Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!

Shida kubwa kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni taifa moja kukubali kujizika {Tanganyika} na kuuvaa Utanzania na wakati huo huo Wazanzibar hawataki kupoteza utambulisho wao kama Wazanzibar,hivyo kuwa na serikali moja ni ndoto za alnacha.
 
Andiko bora kabisa na Kaka mkubwa Paskali Mayalla.

Moja ya mkanganyiko wa katiba ya 1977 ni kuwa mpaka sasa katiba inatambua uwepo wa Waziri Kiongozi toka Zbar, wakati baada ya SUK iliyoasisiwa na Rais Amani Karume na Maalim Seif walikubaliana kuwa na Rais na Makamu wa Kwanza wa Rais (ambae atatoka chama cha pili kwa wingi wa kura) na Makamu wa pili wa Rais ambae kimajukumu ni kama Waziri Kiongozi.

Tungekiwa na Mahakama ya Kikatiba, ilitakiwa wanasheria ukiwemo Paskali, mfungue shauri la mgogoro wa kikatiba kwa Zbar kuvunja katiba ya JMT.

Ila sasa, kwa kuwa tunaishi kidugu na sio kisheria, acha tuendelee, ipo siku tutalimaliza na hili.

Kweli tuendelee kujipongeza kwa Muungano kufikisha miaka 60.

Weekend njema wakubwa!
 


Hali ilikuwa hivi


View: https://youtu.be/ubZNgy8EGzo?si=CFrWBie0sIEDj6Uy
 
bandiko safi sana Poti... haya ndiyo tunayotaka kusoma, sio yale ya anaupiga mwingi 🙂
 
Mkuu, P


Kwa sasa hatuna muungano ila tuna ushirika wa kihistoria kulingana na jiografia ya eneo na maingiliano ya kijamii tu.

1. No political union-reflection is the contradictory laws functional to each side
2. No security union-reflection is in the constitution
3. No real union between the two republics (Tanganyika and Zanzibar)-reflection, Zanzibar refrains from merging its cultural heritage as such directly affects the laws. Mainlanders are denied establishing permanent assets in the Isles for fear of their identity being diluted due to social integrations!!!
 
Mkuu, P
Kwa sasa hatuna muungano ila tuna ushirika wa kihistoria kulingana na jiografia ya eneo na maingiliano ya kijamii tu.
Naomba kuheshimu mawazo yako lakini muungano upo!.
1. No political union-reflection is the contradictory laws functional to each side
Muungano wetu politically ni union, wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!. Hapa hakuna contradiction yoyote!
2. No security union-reflection is in the constitution
Hatuna hitaji la muungano wowote wa security kwasababu security ni union matter, Zainzibar sio dola na haina dola!
 
Mkuu swali lako la Ikulu 2016 lilisababisha nikaipenda JF na kuwa active member, mwanzoni nilikuwa sijui hata nilijiungaje nikasema mbona JF ina watu potential hivyo, hapo katikati ulikuja ukalamba asali kidogo ukaingia na channel 10 ambayo ni ya makada pure wa CCM. Vipindi vyako vya star TV na Dotto Buledu vilikuwa bora sn tofauti na vya channel 10 ambavyo ni soft sn.
 
Ni rahisi kuvunja muungano kuliko kuunganisha nchi iwe moja.......

Kuunganisha nchi iwe moja lazima dictatorship ihusike
 
Asante. Wewe sio kama walalamikaji na wanung'unikao lakini unatoa pia suluhisho. Ni jukumu la wenye mamlaka kuyachukua na kuyatendea kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…