Siyo TZ vs Kenya, hili siyo lengo la Mada yangu kwanza ni kinyume chake, ukiangalia ni tofauti ya USD 270 tu, hivyo sisi wote (TZ na Kenya) bado ni nchi masikini sana!
Ni aibu sana kwa liinchi lote hilo lenye kila aina ya raslimali kujivunia eti kila mwananchi wake ameachwa nyuma na Mkenya kwa dola 270 (Tshs 594,000), fahamu mpo hapo mlipo kwa ajili ujamaa uliwalemaza kiakili mkaishia kuwa mivivu balaa. Nchi yenu hiyo (kwanza ni muungano wa mataifa mawili) mlifaa kuwa mnachezea kwenye ligi ya juu tena kwa kuiacha Kenya mbali (kainchi ketu kadogo halafu nusu yake kame tupu).
Ukubwa wa 945,000 km za mraba, hapo inabidi uunganishe Kenya, Uganda na Rwanda ndio ulinganishe na ukubwa wa Tanzania, halafu ardhi yote yenye rotuba, hamna ukame wowote.
Nchi yenu haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.
Kwa miaka yote tangu uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km
Mataifa kama Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo yanategemea bandari yenu
Ziwa Victoria ambalo ni la tatu kwa ukubwa duniani na la kwanza Afrika, mumechukua sehemu kubwa
maziwa mengine makubwa kama Tanganyika na Nyasa na mengine madogo madogo
Mito ndio usitaje, yamejaa kotekote
Nchi yenu ndio ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika
Migodi ya almasi lukuki
Tanzanite ipo kwenu tu
Orodha ya madini ni ndefu chuma, makaa ya mawe, madini ya Uranium, madini mengi ya graphite, madini ya nickel, madini ya niobium
Nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani
Nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii
Mna gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2)
Yaani bora niishie hapo maana orodha ni ndefu mno hadi inalewesha, kuna mengi sijayataja
Lakini la kushangaza mpo bado mnatajwa kama LDC, maskini wa kutupwa, omba omba wenu wamejaa Kenya, nchi yenu pekee ndio Afrika yenye raia wake wanavuka mpaka kwenda kuwa omba omba. Uvivu uliopitliza, ni aibu sana mkifungua nyuzi kama hizi za kujifariji.