Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

A double faced person eventually forgets which mask is real......
Kumbuka,
The mirror never lies, even when people do.

Salamaleko.
 
Sasa kubagazwa hapo kuko wapi?. Au kusema ukweli ndio kuwabagaza? Hili ni tatizo la tulipofikia sasa. Ukweli unatakiwa upindishwe.

BBC wametoa kile kilichopita na vyote vipo live. Je hao polisi wanaonekane wakimgombania kumkamata ni uongo?. Je kwamba yuko gerezani ni uongo?. Kwamba Lisu alipigwa risasi akitokea kwenye shughuri za bunge ni uongo?. Kwa ujumla kipi ni uongo hivyo vyote ktk maelezo hapo?

BBC hongera sana. Tuendelee
 
MZEE MAYALA aka Njaa, pia tuwambie watu fulani hasa wale watekaji kwamba waache kuchafua serikali kwa kuteka watu pindi watu wanapokuwa wameikosoa serikali.timing ya utekaji ule ni dhahiri ni kuichafua serikali tukufu ya CCM. mf: mtu kaikosoa Ccm AU rais siku mbili au wiki moja baadaye ametekewa ,ameuawa au kupigwa lisasi ,wewe huoni kama unakuwa unaichafua serikali kwa kuihusisha na unyama ule? lakini kama utekaji ungefanywa after one month nakuendelea ,hakuna mtu angewazia vibaya serikali.
 
Nilichogundua ni kwamba hata wahuni huzeeka.
Imagine huyu ni mwanasheria na mwandishi wa habari wa muda mrefu lakini anakataa kitu ambacho kipo wazi kabisa.
Huyu eti naye ni baba na mme wa mtu,ni hasara kubwa kwa taifa kuwa na wasomi wa aina ya huyu mzee mayala
 
Mtafuteni muwakilishi mmoja aende BBC akaongee ukweli sasa
 
Sasa mjomba p.hiyo taarifa Kwa Umma,sisi tumeisikia BBC,alichokuwa anaeleza TAL nilitegemea,msemaji wa serikali angetoa hayo majibu yaliyokuwa yanatakiwa Kwa upande wa TAL Kwa ufupi ili tusubirie Hilo tamko rasmi la serikali,kuliko kutuambia tusisambaze habari zisizothibitiswa, wakati tayari BBC wamezisambaza!
 
Unafiki hauna utofauti na uchawi mkuu! Chagua Baridi ama Moto sio unakuwa vuguvugu ni dhambi kuu. Karma haijakuacha salama ndio maana hata teuzi ya kuwa diwani hawakupi. Mimi sijaona tatizo lolote kwenye ile documentary Mnafichaficha Mtaficha hadi lini Watanganyika sio wajinga tena Kazi Mnayo Mwambie huyo mama wa kambo watoto wanaitaka nyumba ya baba yao!
 
Mkuu umezeeka vibaya au uchawa unakupelekea uwe kipofu?. Nyeusi uite nyeupe?.

Kwa ninavyokujua sio kweli kwamba hujui ukweli wote ulio wazi tu kwenye hiyo documental ya BBC. Isipokuwa kwa makusudi umeamua kupotosha kwa kuhubiri usichokiamini.

BBC wametoa documental yao kwa matukio yale yale yaliyokea kiuhalisia kabisa. Lakini wewe na wenzio mmeamua kubishana na uhalisia. Na bahati mbaya hamuweki wazi wapi ni uongo wa BBC.

Hivi kwa dunia ya sasa hivi kijana gani mjinga ataendelea kuwaamini kwa kuchengesha chengesha lugha kuzigeuza geuza kama mlivyozoea?. Hayupo. Dunia imewaumbua.
 
BBC wamesema waliwatafuta wahusika upande wa pili ili kutoa ufafanuzi hawakuonyesha ushirikiano wametoa kile walichokipata, ni muda muafaka wa Msigwa kuwafuata huko huko akaonyeshe ushirikiano sasa, kuliko kujibia huku uchochoroni aende huko huko
 
P tuambie nini cha uongo walicho kisema?Ama ni kuwa proactive ama reactive?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…