Pongezi sana kwenu Watanzania wa X( Twitter), Machawa wameanza kutoa milio. Endeleeni kufinya hivyo hivyo

Pongezi sana kwenu Watanzania wa X( Twitter), Machawa wameanza kutoa milio. Endeleeni kufinya hivyo hivyo

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Leo account maarufu ya Kiongozi wa machawa waliopo X ( Twitter) imeanza kutoa milio baada ya Watanzania wapenda haki wa X (Twitter) kuanza kuzi tagg account za wafadhili wa Tanzania na mashirika ya Kimataifa (Washirika wa Maendeleo) kuhusu udhalimu unaofanywa na Serikali ya Samia dhidi ya Watanzania ili wachukue hatua stahiki dhidi ya Serikali ya Samia.

Screenshot_20250621-201356_X.jpg


Napenda kuwapongeza sana Watanzania wa X ( Twitter) kwa hii movement mliyoanzisha ya kuwatagg washirika wa maendeleo wa Tanzania kwenye post zinazohusu udhalimu unaofanywa na Serikali ya Samia dhidi ya Wananchi.

Kwa mwendo huu lazima tutapata mabadiliko maana kiuhalisia na kwa hali ya kiuchumi ilivyo, Serikali ya CCM haiwezi ku survive bila Misaada na Mikopo na Wafadhili. Wanachokusanya chote kinalipa mishahara pamoja na kulipia deni la Taifa hivyo kwa namna yeyote ile hawawezi kuvumilia kuchukuliwa hatua na Wafadhili.

Rai yangu kwenu, endeleeni kufinya hivi hivi. kwenye kila post inayohusu udhalimu wa Samia na Serikali yake tuwatagg washirika wote wa Maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia, IMF, Donald Trump, Serkali ya Marekani, Umoja wa Ulaya pamoja na Balozi za Nchi za Ulaya.

Tusiache pia kuwa tagg Umoja wa Mataifa hasa Mashirika yake yanayoshughulikia haki za Binadamu pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC. Vyovyote vile lazima tupate mabadiliko kabla ya Uchaguzi na wakitukatalia mabadiliko wajiandae kukosa fedha hadi za kulipa mishahara wanajeshi na Watumishi bila kusahau kuwekewa vikwazo.

No Reforms No Election ✊️✌️
 
Back
Top Bottom