Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Nilipohudhuria ibada kuanzia Alhamisi Kuu, Ijumaa Kuu mpaka Jumapili ya Pasaka nimeona jinsi viongozi wetu wa dini walivyojipanga katika kukemea maovu haya. Siku ya Ijumaa kuu, Askofu alitumia muda mwingi kukemea tabia za ushoga na ndoa za jinsia moja (sikuelewa kwanini alitilia mkazo sana), Pia siku ya Pasaka nimeona jambo hilohilo limeendelea kutiliwa mkazo.Baada ya kutulia naangalia taarifa ya habari report za makanisa mbalimbali katika kusherehekea Sikukuu hii naona makanisa mengi na viongozi wengi wa dini wote wanalizungumzia swala hili.Bila shaka walikutana katika vikao vya ndani (TEC,KKKT n.k) na kukubaliana kwa pamoja kukemea uovu huu.
Kwa hili, Nawapongeza sana viongozi wetu wa kiroho.Kuna nguvu kubwa na vita kubwa katika ulimwengu wa kiroho.Inaonekana Shetani ameamua kuongeza nguvu ili kuingiza ajenda zake na kuhalalisha maovu na kuhakikisha anashinda vita hii (Nguvu inayotumika ni kubwa mno! Wahusika ni watu wakubwa! Si wanasiasa,viongozi wa dini (wasaliti),wasanii maarufu na watu mashuhuri n.k) Hivyo bila kuongeza juhudi na nguvu, Shetani anaweza kushinda vita hii na kuigeuza dunia Sodoma na Gomora nyingine.
Kwa hili, Natoa pongezi kwa dhati.