Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Wanachonung'unikia wengi mnakujia......yaani Tanzania ni nchi tajiri na mali ni zetu sote kwa maana tumezikuta halafu mnatuambiaga sisi ndio mabosi zenu yaani nyinyi mnatutumikia sisi sasa kwanini nyinyi mko juu sana kimaendeleo ilhali sisi hatutamaniki.
 
This is too low for you Pascal. Angalao unapaswa kuimengenya taarifa kabla ya kuipost hapa. Takwimu ni zakabla ya utawala wa Awamu hii. Ndio mafanikio ni ya Tanzania lakini sio matokeo ya awamu hii.
 
Mkuu Pascal Mayalla 2000 to 2011 ni utawala wa awamu gani?
2000 - 2011 hapo nilikuwa hata sijazaliwa.
2000 - 2011 hapo nilikuwa hata sijazaliwa.
Hata kama iwe 2000-2015 abadilishe tu, aseme tunaipongeza CCM kwa juhudi za kupunguza umaskini uliotopea.
Tuisubiri na ripot ya 2015-2025.... ndiyo tuitaje hii awamu pendwa.
Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P
 
Mkuu Pascal Mayalla 2000 to 2011 ni utawala wa awamu gani?
Mini nimejiuliza kurudia rudia kule kwa kutoa sifa na angalizo alikuwa anajihami dhidi ya watu kumshushua kwa data zake mwenyewe alizo zileta. Ndiyo maana watanzania wengi hatujielewi, hakika elimu ndogo ni sumu!
Hiki kama mnaweza kutoa pongezi na kusifu kupita maelezo kiasi hicho kwa kitu ambacho kipo wazi namna hiyo, yale ambayo yanatokana na taarifa zao za kupika mnaweka kiwango gani cha sukari? Debe katika glasi??? Report ni ya kipindi cha 2000 hadi 2011. Report imetoka leo, yafaa apewe sifa Mkapa aliye anzisha TASAF na Kikwete aliye iendeleza katika kipindi hicho kilichopimwa. Utasifu vipi awamu ambazo hazikuusika? Wao muda wao haujafanyiwa tathimini! Subiri majibu ya wakati wao ndiyo ujaji hapa!.
Kweli Watanzania tu mbumbumbu, ndiyo maana wanasiasa wanatuchezesha sindimba!
 
Ripoti ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication na sio dates of data collection.
P
Najizuia kucheka. Performance inayozungumziwa ni iliyotajwa kwenye taarifa ya utafiti yaani 2000 to 2011. Impression yako ni nzuri ila haina "back up" ya utafiti kama huu
 
magufuli hana cha kuweza kupongezwa kwa kuwa ni elfu mbili mpaka elfu mbili kumi na moja KIKWETE apokee pongezi hizo wala yeye magu haingii hapo.
 
Umeniwahi Mkuu ,mimi nimeshangaa Mtu akipenda Chongo haoni wala hasikii.Kakutana tu na Report kaja huku kupongeza na kusifu.
Cha kuongezea ,ipo tofauti ya Umasikini uliotopea na Umasikini wa kawaida.
Pascal Mayalla ,punguza Joto Mkuu.
Ripoti ni ya mwaka huu!, 2019!.
Umasikini wa kawaida unaitwa poverty,
Umasikini uliotopea ni object poverty wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.
P
 
Back
Top Bottom