GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nimemuona Chama akikizungumza vizuri kweli kweli, pia nimemuona na Aucho nae akikizungumza vyema tu ila Kubwa kuliko Mtu ambaye sikutegemea kutokana na kuwa na mambo mengi Bernard Morisson nae akikizungumza vizuri tu. Hawa ni wachache sana ila najua wapo Wachezaji wengi wa Kigeni ambao kwa sasa wanakizungumza Kiswahili.
Nitoe Pongezi zangu kwa wale Wote ( Watanzania ) ambao wamefanikisha kuwafanya hawa Wachezaji wa Kigeni hapa Tanzania si tu wakizungumze Kiswahili bali hata ukiwatizama tu wakiwa wanakiongea utawaona pia wanakipenda sana Kiswahili chetu. Hakika kila Mtanzania popote alipo anatakiwa ajivunie kuwa na hii Lugha adhimu na inayopendwa kwa sasa Afrika.