ya 2000-2011. Tatizo linakuja pale unaposema au unapojaribu kusema huo ndio ukweli kwa mwaka huu wa 2019. Ili iwe kweli basi lazima kuwe na njia ya kufanya prediction kutumia hiyo data kutoka data collection time to the current time. Wewe kama mleta uzi ulitakiwa ujiridhishe kwamba kitu kama hicho kimefanyika vinginevyo ulitakiwa uwatahadharishe wasomaji wako kuhusu ukweli huo. Sasa wewe ulivyoiweka inaonyesha kama mambo hayo ni kweli kwa 2019 na bahati mbaya hata kama ni kweli hiyo haikuwa awamu ya Magufuli. Hapo ndio umejipalia mkaa.Kiukweli kunahitajika elimu kwa Watanzania kusoma ripoti. Mwaka 2000-2011 was the data collection period, unaweza kukuta kwa data hizo, kwa mwaka huo, wala Tanzania haikuongoza. Date of publication ndio hii ya Dec, 2019. Hii maana yake Tanzania ndio inayoongoza sasa kwa ripoti ya mwaka huu.
aisee HUNA AKILI WEWE! pumbavu kabisa!Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P