masterplanner
JF-Expert Member
- Oct 23, 2015
- 268
- 342
tuwape tu uhuru wazanzibar wachague, wakitaka kusepa waende tena asubuhi kabisa.Wanabodi,
Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.
Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.
Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.
Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.
Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.
Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?
Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu muungano na serikali moja.
- Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
- Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
- Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano
- Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile!
Mkuu Yesu Anakuja , umewahi kupendwa usipopenda, ukaamua kumhurumia mpendaji, ukamkubalia kumuoa ili kumsitiri, na baada ya ndoa, ukajikuta na wewe sasa unapenda, ikitokea sasa mpendaji mara anasema hakutaki tena, ungekuwa wewe, talaka utatoa?. Niliwahi kuuliza Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?tuwape tu uhuru wazanzibar wachague, wakitaka kusepa waende tena asubuhi kabisa.
Hakuridhia kwa maandishi, aliridhia kwa kauli tuu, video na audio zipo. Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?
P
Mkuu Yesu Anakuja , umewahi kupendwa usipopenda, ukaamua kumhurumia mpendaji, ukamkubalia kumuoa ili kumsitiri, na baada ya ndoa, ukajikuta na wewe sasa unapenda, ikitokea sasa mpendaji mara anasema hakutaki tena, ungekuwa wewe, talaka utatoa?. Niliwahi kuuliza Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?
Aliyeomba muungano ni Zanzibar,
Ili Tanganyika imsitiri
Tanganyika ikakubali
Tukaungana
Tanganyika ikapenda kufa, ikafa ikaoza, ikajifuta hadi jina la Tanganyika ikalifuta.
Kuna kumwacha tena huyu mwali?!.
Ni kufa na kuzikana!.
Muungano wetu adimu na adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote, milele na milele.
P
Tanzania hatuna sheria ya kura ya maoni!, serikali yetu ikitaka kufanya jambo lolote inafanya tuu bila kuwauliza wananchi wenye nchi, lakini Zanzibar, wao wanayosheria ya kura ya maoni, wakitaka kufanya jambo kubwa, wanawauliza Wazanzibari.
Tanzania ndio nchi, halafu Zanzibar ni nchi ndani ya nchi!. Zanzibar wanaweza kupiga kura ya maoni na wakaamua, tatizo ni uamuzi huo huishia Chumbe, Tanzania hatuutambui, Tanzania hatuitambui katiba ya Zanzibar, wala hatuitambui GNU!.
P.
Sio kama Zanzibar hawaitambui katiba ya Zanzibar, ni katiba ya JMT ndio haitambui katiba ya Zanzibar lakini inawatambua Wazanzibari kama Watanzania wengine wote na wana haki zote sawa sawa ikiwemo kuwa rais wa JMT.Kama Zanzibar hamuitambui Katiba ya Zanzibar , huyo Lissu na Chadema yake wanalalamika kitu gani kutawaliwa na Mzanzibari ?
kwa bahati mbaya au nzuri, kile amesema Lisu ndio kipi moyoni mwa Watanganyika wengi, ila wanaogopa tu, ila wangekuwa huru kuongea, ungeshangaa sana. hakuna mtu wa Bara anajua faida tunapata kuungana na zanzibar, given the treatement we receive from zanzibaris na faida wanazozipata wao kwetu wakati sisi kwao hatupati kitu. ni unahudumia mchepukoKama Zanzibar hamuitambui Katiba ya Zanzibar , huyo Lissu na Chadema yake wanalalamika kitu gani kutawaliwa na Mzanzibari ?
Tatizo la vijana wa kisasa wa dot com, hampendi kusoma, karibu hapa, Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?Unaweza kuweka hizo video? Kwani Zanzibar ni Mali yake hata akiridhia mtu mmoja kwa mdomo ndiyo ikubalike kisheria?
Tatizo la vijana wa kisasa wa dot com, hampendi kusoma, karibu hapa, Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?
P
kwa bahati mbaya au nzuri, kile amesema Lisu ndio kipi moyoni mwa Watanganyika wengi, ila wanaogopa tu, ila wangekuwa huru kuongea, ungeshangaa sana. hakuna mtu wa Bara anajua faida tunapata kuungana na zanzibar, given the treatement we receive from zanzibaris na faida wanazozipata wao kwetu wakati sisi kwao hatupati kitu. ni unahudumia mchepuko
kwanza mnapata exposure ya alimu,Kwani Wazanzibari wanapata faida kwa kuuliwa ndugu na jamaa zetu kila uchaguzi kulazimisha kuweka vibaraka vyenu?
kwanza mnapata exposure ya alimu,
pili, mnaajiriwa bara ili kulisha watoto wenu.
mnaruhusiwa kumiliki ardhi yeyote mpendayo.
mnateuliwa vyeo serikalini huku bara.
mnakopa ila sisi tunawalipia wakati mna TRA yenu.
vipi,niendeleee?
ndio tunataka muondoke ili mkaishi peke yenu huko zanji. muondoke kigamboni na DSM na mikoani, mrudi tu kwenu, manake hakuna usawa. kwanza iweje kamkoa kenye watu 2m kajifanye kako sawa na nchi yenye watu 58m. haiji akilini. mmelishwa kila kitu lakini hamridhiki, ajira, ardhi everything hadi ulinzi ila hamridhiki.kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu nz wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
Wanabodi,
Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.
Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.
Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.
Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.
Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.
Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar
Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?
Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu muungano na serikali moja.
- Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
- Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
- Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano
- Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile!M
ndio tunataka muondoke ili mkaishi peke yenu huko zanji. muondoke kigamboni na DSM na mikoani, mrudi tu kwenu, manake hakuna usawa. kwanza iweje kamkoa kenye watu 2m kajifanye kako sawa na nchi yenye watu 58m. haiji akilini. mmelishwa kila kitu lakini hamridhiki, ajira, ardhi everything hadi ulinzi ila hamridhiki.
View attachment 2978448
nani ameuwa ndugu zako aisee mbona unaongea makorombwezo? haueleweki. tukisema muondoke unarukia kuwa tunauwa ndugu zako, wepi? na ninyi mbona mnatubagua tukija huko na mnaturushia mabom ya petroli?Sasa jibu swali
kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu nz wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
nani ameuwa ndugu zako aisee mbona unaongea makorombwezo? haueleweki. tukisema muondoke unarukia kuwa tunauwa ndugu zako, wepi? na ninyi mbona mnatubagua tukija huko na mnaturushia mabom ya petroli?
kama mmeuliwa mbona wewe upo hai sasa.Unajifanya kama huelewi namna jeshi linavyomwagwa wakati wa uchaguzi pamoja na Polisi na Usalama wa taifa wenu
Yule Mkuu wenu wa usalama Diwani alipiga kambi pale Government press .
nakuonyesha namna tunavyoteswa kila uchaguzi na vyombo vyenu vya ulinzi ili kuwaweka madarakani vibaraka wenu
View: https://www.youtube.com/watch?v=gmxrblkDnbc&t=19s