Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!

Wazo zuri sana kama litakubaliaka.
 
Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?
Hatutakuwi kuishi kwa ndoto ya yoyote yule, tuwaulize watanganyika na wazanzibari kama wanalitaka hilo.
 
Salama ya kitu gani kwani Zanzibar iko salama kwa kuvamiwa na Tanganyika? Si mnatuuwa kila uchaguzi kulazimisha kuweka vibaraka vyenu?
 
Yaani tutaqaliwe na Zanzibar ? Bora mkoloni arudi.
Tanzania haiwezi kutawaliwa na Zanzibar, bali Tanzania ndio inaitawala Zanzibar, ila Mzanzibari anaweza kuitawala Tanzania, kama sasa hali ilivyo.
P
 
Hilo sahau km ilishindikana wakati ulopta saiv ningum sn fanya uchunguzi pande zote mbili utapata uhalisia
 
Zanzibar ni mali ya tanganyikaaa

Full stop

Ova
Tanganyika ndio mali ya Zanzibar, Mama mnae Hadi 2030 mtake mistake, na tutabadisha katiba awatawale mpaka achoke mwenyewe na hamna la kumfanya.
 
Tanganyika ndio mali ya Zanzibar, Mama mnae Hadi 2030 mtake mistake, na tutabadisha katiba awatawale mpaka achoke mwenyewe na hamna la kumfanya.
Hiyo ya kutawala hainihusu,atawale hata maisha
Ila zanzibar ni mali ya tanganyika

Ova
 
Wakati katiba ya zanzibar inaitambua zanzibar kama nchi serikali ya jamhuri ya muungano ilikua wapi hadi ilo likawezekana?.Mapendekezo yako ni kiini macho tu.wazanzibar walishajitafuta wakajipata na kamwe hawawezi kukubali kurudi nyuma.Ukitazama vizuri utagundua hakuna nchi iliyokufa bali watanganyika tulikubali kua makondoo tukalala uku wenzetu wakiamka.na kamwe hawawezi kukubali walale kwakukubali kupoteza serikali yao.Njia pekee yakupunguza hizo kero ni serikali tatu wala sio moja.Tofauti na hivyo ni porojo za kisiasa uku miaka ikienda.
 
Serikali moja haiwezi kuwa dawa kwa sababu Zanzibar itakataa. Mwalimu alisema Karume alitaka serikali moja lakini yeye alikataa kwa hofu ya kuonekana Tanganyika imeimeza Zanzibar. Kwa vile Muungano hauwezi kuwa wa kulazimisha, hiyo ya serikali moja ni DOA.

Muungano wa serikali tatu nao ni kiini macho na hauwezekani kwa sababu Zanzibar wanataka full sovereignity ambayo ni pamoja na kiti UN na kwenye mashirika mengine ya kitaifa, balozi zake ( ukiwa na kiti UN ni lazima uwe na ubalozi wako), country code yao n.k. Hawasemi sasa lakini bila shaka huko mbeleni watataka kuwa na sarafu yao. Kingine ni kuwa wanataka huo Muungano uwe wa Mkataba kuwa kila baada ya kipindi fulani unaangaliwa upya kama unastahili kuendelea kuwepo. Tanganyika nayo ikiwa na vyote hivyo hapatakuwa na Muungano maana Jamhuri ya Muungano haiwezi nayo kuwa na kiti UN, country code yake na sarafu yake. Haiwezekani kuwa na Muungano wa nchi mbili ambao serikali ya Muungano inakuwa haina meno. Itafika wakati Rais wa Tanganyika au wa Zanzibar wataweza kukataa kuchangia bajeti ya serikali ya Muungano. Aidha, serikali ya Muungano haitaweza kuingia kwenye mikataba ya kimataifa hakuna mtu anajua hatma yake baada ya muda fulani. Kuliko kupoteza muda na aina hii ya Muungano ni heri Muungano uliokuwepo uvunjwe na kila mmoja achukue fito zake. Mfumo huu unaweza kufanikiwa pale tuu ambapo serikali za Zanzibar na Tanganyika zitakuwa kama serikali za majimbo ( mifano hai ni Marekani, India, Canada, UK n.k.) na serikali ya muungano ndio itakuwa na full sovereignity ( itasimamia mahusiano yote na nchi nyingine, ulinzi wa mipaka yake, uchumi, miongozo ya kisera katika masuala ya elimu, miundombinu n.k).

Muungano wa serikali mbili ndio pekee unaweza kuwa na uhai kwa sharti kwamba Zanzibar isahau dai lao la kuwa sovereign country na ikubali kuwa ni junior partner. Hali iliyopo ya kuipa serikali usawa na serikali ya JMT sio sustainable maana kila siku watanganyika wataona wananyonywa na wazanzibari wataona wanatawaliwa na watanganyika.

Kwa matazamo wangu ni kuwa hamna muundo ambao ni sustainable bila ya pande zote mbili kutambua kuwa katika Muungano kila moja itabidi ipoteze sovereignity yake. Kama hilo haliwezekani ni bora mapema tuu tukubaliane kutengana ili kila nchi iende kivyake. Tahadhari ni kuwa tusijidanganye kuwa baada ya kutengana uhusiano wetu utabaki kama ulivyo. Tukumbuke vidonda vilivyoachwa baada ya kuvunjika kwa EAC vilichukua muda mrefu kupona. Kuvunjika kwa JMT itakuwa hivyo hivyo.

Amandla...
 
Nimependa umefanya ufafanuzi rahisi kila mmoja kuelewa!
 
Mkuu Fundi Mchundo, asante sana kwa objectivity yako kwenye hili.
P
 
mkuu bora wewe umeeleweka.
 
Mpaka pale wazanzibar watakapo amua kuukana utaifa wao maana sisi watanganyika tumeshachoka kutanga na nyika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…